Makapuku Forum

Makapuku Forum

1986 - Kombe la Dunia mwaka 1986 nchini Mexico: Mechi ya robo fainali baina ya Uingereza dhidi ya Argentina inafanyika.

Diego Maradona, nahodha wa Argentina anafunga magoli mawili murua na kuitoa England kwa jumla ya magoli 2-1.

Goli la kwanza, Maradona alilifinga kwa mkono na goli hilo linajulikana kama Goli la Mkono wa Mungu.

Goli la pili, Maradona alipiga chenga wachezaji watano wa England kabla ya kufunga. Goli hili linajulikana kama Goli la Karne.

Hiyo ni moja kati ya mechi za kukumbukwa za wakati wote katika historia ya mchezo wa soka.
Ilikuwa siku kama ya leo, anyway Mussolin5 ulipotelea wapi?
 
  • Thanks
Reactions: Lee

1515​

Emperor Maximilian and Vladislav of Bohemia forge an alliance between the Hapsburg and Jagiello dynasties in Vienna.
 
Prince Conde's rebels narrowly defeat Chief Minister Mazarin's loyalist forces at St. Martin, near Paris.
 
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemteua Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Kenan Kihongosi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mpainduzi ( UVCCM) akichukua nafasi ya Raymond Mwangwala ambaye ameteuliwa kuwa DC wa Ngorongoro.

Akitangaza leo, June 22,2021 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema Kamati Kuu iliketi leo chini ya Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan.
20210622_170745.jpg
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr.Mwigulu Nchemba ametangaza majina ya Mabalozi mbalimbali wa kuwahamasisha Watanzania kulipa kodi kwa hiari wakiwemo Hamisa Mobetto, Mbwana Samatta na Edo Kumwembe.
20210622_171017.jpg
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba amesema mfumo wa ulipaji wa kodi ya majengo kwa kutumia mita za Luku haitawahusu wapangaji bali ni wamiliki wa nyumba husika.

Ametoa mfano wa ilivyokuwa kwamba mpangaji anapokuwa amelipa malipo yoyote yaliyopaswa kufanywa na mmiliki huwa anawasiliana na mwenye nyumba wake ili arudishiwe hela yake.

Amesema mambo mengine yote yatapangiliwa vizuri ili kuepusha Watu kupanga foleni ya kwenda kulipa kodi ya pango.

Katika hatua nyingine Bunge limepitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 ambapo Wabunge 361 sawa na asilimia 94 wamekubali na Wabunge 23 sawa na asilimia 6 hawakuamua kwa kutokuwa na upande wowote.
20210622_171142.jpg
 
"Kuhusu makato ya kwenye simu upande wa muda wa maongezi, jambo hili kwa kiwango fulani lilikuwa halijaeleweka, tulichopendekeza ni kwamba tumechukua takwimu za watumiaji wa simu tukaweka makundi yao, kuna watumiaji wasiopungua Milioni 8 ambao wana matumizi yao yasiozidi 1000 ambao inaenda inakua mpaka inafika wanatumia laki moja na kuendelea”

“Wenyewe sio wengi sana wako 60,000 kwa hiyo tulichokiweka kwa wale watumiaji wanaotumia viwango vya chini kwa mfano anayetumia Tsh 1000 na kwenda chini yeye atakatwa Tsh 5 na hiyo atakatwa pale anapoweka, na wale wanaotumia Tsh 7500 hadi 10,000 atakatwa Tsh 75, kwa wale wanaotumia 10,000 hadi 25000 anakatwa Tsh 112"———Dr. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango
20210622_171307.jpg
 
Idadi ya vifo kutokana na ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo ikihusisha magari matatu ambayo ni Toyota Coaster, Toyota Cresta na Lori eneo la nanenane mkoani Morogoro imeongezeka na kufikia Watu 9 kutoka Watu watano jana usiku.

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dr. Kesy Ngalawa amesema pia majeruhi watano wa ajali hiyo wapo Chumba maalum cha Uangalizi (ICU).

Mmoja wa majeruhi Frank Ramsoni amesema Toyota Coaster ilikua inatoka Dar kwenda Mbeya na Dereva aliweka mashada kwenye gari hilo kuashiria imebeba maiti ili kupata wepesi wa kufanya safari ambapo baada ya kufika eneo la Kingulwira Morogoro gari lilisimamishwa na Askari.

Dereva wa gari alishuka kisha Msaidizi wake alichukua gari na kuondoka bila ruhusa ya Askari na wakati yuko barabarani gari likiwa kasi Msaidizi alimpigia simu mwenzake aliebaki na Askari na hapo ndipo akashindwa kulimudu gari likapoteza mwelekeo na kugongana uso kwa uso na lori la Kampuni ya Dangote.

