Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na kusomewa mashtaka mawili ikiwemo la ugaidi.

Mbowe amefikishwa katika Mahakama hiyo leo July 26, 2021 na kusomewa mashataka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Tulimanjwa Majigo amesema kuwa Mbowe anaunganishwa na Washtakiwa wengine watatu waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka mengine yote ya ugaidi wanayodaiwa kuyatenda mwaka 2020.

Katika kosa la kwanza Mbowe anadaiwa kula njama ya kutenda kosa ambapo anadaiwa kula njama hiyo kati ya Mei na Agosti 2020 akiwa katika Hoteli ya Aishi Mkoani Kilimanjaro, kosa la pili la Mbowe ni kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili ugaidi kinyume cha sheria ya ugaidi kati ya tarehe hizo tajwa.

Baada ya kusomewa maelezo Mbowe hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka, kesi imeahirishwa hadi Agosti 5, 2021 na upelelezi umekamilika ambapo zinasubiriwa nyaraka ili ihamishiwe Mahakama kuu.
Screenshot_20210726-185020_GBInsta.jpg
 
Box Rec imemtaja Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo Hassan Mwakinyo namba moja kwa bara zima la Afrika na namba 37 Duniani kati ya Mabondia 2,050 kwenye uzani wa Super Welter.

Baada ya taarifa hii Mwakinyo amezungumza na Ayo TV_na kusema ——— “Namshukuru Mungu na Support ya Watanzania wote na Menejimenti yangu, nimefurahi kwakuwa ni sehemu ya kuona kwamba nipo njiani kutimiza ndoto au safari ninayoiwaza kutokana na vikubwa vinavyozidi kutokea, naamini kupanda kwa rank huku kuna vichocheo vingi zikiwemo Dua za wote wanaonitakia kheri”

“Imekuwa sehemu ya faraja kwangu naamini kuwa namba moja Afrika sio kitu kidogo, sio kila Bondia anaweza kufika na pia sio sifa ya mimi kufika ila naamini ni wakati ambao Mungu ametaka nifike kutokana na jitihada na nguvu nilizowekeza katika kazi yangu” ——— Mwakinyo.
Screenshot_20210726-185310_GBInsta.jpg
Screenshot_20210726-185331_GBInsta.jpg
 
“Kauli ya Askofu Gwajima kuhusu chanjo na dhamira ya Serikali kuleta chanjo nchini haikubaliki, ni hatari kupotosha Watu wanaotuamini kuhusu mambo ambayo hatuna utaalam nayo” asema Mbunge wa Bumbuli January Makamba.

“Mjadala kuhusu usalama wa chanjo ni sahihi lakini kiapo kwamba Serikali imeileta kuwadhuru Watu si sahihi” ——— January

January Makamba ameandika hayo kufuatia Askofu Josephat Gwajima ambae ni Mbunge wa Kawe kupinga kitendo cha Serikali kukubali kupokea chanjo ya Corona kwasababu ya kile alichokiita ni mpango wa Mataifa ya nje kuwaangamiza Watanzania na kusema ambao wanaipigia chapuo chanjo hiyo wameshakula hela za watengenezaji wa chanjo hiyo.

“Naomba watanzania wenzangu tusikubali kuchanjwa kwa sababu chanjo hii hatuna uhakika na usalama wa chanjo hiyo, Mimi nina akili timamu ukiona napinga hii chanjo ujue haiko salama"——— alisema Askofu Gwajima. View attachment 1869275View attachment 1869277
Gwajima yupo sahihi kwa asilimia zote...
 
Anna Mghwira, Mgombea Urais wa ACT Wazalendo mwaka 2015 na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliyepita, amezikwa leo Makumira Wilayani Arumeru, Arusha ambapo Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu alifika kumuwakilisha Rais Samia, Watu na Viongozi mbalimbali pia walihudhuria.
Screenshot_20210727-115936_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ametolea ufafanuzi taarifa zilizosambaa kwamba amesitisha shughuli za harusi Mkoani humo ili kujiepusha na maambukizi ya virusi vya corona.

Kunenge amesema hajazuia Watu kufanya harusi ila amewashauri Wananchi kuwa kutokana na uwepo wa wimbi la tatu la Corona kwa wale watakaoona wanaweza kuahirisha harusi au kusogeza mbele sio mbaya ili kujikinga wao na Ndugu zao lakini kwa atakayeona anataka kufanya harusi afanye ila kwa kuzingatia kuchukua tahadhari zote za kujikinga na coron wakati wa sherehe.
Screenshot_20210727-120117_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amewataka Wananchi wanaokwenda kuwaona Wagonjwa katika hospitali zote za Mkoa wa Dodoma kutakiwa kuvaa barakoa ili kujikikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

