“Idadi ya Watu wanaosafiri na Ndege za ATCL baada ya kufufuliwa imeongezeka kutoka abiria 4000 hadi Elfu 60 kwa Mwezi , hivi karibuni anga likifunguliwa vizuri, safari za Kimataifa zitaongezeka” ———Rais Samia
“Shirika limeanza kufanya huduma za viwanjani na kutayarisha vyakula kwa ajili ya ndege zake, Shirika linaweza pia kufanya matengenezo madogo na makubwa ya Ndege hongereni sana”——-Rais Samia
“Nimefurahi kuona miongoni mwa Marubani, wanne ni Wanawake na nashuhudia hili kwasabau wananirusha hata kwa Safari za Kimataifa na naambiwa wengine watatu wataongezeka”———Rais Samia
“Miaka mitano ijayo Serikali tumejipanga kuliimarisha Shirika la Ndege, lakini pia Sekta nyingine za usafirishaji Baharini, Barabara na Reli ili kuimarisha Sekta ya Usafirishaji, Watanzania tujipange vema ili kunufaika na fursa za usafirishaji ” ——-Rais Samia
“Nimepokea mpango kazi wa Shirika, changamoto zote za Shirika tumezipokea tutazifanyia kazi, niliombe Shirika tuzitunze Ndege hizi, tumepanga pia kununua Ndege ya mizigo “———Rais Samia kwenye mapokezi ya Ndege mpya aina ya Bombardier 8-Q400 leo Julai 30, 2021 Uwanja wa Julius Nyerere, Dar es Salaam