Makapuku Forum

Makapuku Forum

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Dr. Dorothy Gwajima amesema Watu 408 wamebainika kuwa na ugonjwa wa covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona nchini Tanzania huku 284 wakiwa katika mashine za oksijeni.

Itakumbukwa juzi July 07,2021, Rais Samia Suluhu akiwa Kibaigwa alisema ———> “Nimetazama hapa (Kibaigwa) ninaowaona Watu walioziba midomo na pua ni kidogo sana, nataka niwaambie tuchukue tahadhari zote dhidi ya maradhi ya Corona, wimbi la tatu lipo kwenye Nchi na hakuna la kuficha, tayari tuna wagonjwa kwenye Mikoa ya DSM, Arusha, Mwanza na mingine hata Dodoma kwa kiasi kidogo sana lakini wapo”

“Chukueni tahadhari hili wimbi la tatu ambalo linapukutisha wenzetu lisije kupukutisha hapa kwetu, gonjwa hili likianza kutuangusha halina kusimama linapukutisha tu”.
20210710_203905.jpg
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Charles Msonde ametangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2021 ambapo amesema Mkoa wa Singida umeongoza kwenye matokeo ya mtihani huo wa kidato cha sita uliofanyika Mei 2021 kwa ufaulu wa 73.91%.

Msonde amesema Mkoa wa Lindi kuwa umeshika nafasi ya pili ukiwa na 73.58% huku mkoa wa Mara ukishika nafasi ya tatu kwa 72.08%.

“Mkoa wa Mara umekuwa mkoa wa kwanza kuongeza ufaulu wake kwa miaka mitatu mfululizo kwa 4.80%, ukifuatiwa na Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa 4.46% na Mkoa wa Katavi ufaulu wake umeongezeka kwa 2.77%” ———Dk. Msonde.
20210710_204142.jpg
 
Rais wa Zanzibar DK. Hussein Mwinyi amewasimamisha kazi Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Wilaya za Unguja na baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi na Idara za Serikali ikiwemo Wakurugenzi wa Wizara ya Afya kwa tuhuma za wizi, kutowajibika na ubadhirifu wa mali za Serikali.
20210710_204313.jpg
 
Senegal, Umoja wa Ulaya, Marekani na Wadau wengine, jana walitia saini mkataba wa kufadhili utengenezaji wa chanjo nchini Senegal.

Hatua hiyo imechukuliwa katika wakati ambapo kuna upungufu wa chanjo na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona kutokana na wimbi la tatu la maambukizi lililokumba Bara la Afrika huku kukiwa na ukosefu wa Taasisi za kutengeneza chanjo Afrika.

Taarifa ya pamoja ya Serikali ya Senegal na Umoja wa Ulaya, imesema kuwa asilimia 95 ya chanjo zinazotumika Afrika zimeagizwa kutoka nje.

Taarifa hiyo imeongeza kwamba mkataba huo mpya wa ufadhili unanuia kuanzisha utengenezaji wa chanjo katika taasisi ya Pasteur mjini Dakar na kupunguza utegemeaji wa chanjo kutoka nje, Waziri wa masuala ya uchumi wa Senegal Amadou Hott amesema kuwa hatua hiyo itaweka msingi wa uhuru wa kimatibabu na dawa.
20210710_204413.jpg
 
Mtaalamu wa Masaji (anayewafanyia Watu massage) Julian Roddis wa Uingereza amehukumiwa miaka minne Jela kwa kosa la kutumia camera ya siri iliyofichwa kwenye saa yake kuwarekodi Wateja Wanawake waliofika kufanyiwa Masaji.

Uchunguzi umebaini kuwa ametumia miaka miwili kuwarekodi Wanawake zaidi ya 900 na amekutwa na video zaidi ya 2000 za matukio ya Wanawake tofauti wengine wakiwa bila nguo.

Mmoja wa Wateja Wanawake alifichua siri hiyo baada ya kuwa na wasiwasi na saa ya Julian na alipoenda kuigoogle akajiridhisha kuwa ni saa ambazo huwekwa camera pia.

“Baada ya kurekodi alikuwa anaunganisha camera na laptop na kuanza kuangalia”
20210710_204536.jpg
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Dr. Dorothy Gwajima amesema Watu 408 wamebainika kuwa na ugonjwa wa covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona nchini Tanzania huku 284 wakiwa katika mashine za oksijeni.

Itakumbukwa juzi July 07,2021, Rais Samia Suluhu akiwa Kibaigwa alisema ———> “Nimetazama hapa (Kibaigwa) ninaowaona Watu walioziba midomo na pua ni kidogo sana, nataka niwaambie tuchukue tahadhari zote dhidi ya maradhi ya Corona, wimbi la tatu lipo kwenye Nchi na hakuna la kuficha, tayari tuna wagonjwa kwenye Mikoa ya DSM, Arusha, Mwanza na mingine hata Dodoma kwa kiasi kidogo sana lakini wapo”

“Chukueni tahadhari hili wimbi la tatu ambalo linapukutisha wenzetu lisije kupukutisha hapa kwetu, gonjwa hili likianza kutuangusha halina kusimama linapukutisha tu”.View attachment 1848794

Serikali wakae wakijua hatutaki hizo taarifa...
 
Raia nchini Urusi wametakiwa kutokukutana kimapenzi na Wapenzi wao kwa siku tatu baada ya kupewa chanjo ya Corona, agizo ambalo limekosolewa na baadhi ya Wataalamu wa Afya na Wananchi.

Dr. Denis Grafier Mtaalamu wa Afya na Naibu Waziri wa Afya kutoka Mkoa wa Saratov amesema Watu waliopewa chanjo wanapaswa kujiepusha na vitu vinavyowapa stress na vile vinavyofanya watumie nguvu.

“Wote tunajua tendo la ndoa humfanya Mtu atumie nguvu kubwa, Watu hawashauriwi kufanya kwa siku 3, pia waepuke kutumia vodka na kuvuta sigara ili chanjo ifanye kazi vizuri”.
20210710_211829.jpg
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Charles Msonde ametangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2021 na kutaja Shule kumi bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo ambapo Shule iliyoshika nafasi ya kwanza kitaifa ni Kisimiri ya Arusha yenye Watahiniwa 72.

Msonde ametangaza matokeo hayo Visiwani Zanzibar leo ambapo amesema Shule iliyoshika nafasi ya pili Kitaifa ni Kemebos ya Kagera yenye Watahiniwa 35 huku Dareda ya Manyara yenye Watahiniwa 101 imeshika nafasi ya tatu.

Tabora Girls yenye Watahiniwa 100 imeshika nafasi ya nne ikifuatiwa na Tabora Boys yenye Watahiniwa 120 ambayo imeshika nafasi ya tano.

Nafasi ya sita imeshikwa na Feza Boys ya Dar es Salaam yenye Watahimiwa 71 ikifuatiwa na Mwandet ya Arusha yenye Watahimiwa 53 ambayo imeshika nafasi ya saba.
20210710_212006.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom