Makapuku Forum

Makapuku Forum

Italo Ferreira raia wa Brazil ametwaa medali ya dhahabu ya kwanza katika mashindano ya Olimpiki baada ya kumshinda Kanoa Igarashi wa Japan katika fainali ya mchezo wa ‘Surfing’ kwa wanaume.

Ferreira, ambaye alijifunza kuchezea mawimbi ya maji kupitia kwenye sanduku ambalo baba yake alitumia kuuza samaki , alishinda kwa pointi 15.14 dhidi ya Igarashi's mwenye 6.60 katika mchezo uliofanyika katika ufukwe wa Tsurigasaki , wakati Owen Wright wa Australia akishinda medali ya shaba.
Screenshot_20210727-123534_GBInsta.jpg
 
Naibu Waziri wa TAMISEMI, David Silinde ameagiza kuwa vipindi vya Dini viwe vya lazima kufundishwa katika Shule zote nchini ili kupunguza uovu kwasababu Wanafunzi ambao wanahofu ya Mungu hawawezi fanya utovu wa nidhamu kama wa kuchoma Shule.

Silinde amesema uwepo wa vitendo vingi vya Wanafunzi kuchoma moto mabweni ni kiashiria kwamba Watoto wengi hawana hofu ya Mungu “hili somo la Dini liwe lazima Mwanafunzi awe anataka au hataki ahudhurie hata kama hafanyii Mtihani ila awepo pale”
Screenshot_20210727-193308_GBInsta.jpg
 
Mbunge wa Segerea Bonnah Kamoli amesema kiasi cha Tsh. Bilioni 3 zimeongezwa ili kukamilisha kipande cha Barabara kuanzia Darajani kuelekea Barakuda, ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Jimbo la Segerea.

“Tunategemea Barabara hii kukamilika October 27, 2021, ukamilikaji wake utasaidia sana kupunguza adha kwa Wananchi hasa kipindi cha mvua”———-Bonnah

“Tunamshukuru sana Rais Samia kupitia kwa Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu kwa kutupatia pesa hizi maana zisingetolewa hii Barabara isingejengwa wakati huu na huenda ingejengwa siku za usoni”———Bonnah
Screenshot_20210727-193540_GBInsta.jpg
 
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeanzisha Mfuko maalumu wenye thamani ya shilingi Trilioni moja ambao utatumika kukopesha Mabenki na Taasisi za fedha kwa riba ya asilimia 3 ili Taasisi hizo ziweze kukopesha Sekta binafsi.

Benki au Taasisi ya Fedha itakayofaidika na mfuko huu itatakiwa kukopesha sekta binafsi kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka kitendo ambacho kutaongeza ukwasi na kupunguza riba za mikopo kwa sekta binafsi.
Screenshot_20210727-193858_GBInsta.jpg
 
Serikali ya Haiti inamshikilia, Afisa wa Ngazi ya Juu ambae alikuwa akihudumu kama Kiongozi wa Uratibu wa Usalama wakati Rais wa Nchi hiyo, Jovenel Moise akiuawa.

Jena Laguel Civil anaungana na Watu wengine zaidi ya 24, ambao wamekamatwa na polisi wakihusishwa na mauaji hayo.

Wakili wake Reynold George amekiita kitendo hicho kuwa ni cha kupandikizwa kisiasa, hata hivyo haijawa wazi Afisa huyo anashtakiwa kwa mashtaka gani hasa, ukamataji huo umefanyika wakati zaidi ya Watu 1,000 wakiwa wamekusanyika nchini humo kwa kumbukumbu ya Rais Moise

Moise aliuawa July 7, 2021 wakati akiwa katika makazi yake binafsi nje kidogo ya jiji la Port au Prince.
Screenshot_20210727-194046_GBInsta.jpg
 
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imepunguza kiwango cha sehemu ya Amana za Mabenki kinachotakiwa kuwekwa Benki kuu, hatua hii ni kutoa msukumo mkubwa wa kuongeza kasi ya mikopo kwa sekta binafsi na kupunguza riba na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, hii ni sehemu ya hatua tano za kisera ambazo BOT wamezitaja leo ili pia kuweka mambo sawa kutokana na janga la Corona kuathiri shughuli za kiuchumi.

Gavana wa Benki Kuu Prof. Florens Luoga amesema nafuu hii itatolewa kwa Benki itakayotoa mikopo kwa sekta ya kilimo kulingana na kiasi cha mkopo kitakachotolewa ambapo Benki itakayonufaika itatakiwa kutoa mikopo kwa sekta ya kilimo kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka.

Hatua nyingine ambayo imechukuliwa na BOT ni pamoja na kulegeza masharti ya usajili wa Mawakala wa Benki ambapo imeondoa sharti la uzoefu wa kufanya biashara kwa angalau miezi 18 kwa Waombaji wa biashara ya Wakala wa Benki na badala yake Waombaji wa biashara ya Wakala wa Benki watatakiwa kuwa na kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho cha Taifa.

Profesa Luoga amesema hatua hii itachangia kuongeza fedha katika Mabenki kutokana na ongezeko la amana na kupunguza riba za mikopo.
Screenshot_20210727-194242_GBInsta.jpg
 
Baada ya mijadala mbalimbali Nchini Tanzania kuhusu chanjo ya virusi vya corona, leo kwenye Clouds 360 ya Clouds TV Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR) Profesa Yunus Mgaya ameongea haya.

“Kitu chochote kinachoitwa dawa kina athari lakini kinachoangaliwa ni faida unayopata zikilinganishwa na athari hasi au risks, faida ikiwa kubwa kuliko athari inaweza kutumika"

"Walipoanza kuchanja kulikuwa na ripoti baadhi ya Watu kulingana na miili yao kupata damu kuganda, idadi ilikuwa katika Watu 1,000,000 ni Watu 4 tu wanaathirika, kwa asilimia ni 0.0004%, ukiambiwa asilimia ya wanaoathirika na aspirin inaweza kuwa kubwa zaidi"———Prof Yunus Mgaya.
Screenshot_20210727-194423_GBInsta.jpg
 
Baada ya mijadala mbalimbali Nchini Tanzania kuhusu chanjo ya virusi vya corona, leo kwenye Clouds 360 ya Clouds TV Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR) Profesa Yunus Mgaya ameongea haya.

“Chanjo imetokomeza baadhi ya magonjwa hapa ulimwenguni, Ndui ilikuwepo na ilisambaa sana, polio, surua tunakaribia kuitokomeza kabisa na TB sasa hivi Watoto wakiwa wadogo wanapewa chanjo , chanjo ina ushahidi wa kihistoria wa kudhibiti magonjwa kwa mpaka 100%"

"Virusi vikiwa kwenye mapafu inakuwa shida sana (kujifukiza haisaidii) ila virusi vikiwa sehemu za kichwani kupitia mvuke wa kujifukiza inasaidia sana mgonjwa kupata unafuu ndio hiyo wanaiita kupiga nyungu" ——— Prof. Yunus Mgaya.
Screenshot_20210727-194552_GBInsta.jpg
 
Baada ya mijadala mbalimbali Nchini Tanzania kuhusu chanjo ya virusi vya corona, leo kwenye Clouds 360 ya Clouds
TV Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR) Profesa Yunus Mgaya ameongea haya.

“Kama alivyosema Rais Samia Suluhu Hassan hatuishi kwenye Kisiwa, sisi ni sehemu ya kijiji kinachoitwa Dunia na Ulimwengu sasa uko so connected hivyo huu ugonjwa wa Uviko-19 umetapakaa Nchi zote zinazotuzunguka”

“Katika Afua namna ya kudhibiti ugonjwa huu kuna Afua moja tu ambayo ina ushahidi wa kisayansi ni chanjo (vaccine)”

“Suala la kupatikana chanjo kuwa la muda mfupi wala isilete wasiwasi kwa sababu ya teknolojia, imeendelea mno na teknolojia inaendelea kuboreshwa, hata hizi chanjo naamini miaka inavyozidi kwenda na teknolojia ya hii chanjo itaongezeka"——— Prof Yunus Mgaya.
Screenshot_20210727-194707_GBInsta.jpg
 
"Chama Cha Mapinduzi kinafutilia kwa makini mienendo ya baadhi ya Viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha Umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu na maadili ya Chama”

“CCM inawakikishia Wanachama na Watanzania kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote ambao wanatumia nafasi iyo kusukuma ajenda zao binafsi, kwa mujibu wa Katiba, kanuni za maadili na uongozi za CCM" ——— Shaka Hamdu Shaka Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi.
Screenshot_20210727-194842_GBInsta.jpg
 
"Ndugu Askofu Josephat Gwajima anahamasisha Wananchi wasiende kuchanjwa, ni utovu wa nidhamu kwanza kwa Serikali lakini pili kwa Chama cha Mapinduzi na lazima atambue kuwa dhamana aliyopewa ni dhamana ya CCM hivyo sisi kama Vijana wa Chama cha Mapinduzi tunalaani vikali kauli zile na tunakiomba Chama chetu kwamba Viongozi wa namna hiyo wachukuliwe hatua kali za kinidhamu"——— Kenani Kihongosi Katibu Mkuu UVCCM.
Screenshot_20210727-195053_GBInsta.jpg
 
Rais Samia Suluhu leo July 27, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika (Africa CDC), Dkt. John Nkengasong Ikulu Dar es salaam.

Dkt. John amempongeza Rais Samia kwa hatua anazochukua kukabiliana na Covid 19 na kusema Africa CDC inaunga mkono juhudi hizo za Serikali ya Tanzania katika mapambano ya Corona.
Screenshot_20210727-195210_GBInsta.jpg
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema makato ya simu za mkononi yaliwekwa kwa nia njema, lakini baada ya malalamiko ya wananchi tayari kamati maalumu ya kufanya mapitio kuhusu jambo hilo imeundwa na itatoa taarifa yake siku za karibuni.

Kamati hiyo inaongozwa na Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba, na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Faustine Ndugulile.
Screenshot_20210727-195338_GBInsta.jpg
 
Kufuatia kuadimika kwa mbolea nchini Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani amewatoa hofu wakulima nchini akieleza kuwa tayari Serikali imefanya jitihada za kuhakikisha kuwa mbolea kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo itapatikana kwa bei nafuu na elekezi.
Screenshot_20210727-195617_GBInsta.jpg
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaapisha mabalozi wateule 13 Ikulu jjijini Dar es Salaam, huku akiwaeleza kuwa watanzania wanaimani nao hivyo wakachape kazi na kuhakikisha wanaiwakilisha nchi kwa weledi mkubwa.
Screenshot_20210727-195716_GBInsta.jpg
 
Viongozi wa umoja wa dini mbalimbali umesema msimamo wao katika mapambano ya ugonjwa wa Covid-19 ni kusikiliza sauti za wataalamu na wanasayansi ikiwemo maamuzi ya chanjo ya kupambana na ugonjwa huo.

Kauli ya viongozi hao imekuja siku chache baada ya chanjo zaidi ya milioni 1 za Covid - 19 kuwasili nchini, huku Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuzindua chanjo hiyo kesho kwa kuchanjwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Screenshot_20210727-195829_GBInsta.jpg
 
Wananchi wamegawana nyama ya fisi aliyeuawa baada ya kukwepa risasi zaidi ya arobaini mkoani Tabora.

Fisi huyo aliyeua mtoto wa mwaka mmoja na nusu baada ya kuvamia nyumba katika Kijiji cha Kangeme wilayani Kaliua alijeruhi pia watu watatu ambao inaelezwa wanaendelea vizuri.

Diwani wa kata ya Zugimlole, Ramadhan Balikeka amesema kuwa wananchi waligawana nyama na haelewi walienda kufanya nini.

"Watu baada ya fisi kuuawa walidai watamshughulikia na kuchukua nyama huenda walienda kuila,"amesema.
Screenshot_20210727-195945_GBInsta.jpg
 
Mwanamuziki wa Marekani wa R&B R. Kelly amekabiliwa na shutuma mpya za kumdhulumu kimapenzi mvulana mwenye umri wa miaka 17 .

Waendesha mashtaka wanadai mwimbaji huyo alimnyanyasa kijana huyo baada ya kukutana naye huko Chicago katika mkahawa wa McDonald's mnamo 2006.

Wanataka ushahidi wa dhulma hizo na uhalifu mwingine unaodaiwa kutekelezwa naye ambao hakushtakiwa ujumuishwe katika kesi ya Kelly mnamo Agosti.Kelly anakanusha kumnyanyasa mtu yeyote, na mawakili wake hawajajibu madai haya ya hivi karibuni.

Mshindi huyo wa tuzo ya Grammy, ambaye jina lake halisi ni Robert Kelly, anatarajiwa kushtakiwa New York mwezi ujao kwa mashtaka yakiwemo unyanyasaji wa kingono wa watoto,kuchukua picha mbaya za watoto, udanganyifu na uzuiaji wa haki.

Mashtaka hayo yanahusisha wanawake na wasichana sita ambao hawajatajwa majina.
Screenshot_20210727-200204_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom