Tresor Mandala
JF-Expert Member
- Aug 20, 2010
- 43,242
- 90,420
Huyu mbunge ana akili nzuri
Ajengewe sanamuHuyu mbunge ana akili nzuri
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ameeleza kukasirishwa kwake na utaratibu usiofaa wa ukamataji wa magari kwenye maegesho yasiyo rasmi ‘wrong parking’, sasa ameelekeza kuitishwa kikao cha pamoja baina yake, Wakurugenzi wa Halmashauri na TARURA ili kupatia ufumbuzi.
RC Makalla amefikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko mengi ya Wananchi juu ya utaratibu mbovu unaotumika na kusema Kama kiongozi hawezi kuruhusu jambo hilo liendelee.
RC Makalla amesema amebaini pia baadhi ya Vijana wanaofanya kazi hiyo wamekosa weledi na busara na wengi wao wamekuwa wakivizia Mtu afanye kosa ili wamuadhibu badala ya kutoa elimu ili makosa yasifanyike.
Makalla amesema hayo wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Jengo la utawala la Manispaa ya Ubungo na kuipongezea Manispaa hiyo kwa usimamizi mzuri wa fedha za Serikali na kuwataka Watumishi kutoa huduma bora kwa Wananchi.
RC Makalla ameipongeza Manispaa hiyo kwa ukusanyaji Mapato jambo linalopelekea waanze kutekeleza miradi kwa fedha za ndani na pia kutumia Force Account kukamilisha miradi iliyokuwa ikisuasua ikiwemo Jengo hilo la utawala. View attachment 1865345View attachment 1865346View attachment 1865347
Ajengewe sanamu