Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,974
Mfahamu Janet Kainembabazi Kataaha Museveni, mwanamke anayeaminiwa kuwa na ushawishi mkubwa Uganda.
Bi Janet Kainembabazi Kataaha Museveni ni mmoja wa wake wa marais waliohudumu kwa muda mrefu katika wadhifa huo nchini Uganda, kutokana na mume wake Yoweri Kaguta Museveni kuwa mamlakani kwa muhula wa sita sasa.
Sawa na wake wa marais wa Rwanda na Burundi Janet Museveni alionja maisha ya kuwa mkimbizi kabla ya kuwa mke wa rais.
Alikimbia ghasia kufuatia mapiganao ya mwaka 1971, wakati Idi Amin alipoupindua utawala wa Milton Obote na wakati alipokuwa ukimbizini alikutana na Bw Yoweri Museveni na wakaoana.
Mnamo mwaka 1979, alirejea nyumbani nchini Uganda kutoka Tanzania ambako alikuwa akiishi kama mkimbizi na mume wake.