"Unakuja kumuona Mgonjwa huna barakoa hatutakuruhusu kumuona kwa hiyo ili umuone kwenye eneo la kutoa huduma ndani ya Dodoma, kiwe kituo cha afya, zahanati, iwe hospitali ya Serikali au binafsi ili uruhusiwe kumuona mgonjwa au kupeleka chakula tunakuomba uwe umevaa barakoa”

“Ni kwa faida yako kujikinga lakini pia ni kwa faida ya mgonjwa unayeenda kumuona"
Screenshot_20210727-120321_GBInsta.jpg
 
UNAAMBIWA

Swala Dume ana uwezo wa kuwa na majike zaidi ya 20 ndani ya kundi moja kwa nia ya kuzaliana ila ili kuweza kuwa na kundi kubwa kama hilo ni lazima aweze kuwashinda wenzie katika ugomvi na yule anayeshindwa anarudi kujiunga na kundi la wasio na majike (bachelor group) ambao huwa hawachezi mbali na kikundi hiki cha dume mmoja na majike wake, wakisubiri azidiwe nguvu ili waweze kupambana naye tena na atakayeshinda atachukua majike.
Screenshot_20210727-120536_GBInsta.jpg
Screenshot_20210727-120556_GBInsta.jpg
 
UNAAMBIWA

Baadhi ya Jamii Uchagani huzingatia kukata (kuiondoa) ncha ya mambo (mti wa kuchomea nyama) baada ya kumaliza kuchoma nyama wakiamini kwamba kwa kufanya hivyo kunamzuia Mtu yeyote mwenye nia mbaya ikiwemo ya kishirikina kuwadhuru waliokula nyama iliyochomwa kwa kutumia mambo hiyo.
Screenshot_20210727-120802_GBInsta.jpg
 
UNAAMBIWA

Utafiti wa Maastricht University unaeleza kwamba pombe inasaidia kumfanya Mtu aongee lugha ya kigeni kwa kujiamini zaidi au kuongea bila kuogopa tofauti na ambavyo ingekua kabla hajanywa.

“Watu wengi tuliowafanyia utafiti walijifunza kwa haraka kuongea lugha za kigeni na kuziongea baada ya kunywa glass kadhaa za wine waliweza kuongea vizuri hata wakati ambapo waliamini hawatoweza”
Screenshot_20210727-121045_GBInsta.jpg
 
UNAAMBIWA

Ndege aina ya Shashi (oxpeckers) maarufu pia kama Askari wa Faru wanapendwa na Wanyama kama Nyati, Faru, Twiga na wengine sababu huwala kupe wanaowasumbua kwenye ngozi zao na pia wakati mwingine husaidia kupiga kelele kama wameona hatari na ikasaidia Wanyama kukimbia.
Screenshot_20210727-121302_GBInsta.jpg
Screenshot_20210727-121319_GBInsta.jpg
 
Miradi 17 yenye thamani ya Sh11.2 bilioni katika wilaya 17 nchini imebainika kuwa na dosari ikiwamo ubadhilifu wa fedha za umma.

Kasoro za miradi hiyo zimegundulika kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 zilizokagua na kuweka mawe ya misingi.

Hadi jana miradi 491 yenye thamani ya Sh786.9 bilioni imezinduliwa na mwenge huo uliokimbizwa katika mikoa 15 mpaka sasa.

Hilo limebainishwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Patrobas Katambi wakati wa makabidhiano ya mwenge huo kati ya Mkoa wa Singida na Dodoma yaliyofanyika katika Kijiji cha Nagulo wilayani Bahi.
Screenshot_20210727-122948_GBInsta.jpg
 
Mchungaji John Magafu ambaye alikuwa mratibu wa vipindi vya dini vinavyoandaliwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), amemuomba mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo, Fredrick Shoo kuingilia kati ili alipwe zaidi ya Sh92 milioni anazodai.

Mchungaji Magafu alisema tangu alipoondolewa kazini Agosti 30 mwaka 2010 hajalipwa stahiki zake na amebaini CCT walikuwa hawapeleki michango yake ya pensheni kwa miaka 11.

Screenshot_20210727-123057_GBInsta.jpg
 
Serikali imehimiza matumizi bora na salama ya mfumo wa mtandao, ili kuhakikisha maudhui mtandaoni yanasalia kuwa yenye manufaa kwa watumiaji wote na kuhakikisha makosa ya uvunjifu wa sheria za mtandao yanapungua.

Pia, watumiaji wamekumbushwa kutumia vema huduma hizo ili kuchagiza ukuaji wa uchumi na kuepuka matumizi ya mitandao yanayokiuka sheria za nchi, kanuni na maadili.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Pauline Gekul leo Jumatatu Julai 26, 2021 alipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA akisema matumizi sahihi na salama ya mitandao yatawezesha kufikiwa kwa malengo ya maendeleo kwa watumiaji binafsi na kuiwezesha Serikali kuongeza tija katika maendeleo ya uchumi.
Screenshot_20210727-123433_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom