Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais Cyril Ramaphosa wa South Africa amesema leo kuwa Taasisi za usalama Nchini humo zimewatambua watu kadhaa wanaoshukiwa kuchochea vurugu wiki hii.

Ramaphosa ameyasema hayo alipotembelea Manispaa ya Ethekwini ambayo inajumuisha mji wa bandari wa Durban, moja ya maeneo yaliyoathirika pakubwa katika wiki nzima ya uporaji ambao uliharibu mamia ya maduka na kuwauwa zaidi ya Watu 100.

Rais huyu amesema pia Wanajeshi 25,000 watapelekwa katika maeneo yenye vurugu hivi karibuni na hiyo itakua imeongeza idadi ya Wanajeshi mitaani kutoka 10,000 ambayo tayari wameshaingizwa mitaani.

Ramaphosa amesema waliochochea vurugu hizo wanasakwa na pia utulivu umeanza kurejea kwa sehemu katika mji mkuu wa kibiashara Johannesburg japo maduka mengi bado yamefungwa na operesheni katika bandari za Durban na Richards Bay zinaimarika.
Screenshot_20210716-191924_GBInsta.jpg
 
Askari Polisi wa Kenya Caroline Kagongo ambaye amekuwa akisakwa kwa wiki mbili kwa tuhuma za kuua Watu wawili wanaodaiwa kuwa Wapenzi wake wa zamani, amekutwa amefariki nyumbani kwa Wazazi wake huko Rift Valley.

Polisi wanasema Caroline alimpiga risasi mwenzake John Ogweno kisha akatorokea eneo la Juja Nairobi ambako nako alimuua Mwanaume mwingine aitwae Peter Ndwiga kwa kumpiga risasi chumbani hotelini.

Ripoti zinasema Caroline amejiua kwa kujipiga risasi akiwa bafuni kwa kutumia bastola ambayo alikuwa amejihami nayo na anayoshukiwa kuitumia kutekeleza muaji hapo awali.

Baadhi ya Watu mitandaoni nchini Kenya na maeneo mengine wamewaomba Polisi kufanya uchunguzi zaidi kuhusu chanzo cha kifo cha Polisi mwenzao huyo huku wakidai upo uwezekano kuwa aliuawa na kisha akashikishwa bastola mkononi.

Bado hadi sasa haijaewekwa wazi ukweli wa mfululizo wa matukio anayodaiwa kuyafanya, tunaendelea kufatilia.
Screenshot_20210716-192046_GBInsta.jpg
 
Majonzi yametawala Mbezi Makabe Dar es Salaam baada Msichana aiwate Grace Mushi maarufu kama Neema kudaiwa kumuua Boyfriend wake aitwae Hamis maarufu Zungu kwa kuichoma kwa petroli nyumba aliyokuwemo.

AyoTV na millardayo.com imefika eneo la tukio na kuzungumza na mmoja wa Mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni Mpangaji katika nyumba hiyo iliyochomwa moto.

"Nilikuwa nimelala nikashtuka mida ya saa 7 nilitaka kwenda chooni, nikaona mlangoni kuna uwazi kama unaingiza mwanga kwa ndani, nilivyofungua mlango nikaona moto umetanda karibia na chumba changu nikaanza kupiga kelele”

“Nikauliza kuna nini mbona moto unawaka, ndio yule Kaka Zungu akaanza kusema Mama Su nipo naungua ndani huku moto umewaka nikamuuliza kuna nini Zungu akanambia Neema kanifungia mlango, nikamwambia fungua mlango akasema siwezi kufungua”

“Ilibidi nianze kufanya ustaarabu wa kumtoa mtoto wangu, nikwambia ngoja nitoke nje niombe msaada wa Watu kuja kunisaidia maana peke yangu siwezi akanijibu sawa Mama Su fanya haraka” ——— Shuhuda.
Screenshot_20210717-152313_GBInsta.jpg
 
Ni picha kutoka kwenye eneo la tukio Mbezi Makabe Dar es salaam ambako Msichana aitwae Grace Mushi maarufu ‘Neema’ anatuhumiwa kumuua Boyfriend wake aitwae Hamisi kwa kumfungia ndani ya nyumba, kuimwagia petroli na kuichoma moto.

Tayari Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia Grace kwa tuhuma hizo na kusema alijaribu kutoroka lakini Polisi kwa kushirikiana na Wananchi wakafanikisha kumkamata.
Screenshot_20210717-152502_GBInsta.jpg
Screenshot_20210717-152519_GBInsta.jpg
Screenshot_20210717-152537_GBInsta.jpg
Screenshot_20210717-152553_GBInsta.jpg
 
Mmoja wa Mashuhuda kwenye tukio la Hamisi kudaiwa kuchomewa ndani ya nyumba na girlfriend wake aitwae Neema anaendelea kusimulia kilichotokea baada ya kugundua Hamisi kafungiwa ndani na moto unawaka.

“Nilimwambia fungua mlango akasema siwezi kufungua ikabidi nianze kufanya ustaarabu wa kumtoa mtoto wangu, nikwambia ngoja nitoke nje niombe msaada wa watu kjja kunisaidia maana peke yangu siwezi akanijibu sawa Mama Su fanya haraka”

"Nikaanza kutoka nje kukimbia naomba msaada wa Watu, nimetoka nikazunguka nikazunguka naita Watu kwa usiku ule walikuja baadhi kama watatu tu wakawa wanaangalia jinsi ya kusaidia kuhangaika hangaika hadi kuja kubomoa Zungu akawa haongei tena maana hadi watu wanafika alikuwa anaendelea kulia naungua...naungua...nisaidie majirani naungua”

“Hadi kuja kusukuma mlango tayari Zungu akawa kaacha kuongea, kwenye nyumba tulikuwa tunaishi wawili mimi na yeye(Neema/Grace).

"Baada ya hapo kuna Boda boda walikuwa wanapita tukawa tunaomba msaada watoe taarifa Polisi, Polisi wakaja wakawapigia simu FIRE ambapo wakaja wakazima moto na kufanikiwa kumtoa Zungu na hadi moto unawaka Neema hakuwepo ndani ya nyumba," amesema Shuhuda (Mama SU).
Screenshot_20210717-152732_GBInsta.jpg
 
Mahujaji wa ndani ya Saudia Arabia, leo wanaanza kuwasili katika Mji Mtakatifu wa Mecca kushiriki Hijja ya pili iliyopunguzwa idadi ya Watu kutokana na Corona.

Waumini wa ndani wapatao Elfu 60,000 ambao wamepatiwa chanjo kamili ya Corona ndio wataruhusiwa kushiriki Hijja ya mwaka huu itakayoanza kesho Jumapili.

Mwaka 2019, Waumini Milioni 2.5 wa Kiislamu kutoka kote duniani walishiriki katika Hijja ambayo ni nguzo muhimu katika dini ya Kiislamu.

Mapema mwezi huu, Wizara inayohusika na masuala ya Hijja ya Saudi Arabia ilisema kuwa inafanyia kazi viwango vya juu zaidi vya tahadhari za kiafya kwa kuzingatia janga la Covid-19 na kuibuka kwa aina mpya ya virusi.

Saudi Arabia imeorodhesha zaidi ya maambukizi 507,000 ya Covid-19 na vifo ni zaidi ya 8,000.
Screenshot_20210717-153030_GBInsta.jpg
 
Idadi ya Watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko magharibi mwa Ujerumani imepanda na kuzidi Watu 130.

Kazi ya uokoaji imeendelea kote Ulaya ambapo Watu zaidi ya 150 wamepoteza maisha katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya Ujerumani, Ubelgiji, Ufaransa, Uswisi, Luxembourg na Uholanzi.
Screenshot_20210717-153201_GBInsta.jpg
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia Grace Mushi maarufu mtaani kwao kwa jina la Neema kwa tuhuma za mauaji ya mpenzi wake Hamis Abdallah ‘Zungu’ ambaye alimmwagia Petroli akiwa ndani kisha kumchoma moto.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea Mbezi Makabe kwa Mzungu.

"Muda wa saa 8:30 usiku Mtuhumiwa huyu alimfungia ndani ya nyumba Hamis akammwagia mafuta ya Petrol na baadaye akachoma moto kitu kilichosababisha Hamisi kufariki”

“Hamis alikua ni Rafiki yake wa kiume (Boyfriend), Mtuhumiwa alijaribu kutoroka lakini Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wananchi tukamkamkata na uchunguzi umebaini kulikuwa na mgogoro mkubwa wa kimapenzi kabla kufanyika kwa tukio hili la Kikatili” ——— Kamanda ACP Muliro Jumanne Muliro.
Screenshot_20210717-153304_GBInsta.jpg
 
Idadi ya waliofariki kutokana na ghasia zinazoendelea nchini Afrika Kusini imepanda na kufikia Watu 212 kutoka vifo 117 vilivyoripotiwa awali.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Khumbudzo Ntshavheni amesema vifo vipya vimetokea katika jimbo la kusini mashariki la KwaZulu-Natal ambalo ndiyo kitovu cha machafuko ya sasa.

Hata hivyo amesema hali ya utulivu imeanza kurejea na hadi sasa zaidi ya Watu 2,500 wamekamatwa kutokana na vurugu za karibu wiki nzima zilizohusisha uporaji wa mali na uchomaji wa moto majengo ya biashara.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema vurugu hizo ambazo zimelitikisa taifa hilo zilipangwa na ameapa kuwasaka wote walihusika———“Ni wazi kwamba matukio yote haya yalichochewa, kulikuwa na Watu waliopanga na kuyaratibu”
Screenshot_20210717-153650_GBInsta.jpg
 
UNAAMBIWA

Mwanaume mmoja nchini Zimbabwe aitwaye Mark Muradzira, alipanda Milimani peke yake kwa lengo la kufunga kwa siku 40 bila kula wala kunywa chochote ili maombi yake yasikike kwa Mungu ampe uwezo wa kununua gari la kifahari aina ya Lamborghini ili amzawadie Mpenzi wake kwakuwa hilo ndilo lilikuwa gari la ndoto za Mwanamke huyo (Dream Car).

Ndugu, Jamaa na Marafiki walishtuka kutomuona mtaani na kuamua kuanzisha msako ambapo walikuja kumpata siku ya 33 akiwa hoi msituni akikaribia kufariki kwa njaa na kiu wakamuwaisha Hospitali akapona, Ndoto kubwa ya Mpenzi wako ni nini? uko tayari kufunga siku ngapi?

Babe wangu salaam zikufikie
Screenshot_20210717-153910_GBInsta.jpg
 
UNAAMBIWA

Utafiti uliochapishwa kwenye mtandao wa linkedin unaeleza kuwa kwa wastani Mtu hutumia Dakika 20,160 kwenye maisha yake kubusu (kissing), hii ni sawa na saa 336 , siku 14 ambazo ni sawa na wiki mbili….. hiko ni kipimo cha wastani lakini kuna baadhi wanaweza kuwa chini ya wastani na wengine wakawa wamezidisha kilometa unajikadiria wapi?
Screenshot_20210717-154129_GBInsta.jpg
 
UNAAMBIWA

Nchini Norway Vyuo Vikuu vya Umma vinatoa elimu bure bila kujali kama Mwanafunzi ni Raia wa Norway au anatoka nje ya Nchi hiyo, hii ni fursa kipekee ya kupata Degree na zaidi bila kulipia gharama na ni miongoni mwa sababu zinazofanya Norway iwe kivutio kwa Wanafunzi wengi wa kigeni.
Screenshot_20210717-154309_GBInsta.jpg
 
UNAAMBIWA

Maisha ya porini yana mengi sana hasa katika maumbile ya mnyama Dume na uwezo wake wa kupambana na kutunza Familia, licha ya kuwa Simba Dume wote wana nywele kuzunguka shingo kuna tofauti kubwa sana katika wingi na rangi za nywele hizo kwa Madume.

Dume mwenye nywele zenye rangi iliyokoza (dark mane) ndio Simba anayeaminika kuwa Mpambanaji na mwenye nguvu zaidi na Majike wengi hupendelea aina hii ya Madume kwani wanaamini Watoto wao watakuja kuwa na nguvu kama Baba zao na watapata Majike kiurahisi zaidi lakini pia wataweza kuishi kiurahisi porini.
Screenshot_20210717-154412_GBInsta.jpg
Screenshot_20210717-154432_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom