“Binafsi niliwahi kuwa na msimamo wa kukataa chanjo na niliuweka wazi. Nilipopata taarifa mpya na sahihi nilikimbia kuweka wazi mabadiliko ya msimamo wangu, haswa nikihofia watu kukataa chanjo kwa kuwa tu mtu mmojawapo mwenye ushawishi kwenye jamii kakataa chanjo” ——— Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamisi Kigwangalla
“Tumerithi nchi yenye kuruhusu mijadala, ndiyo maana Askofu Gwajima anatumia haki yake ya kusema lakini ukiwa na maadili kidogo tu na ukajua nafasi yako kwenye jamii, utajitenga na uongo na kusimama na ukweli, kwa sasa utajua ukiwa una ushawishi basi utashawishi watu vibaya”
“Askofu Gwajima afanye uungwana azitafute makala za kisayansi asome kwa kina juu ya chanjo; na kama ana mashaka na sayansi yake atafute wataalamu wampe shule ya chanjo. Hata mimi Mbunge mwenzake nimesoma soma kidogo, niko tayari kumfafanulia maeneo kadhaa na kumuondoa shaka”
“Kwenye dunia ya sayansi na usomi, Kama ilivyo kwenye maisha ya kawaida, watu hubadili misimamo kutokana na kupata taarifa mpya, na sahihi zaidi; na ndiyo maana kila siku tunafanya tafiti na kujifunza, na kuboresha. Ndiyo maana leo kuna iPhone 12! misimamo haiwagi kama jiwe”
“Kama ambavyo mimi nilibadili msimamo wangu juu ya Chanjo baada ya ujio wa taarifa mpya za kisayansi juu ya usalama na uwezo wa chanjo, ndivyo ninaamini hata kaka yangu Askofu Gwajima atabadili msimamo wake na kujiunga na serikali kuhamasisha tutumie chanjo kujikinga” ——— Hamisi Kigwangalla.