Zaidi ya Watu laki moja wameandamana nchini Ufaransa kupinga hatua za hivi karibuni za Serikali za kuwashinikiza Watu kwenda kuchanjwa chanjo ya Corona, Serikali inalenga kuzuia maambukizi ya virusi vipya aina ya Delta vinavyosambaa haraka.
Huko Paris, maandamano tofauti ya mrengo wa kulia na mrengo wa kushoto yametawala sehemu tofauti za Jiji, kuanzia Strasbourg Masharimi, Lille kaskazini, Montpellier kusini na kwingineko.
Maelfu ya Watu wameitiki wito wa kuandamana kutoka kwa Mwanasiasa wa mrengo wa kulia Florian Philippot, Mpambe wa zamani wa Marine Le Pen ambaye alitangaza mapema mwezi huu kwamba atawania Urais katika uchaguzi wa mwaka 2022.
Waandamanaji wamelaani uamuzi wa Serikali uliotolewa siku ya Jumatatu kufanya chanjo ya lazima kwa Wafanyakazi wote wa huduma za afya, na Mtu kutakiwa awe na cheti cha kuthibitisha hana Corona au umechanjwa kikamilifu ili kuingia migahawa na maeneo mengine ya umma.
View attachment 1858277View attachment 1858278View attachment 1858281