R.I.P
20210622_171515.jpg
20210622_171531.jpg
20210622_171551.jpg
 
R.I.PView attachment 1826701View attachment 1826702View attachment 1826703
Pole yao sana wafiwa...
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba amesema mfumo wa ulipaji wa kodi ya majengo kwa kutumia mita za Luku haitawahusu wapangaji bali ni wamiliki wa nyumba husika.

Ametoa mfano wa ilivyokuwa kwamba mpangaji anapokuwa amelipa malipo yoyote yaliyopaswa kufanywa na mmiliki huwa anawasiliana na mwenye nyumba wake ili arudishiwe hela yake.

Amesema mambo mengine yote yatapangiliwa vizuri ili kuepusha Watu kupanga foleni ya kwenda kulipa kodi ya pango.

Katika hatua nyingine Bunge limepitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 ambapo Wabunge 361 sawa na asilimia 94 wamekubali na Wabunge 23 sawa na asilimia 6 hawakuamua kwa kutokuwa na upande wowote.View attachment 1826692
Danganya toto ndiyo ishatoka hivyo...

Ni sawa na kwenda kudai return au VAT yake TRA utakesha...
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema kuanzia kesho Jumatano Juni 23, 2021 itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingia eneo la hospitali hiyo au kutoa huduma bila kuvaa barakoa na mgonjwa atatakiwa kuwa na msindikizaji mmoja tu.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Juni 22, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma wa MNH, Amaniel Aligaesha inaeleza kuwa hatua hizo zinatokana na maagizo ya waziri wa afya kwa taasisi mbalimbali akizitaka kuchukua tahadhari ili kujikinga na kuwakinga wananchi dhidi ya wimbi la tatu la ugonjwa wa Uviko-19 (Covid-19).

“Tunawaomba wananchi kuunga mkono hatua hizi ili kuongeza tahadhari ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huu wa Covid-19. Utekelezaji wa maelekezo haya unaanza rasmi tarehe 23 Juni, 2021 (kesho).”
“Tunawaelekeza wafanyakazi, wanafunzi, ndugu na jamaa wa wagonjwa wote wanaoingia eneo la hospitali kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji tiririka yaliyopo katika maeneo mbalimbali ya hospitali au vipukusi (sanitizer),” amesema.

Mbali na hayo MNH imeelekeza kwa wagonjwa waliolazwa wodini wataruhusiwa kuonwa na ndugu zao watano tu, asubuhi wataruhusiwa ndugu wawili, mchana ndugu mmoja na jioni ndugu wawili.

20210622_181811.jpg
 
Asante Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba kwa kuamini kwamba mimi naweza kuwa balozi wa uhamasishaji wa kulipa kodi kwa hiyari kwa Watanzania na wageni wanaokuja nchini.

Nitaifanya kazi hii kwa maslahi mapana ya taifa nikishirikiana na mabalozi wengine uliowateua Mbwana Samata na Hamisa Mobetto ....kwa pamoja TUNAJENGA TAIFA...
20210622_181938.jpg
 
Kwa moyo mkunjufu Nimepokea kwa furaha ubalozi huu wa kuhamasisha walipa kodi kwa hiyari Na Nnaahidi kushirikiana bega kwa bega na mamlaka husika katika kuhamasisha Na kuelezea faida za ulipaji kodi kwa nchi yetu.

Naamini watanzania ni watu waelewa Na haitatumika nguvu kubwa katika kuwaelewesha Na wakaelewa, pia hongera kwa mabalozi wenza my brother Edo Kumwembe pamoja Na my friend Hamisa Mobetto.

Nawasilimu kwa jina la jamhuri
Asante Mh Mwigulu Nchemba waziri wa fedha Na mipango. Wizara ya fedha Na mipango
20210622_182123.jpg
 
Ni heshima kubwa sana kuteuliwa kuitumikia nchi yangu. Ni heshima kubwa kuliko maneno ninayoweza kutumia kuielezea!

Nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai na hekima aliyoweka ndani yangu.

Nimshukuru Pia Rais wangu Mama Samia Suluhu Hassan na serikali nzima akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba kwa kuendelea kuamini vijana kwenye ujenzi wa Taifa letu!

Kwa kutambua umuhimu wa kodi kwenye uendeshaji wa miradi ya nchi na kuchagia maendeleo ya Taifa, naahidi kuitumikia vyema nafasi yangu niliyoteuliwa ya ubalozi wa uhamasishaji wa ulipaji kodi kwa maslahi ya Taifa langu, naahidi kushirikiana na mabalozi wenzangu Edo kumwembe na Mbwana samatta pamoja na viongozi na wadau mbalimbali wa masuala ya ulipaji kodi!

Mwenyezi Mungu nisaidie
20210622_182342.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom