Makapuku Forum

Makapuku Forum

M A B I N G W A

Simba NguvuMoja
Screenshot_20210718-225542_GBInsta.jpg
Screenshot_20210718-225602_GBInsta.jpg
 
Kesi ya muda mrefu ya rushwa inayomkabili Rais wa zamani wa Afrika Kusini aliyeko jela Jacob Zuma itaendelea leo kwa njia ya video licha ya vurugu kali ambazo zimelikumba taifa hilo.

Zuma anakabiliwa na mashitaka 16 ya ulaghai na rushwa kuhusiana na ununuzi wa ndege za kivita mwaka 1999, boti za kushika doria na vifaa vya jeshi kutoka kwa kampuni tano za kijeshi Ulaya wakati akiwa Naibu wa Rais.

Anatuhumiwa kupokea hongo kutoka kwa moja ya kampuni hizo, Thales ya Ufaransa ambayo ilishitakiwa kwa rushwa na utakatishaji pesa.

Kesi hiyo ilianza May 2021 baada ya kuahirishwa na kucheleweshwa mara nyingi, wakati timu ya utetezi ya Zuma ikipambana kutaka mashitaka hayo yafutwe ambapo Zuma mwenye umri wa miaka 79 anasisitiza hana hatia huku Kampuni ya Thales pia ikikana tuhuma hizo.
Screenshot_20210719-150058_GBInsta.jpg
 
Serikali ya Tanzania itaokoa Bilioni 33 kwa mwaka kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Kiwanda cha dawa na Vifaa tiba kinachojengwa kwenye Mkoa wa Njombe, amesema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Dorothy Gwajima baada ya kutembelea kiwanda hicho Idofi-Makambako.

"Hapa nimeangalia takwimu zako Mkurugenzi tunapoenda kukamilisha kiwanda hiki cha mipira ya mikono (gloves), dawa za vidonge (tablet), vidonge vya rangi mbili (capsules) na dawa za maji (Syrup) Serikali kwa mwaka inakwenda kuokoa Bilioni 33 ambazo zingehitajika kununua mahitaji hayo"

Amesema Serikali ingehitaji Bilioni 33 zaidi ili kwenda kununua dawa na vifaa hivyo sehemu nyingine ndani au nje ya Nchi lakini hizo Bilioni zinazoenda kuokolewa tunakua tumeshazalisha kwa gharama za uzalishaji kwa mwaka Bilioni 15 ina maana hii Bilioni 33 inayobaki ukigawanya kwa milioni 700 ambayo ndio gharama za kujenga vituo vya afya na vifaa vyake kwa 'force account' ni sawa na kujenga vituo vya afya 43"
Screenshot_20210719-150345_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon nikk wa pili ametangaza kukamilika kwa maktaba ya TEHAMA kwenye Shule ya Sekondari Jokate Mwegelo kwa hisani ya mfuko wa P4R chini ya TAMISEMI na Wadau wengine kama Vodacom Foundation Tanzania.

DC Nickson aliandika "Rais wetu Samia Suluhu ana nia ya dhati katika kuhakikisha elimu yetu inajikita kwenye kutoa ujuzi, jambo hili limeelekezwa pia kwenye Ilani ya CCM, kwamba ujenzi wa uchumi unategemea watu wenye ujuzi na maarifa"

DC Nickson aliongezea pia kwamba Wilaya hiyo imetenga bajeti kujenga maktaba za TEHAMA kwenye Shule 9 za Sekondari "kwa mipango ya namna hii tunaamini elimu yetu inajenga vijana wenye ujuzi wa kutosha"
Screenshot_20210719-150507_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amerejesha shilingi milioni 85.4 (85,463,848) ambazo Wananchi waliporwa na Watu au Taasisi mbalimbali kinyume cha sheria na kisha Ofisi ya DC Mtatiro ikafanya oparesheni za kuokoa fedha hizo.

1. Shs 44,272,196 kati ya tzs 55,535,497.69 zimerejeshwa kwa Wakulima waliokuwa wameporwa na Vyama vya msingi baada ya Wakulima kuuza mazao kwa mfumo wa stakabadhi za ghala kisha Watumishi wasio waaminifu wa baadhi ya Vyama vya msingi kuwadhulumu fedha hizo.

2. Shs 12,000,000 kati ya 96,000,000 alizodhulumiwa Mwalimu Mstaafu Yusuph Bakari Yusuph baada ya kuwa amekopa 3,300,000 kwa Watu wawili binafsi na Taasisi moja ya ukopeshaji fedha ambapo pensheni yake ya Milioni 96 ilipoingia kwenye akaunti yake Watu hao wawili na Taasisi hiyo wanadaiwa kumteka na kumpeleka mjini kwa mujibu wa DC.

“Baadae walifanya connection Benki na kumpora Tsh. 63 Milioni huku kampuni ya ukopeshaji ikachukua milioni 33 kwa nyakati tofauti kati ya tarehe 14 - 18 Feb 2019. Mzee aliripoti polisi lakini hakusaidiwa, miaka miwili baadaye mwezi Julai 2021 Mstaafu huyo alimfikishia suala hilo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru baada ya kukwama kwenye njia nyingine na ndipo nikachukua hatua na fedha zake zimeanza kurejeshwa baada ya hao waliomuibia kukiri kuwa walimdhulumu” ——— asema DC Mtatiro.

3. “DC Tunduru pia amerejesha Shs 18,381,456 kwa Wanachama wa TUNDURU TEACHERS SACCOS baada ya kutapeliwa na Vipngozi wao, pesa hizi ni 15% tu ya pesa zote wanazopaswa kulipwa, tunaendelea na kazi ya kusimamia hadi wote walipwe fedha zote”

4. Shs Mil 10,810,186 zimerejeshwa pia kwa Wananchi wengine mbalimbali na taasisi za kukopesha pesa na watu binafsi.
Screenshot_20210719-150705_GBInsta.jpg
Screenshot_20210719-150721_GBInsta.jpg
Screenshot_20210719-150739_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom