Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210709_065051.jpg
20210709_065105.jpg
 
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe amepata ajali ya gari leo wakati akitokea Rondo kuelekea Lindi Mjini baada ya tairi la gari kupasuka, Aliyekuwa Msaidizi wa Membe, Allan Kiluvia amesema Membe na wengine wote waliokuwemo kwenye gari wapo salama na hawajapata majeraha yoyote.
20210709_171912.jpg
20210709_171943.jpg
 
Jeshi la Polisi Arusha linamshikilia Melita Ndaletyani wa Noondoto Wilayani Longido kwa tuhuma za kumuua Kaka yake aitwae Kiseri Ndaletyani kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni.

Melita anadaiwa kufanya hivyo kwenye ugomvi uliotokana na Kaka huyo kumzuia kutaka kufanya mapenzi kwa lazima na Shemeji yake ambae ni Mke wa Kiseri.

Kamanda wa Polisi Arusha Justine Masejo amesema kifo cha kaka yake kilitokana na ugomvi uliotokea wakati akimzuia Mdogo wake kulazimisha kulala kimapenzi na Shemeji yake "Usiku wa kuamkia leo saa sita na nusu usiku Kiseri (38) ambae ni Mfugaji alifariki baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali"

"Mdogo wake Melita (34) alitaka kumuingilia kinguvu Mke wa Kaka yake, sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na upelelezi ukikamilika jalada litafikishwa ofisi ya mashtaka kwa hatua za kisheria" ——— RPC Masejo.
20210709_172120.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi kuhakikisha kuanzia sasa Mabasi yote yanashusha na kupakia abiria kwenye kituo kikuu Cha Mabasi Cha Mbezi Louis.

RC Makalla amesema hayo wakati alipotembelea kituo hicho na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za Wafanyabiashara kituoni hapo.

Amesema Serikali inatambua kituo kimoja pekee Cha Mabasi ambacho ni Mbezi na uwekezaji uliofanyika ni mkubwa hivyo hakuna maana kama kila Mmiliki wa Mabasi atakuwa na kituo chake kupakia na kushusha abiria.

RC Makalla ameelekeza uongozi wa Stendi hiyo kuweka utaratibu wa baadhi ya Mabasi kushusha abiria kwenye eneo la kulaza magari ambapo kuna Banda la Mamalishe ili kuchochea biashara.
20210709_172246.jpg
20210709_172308.jpg
 
Wanafunzi wawili, walinzi wanne na baadhi ya Wananchi wanashikiliwa na Polisi Mkoani Geita kwa ajili ya mahojiano baada ya kutokea kwa ajali mbili tofauti za moto katika Shule ya Sekondari Geita zilizoteketeza darasa lilikokuwa na vifaa vyote vya Wanafunzi wa Bweni, na maabara ya biolojia.

Usiku wa kuamkia July 06,2021 darasa moja liliteketea kwa moto kwenye Shule ya Sekondari Geita likiwa na vifaa vya Wanafunzi wa Bweni kisha usiku wa kuamkia July 07,2021 moto mwingine ukazuka na kuteketeza jengo la Maabara ya Biolojia katika Shule hiyohiyo ya Sekondari Geita.
20210709_172515.jpg
 
Shirika la Afya Duniani WHO limesema kirusi kipya cha corona kiitwacho delta kipo kwenye Nchi 10 kati ya 16 za Afrika ambazo covid 19 imesambaa kwa wingi.

WHO imesema bara la Afrika limeathirika vibaya zaidi na janga la virusi vya corona wiki hii ila hali bado itakuwa mbaya zaidi huku wimbi la tatu la maambukizi likishika kasi.

Dokta Matshidiso Moeti ambaye ni mkurugenzi wa WHO Afrika amesema maambukizi katika bara la Afrika yanaongezeka sana kila baada ya siku 18 ikilinganishwa na wakati uliopita.

Moeti amesema ongezeko hili la maambukizi halitoisha hadi baada ya wiki kadhaa ambapo katika wiki iliyoisha July 4 pekee, Afrika ilirekodi zaidi ya maambukizi laki mbili na elfu hamsini ikiwa ni ongezeko la asilimia 20.
20210709_172838.jpg
 
Watu 52 wamefariki huku zaidi ya Watu 50 wakijeruhiwa baada ya moto mkubwa kuzuka kwenye kiwanda kimoja Bangladesh.

Watu walilazimika kuruka kutoka gorofani ili kuokoa maisha yao, Ripoti kutoka eneo la tukio zinasema bado Polisi na Vikosi vya Uokoaji wanaendelea kuwaokoa wengine ambao walikuwa ndani ya jengo hilo.
20210709_173000.jpg
View attachment 1846960View attachment 1846961
20210709_173055.jpg
 
Mashabiki zaidi ya 100,000 wa England wamesaini petition ya kuomba Serikali ya Uingereza itangaze Jumatatu July 12 iwe siku ya mapumziko endapo England watachukua Ubingwa wa Euro 2020.

England wanacheza na Italia Jumapilii ya July 11 ikiwa ni mara yao ya kwanza kufika hatua ya fainali ya Euro lakini ndio wanafanikiwa kufika fainali ya michuano mikubwa kwa mara ya kwanza toka 1966 walipotwaa Kombe la Dunia.
20210709_173217.jpg
 
Shirika la Afya Duniani WHO limesema kirusi kipya cha corona kiitwacho delta kipo kwenye Nchi 10 kati ya 16 za Afrika ambazo covid 19 imesambaa kwa wingi.

WHO imesema bara la Afrika limeathirika vibaya zaidi na janga la virusi vya corona wiki hii ila hali bado itakuwa mbaya zaidi huku wimbi la tatu la maambukizi likishika kasi.

Dokta Matshidiso Moeti ambaye ni mkurugenzi wa WHO Afrika amesema maambukizi katika bara la Afrika yanaongezeka sana kila baada ya siku 18 ikilinganishwa na wakati uliopita.

Moeti amesema ongezeko hili la maambukizi halitoisha hadi baada ya wiki kadhaa ambapo katika wiki iliyoisha July 4 pekee, Afrika ilirekodi zaidi ya maambukizi laki mbili na elfu hamsini ikiwa ni ongezeko la asilimia 20. View attachment 1846955
Wazungu na mambo yao...

Kirusi kianze India kije kiivuruge Africa... waende zao huko...
 
UNAAMBIWA:

Mwaka 1954, Mwanaume mmoja nchini Marekani, John Thomas Doyle alijiua kwa kuruka kutoka juu ya Daraja hadi chini kwenye Daraja la Golden Gate, ujumbe aliouacha ulisomeka ————“sina sababu inayonifanya nijue zaidi ya kusema kwamba nina maumivu kwenye meno”
20210709_173329.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom