Makapuku Forum

Makapuku Forum

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipa siku saba za awali Tume aliyoiunda kuchunguza chanzo cha moto katika soko la kimataifa la Kariakoo ili kubaini nini kimesababisha au nani kasababisha moto huo.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Julai 11, 2021 alipokuwa anaongea na Wafanyabiashara na Wakazi wa eneo la Kariakoo baada ya kukagua hatua zinazoendela kuchukuliwa kudhibiti moto huo, Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kamati iliyoundwa ambayo itafanya kazi na kamati ya ulinzi na usalama iliyoanza kufanya kazi chini ya Mkuu wa Mkoa huo itajumuisha Ofisi ya Rais-Ikulu, TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo itawakilishwa na Mkurugenzi wa Maafa, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, TAKUKURU, TANESCO, Wakala wa Majengo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na DPP.

“Endapo itagundulika kama kuna Mtu alihusika kwa namna moja au nyingine, hatua kali za kisheria zitachukuliwa moja kwa moja, kitendo cha kuungua kwa soko hili la miaka chungu mzima lazima kuwe na uchunguzi wa kina, kwanini leo lishike moto”———-Majaliwa
20210711_124704.jpg
20210711_124719.jpg
20210711_124741.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipa siku saba za awali Tume aliyoiunda kuchunguza chanzo cha moto katika soko la kimataifa la Kariakoo ili kubaini nini kimesababisha au nani kasababisha moto huo.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Julai 11, 2021 alipokuwa anaongea na Wafanyabiashara na Wakazi wa eneo la Kariakoo baada ya kukagua hatua zinazoendela kuchukuliwa kudhibiti moto huo, Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kamati iliyoundwa ambayo itafanya kazi na kamati ya ulinzi na usalama iliyoanza kufanya kazi chini ya Mkuu wa Mkoa huo itajumuisha Ofisi ya Rais-Ikulu, TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo itawakilishwa na Mkurugenzi wa Maafa, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, TAKUKURU, TANESCO, Wakala wa Majengo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na DPP.

“Endapo itagundulika kama kuna Mtu alihusika kwa namna moja au nyingine, hatua kali za kisheria zitachukuliwa moja kwa moja, kitendo cha kuungua kwa soko hili la miaka chungu mzima lazima kuwe na uchunguzi wa kina, kwanini leo lishike moto”———-MajaliwaView attachment 1849512View attachment 1849513View attachment 1849514
At least hapo nawaona Garda world ambao ni private zamani Ultimate...
 
Hatimae Lionel Messi anashinda Kombe lake la kwanza na Timu ya Taifa baada ya Argentina kuifunga Brazil leo goli 1-0 lililofungwa na Di Maria dakika 22 katika michuano ya Copa America.

Messi amefanikiwa kucheza fainali nne za Copa America 2007, 2015 na 2016 zote Argentina alipoteza kabla ya fainali ya nne leo kuandika historia mpya.

Messi amefanikiwa pia kuibuka mchezaji bora wa mashindano, mfungaji bora akiwa na magoli 4 na assist 5, amechangia katika magoli 9 ya Argentina kati ya 12 yaliofungwa katika michuano hii huku akicheza dakika zote 630 za michuano hiyo sawa na mechi 7.
20210711_124926.jpg
20210711_124944.jpg
20210711_125007.jpg
 
"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”

"Kwenye chungu, ni lazima bajeti, fedha zitatoka wapi ni lazima tutoe kodi, mwaka huu tumeleta kodi ya miamala, ni vizuri sana mjue hili la kwenye miamala sio tu kodi, hili tunatunisha mfuko, ni solidarity fund, huu ni mfuko wa mshikamano wa Watanzania"

"Sisi wenzenu tunaotafsiri dira ya Rais Samia, tumesema itakuwa aibu mno kwa kizazi hiki cha leo ziwepo shughuli zinakwama sababu tu tunataka tusitoe kodi, kwamba tusubiri tuletewa wengine wanaoweza kutozana kodi kutoka Nchi nyingine, hii haileti heshima kwa Nchi yetu na wala hailindi Uhuru wa Nchi yetu, Nchi inapokuwa huru ni lazima ijitegemee"———-Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba kwenye Clouds360 ya
20210712_141950.jpg
 
"Kuna Shule zinakusanya Watoto mpaka 1500 au 1000 na Shule haina maji wanaambiwa waende Shule na kidumu cha maji, sasa tunafanyaje ili maji yapatikane? ndio maana kuna uwepo wa kukatwa Tsh. tano kila unapotuma hela kwa ajili ya huu mfuko wa mshikamano"

“Mimi naunga mkono dira ya Rais ya kutaka maji yapatikane kila kijiji, sasa tunafanyaje? tukasema tuchangishane, hivi unaona tunaweza kupoteza maisha ya Mtoto sababu ya maji, kisa unalia unakatwa Tsh.5?, mbona milio ya simu tunaweka na unakatwa Tsh. 100?"

"Akaunti zilifungwa kipindi kile kwasababu ya masuala ya kikodi na Wafanyabiashara wanarudishiwa fedha zao kwasababu akaunti imelipa kodi au hesabu zake zilipigwa vibaya kwahiyo kuna fedha ambayo haikuwa kodi inarudishwa"———Waziri Mwigulu kwenye Clouds360 ya clouds tv.
20210712_142134.jpg
 
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameongeza wiki mbili nyingine za “lockdown” kama njia mojawapo ya kupunguza maambukizi ya Covid- 19 nchini humo.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini Afrika ya Kusini.
Ramaphosa alisema kuwa shule zitaendelea kufungwa na kuendelea kuzuia mikusanyiko katika sehemu mbalimbali ikiwemo sehemu za starehe.

Huku sehemu za mazoezi na migahawa katika sehemu mbalimbali ya miji ikiruhusiwa kufunguliwa kwa sharti la wateja wao kukaa mbalimbali.
“Serikali itaongeza fedha katika mfuko wa Covid ili kufidia biashara zilizoathiriwa,” Rais alisema.

Afrika Kusini imeripoti maambukizi mapya 16,302 siku ya Jumapili yakileta jumla ya idadi ya maambukizi kuwa 2,195,599.
Jana watu 151 walifariki kwa sababu ya Covid na kusababisha idadi ya vifo kufikia 64,289
20210712_143314.jpg
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa wamekutana katika kikao cha pamoja kujadili namna wizara wanazozisimamia zitakavyotekeleza suala la mgao wa mrabaha kwa kazi za wasanii wa muziki zinazochezwa kwenye vyombo mbalimbali vya Habari.

Katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam, mawaziri hao wawili wamekutana na wakurugenzi wakuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Chama cha Hatimiliki Tanzania (COSOTA), Makatibu Wakuu wa Wizara zote mbili pamoja na wataalaam kutoka Kituo cha data cha Taifa,TCRA na wizara.

Kikao kazi hicho kimejadili na kuweka mikakati ya pamoja juu ya utekelezaji wa zoezi la kuanza rasmi kwa mgao wa mrabaha kwa wasanii, pia wamejadili na kupitia mapendekezo ya marejeo ya kanuni za maudhui mtandaoni ili kuona uwezekano wa kupunguza au kufuta baadhi ya tozo za leseni za maudhui mtandaoni.
20210712_143513.jpg
 
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameongeza wiki mbili nyingine za “lockdown” kama njia mojawapo ya kupunguza maambukizi ya Covid- 19 nchini humo.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini Afrika ya Kusini.
Ramaphosa alisema kuwa shule zitaendelea kufungwa na kuendelea kuzuia mikusanyiko katika sehemu mbalimbali ikiwemo sehemu za starehe.

Huku sehemu za mazoezi na migahawa katika sehemu mbalimbali ya miji ikiruhusiwa kufunguliwa kwa sharti la wateja wao kukaa mbalimbali.
“Serikali itaongeza fedha katika mfuko wa Covid ili kufidia biashara zilizoathiriwa,” Rais alisema.

Afrika Kusini imeripoti maambukizi mapya 16,302 siku ya Jumapili yakileta jumla ya idadi ya maambukizi kuwa 2,195,599.
Jana watu 151 walifariki kwa sababu ya Covid na kusababisha idadi ya vifo kufikia 64,289View attachment 1850488
Anaacha ku deal na waandamaji wa Zuma wanaoiba kwenye maduka, anahangaika na lockdown...
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ameruhusu kuanza kwa shughuli za biashara Kwenye soko dogo la Kariakoo Kutokana na eneo hilo kutoathiriwa na moto.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea sokoni hapo ambapo ametaka Wafanyabiashara wote wanaoendesha biashara zao eneo la hifadhi ya Barabara ya kuingia sokoni humo waondoke ili Barabara ibaki wazi.

Makalla amesema kwa wakati huu ambao hali ya usalama soko kubwa haijakaa sawa anashauri Wafanyabiashara wachukue mali zao na kuhamia Soko la Kisutu na Machinga Complex hadi marekebisho yatakapofanyika.

Kuhusu Soko la Shimoni ambalo inaelezwa halijaathiriwa kwa kiasi kikubwa na moto, RC Makalla amesema Kutokana na mfumo wa umeme sokoni humo kuharibika ameagiza ufanyike uratibu Wafanyabiashara wakachukue bidhaa zao na kuhamia Soko la Machinga Complex na Kisutu.
20210712_182847.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ameruhusu kuanza kwa shughuli za biashara Kwenye soko dogo la Kariakoo Kutokana na eneo hilo kutoathiriwa na moto.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea sokoni hapo ambapo ametaka Wafanyabiashara wote wanaoendesha biashara zao eneo la hifadhi ya Barabara ya kuingia sokoni humo waondoke ili Barabara ibaki wazi.

Makalla amesema kwa wakati huu ambao hali ya usalama soko kubwa haijakaa sawa anashauri Wafanyabiashara wachukue mali zao na kuhamia Soko la Kisutu na Machinga Complex hadi marekebisho yatakapofanyika.

Kuhusu Soko la Shimoni ambalo inaelezwa halijaathiriwa kwa kiasi kikubwa na moto, RC Makalla amesema Kutokana na mfumo wa umeme sokoni humo kuharibika ameagiza ufanyike uratibu Wafanyabiashara wakachukue bidhaa zao na kuhamia Soko la Machinga Complex na Kisutu.View attachment 1850701
Machinja complex hoyeee...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom