Hatutaki hizi taarifa na hatuziamini...Wizara ya Afya Tanzania imesema imeanza kuona viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la mlipuko wa Covid 19 Tanzania, hii ni kutokana na taarifa za ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huu na mwingiliano wa Watu wa Tanzania na Watu wa Nchi jirani na Mataifa mengine Duniani katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
"Tunakuwakumbusha Watanzania wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Covid 19, na tahadhari hii ya leo ni kutokana na hali ya mwenendo wa ugonjwa wa Covid 19 Duniani na ongezeko la maambukizi Afrika zikiwemo Nchi jirani ambazo zimekumbwa na wimbi la tatu la mlipuko wa Covid 19 na maambuki yameongezaka maradufu kuliko ilivyokuwa katika wimbi la pili”
"Kwa mujibu wa taarifa kutoka WHO iliyotolewa katika jarida la wiki ya 24 inayoanzia June 07 hadi June 13, 2021 katika Kanda ya Afrika idadi ya wagonjwa imekuwa ikiongezeka kwa wiki tano mfululizo “
"Mfano katia Wiki moja iliyopita Afrika Kysini, Uganda, Zambia, DRC, Namibia, Angola n.k zimeendelea kuonesha kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa isiyoshuka huku ikiripotiwa Nchi hzio kukumbwa na anuai ya virusi vipya vinavyosababisha Covid 19 kuwa kali zaidi na kuathiri hata mkundi ya wenye umri mdogo” ———-Mkurugenzi wa Idara ya Kinga - Wizara ya Afya, Dkt. Leonard Subi
View attachment 1824326
Safi sana, wazee wa suti nyeusi...Rais Samia amemteua Godwin Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Dar es salaam, kabla ya hapo Gondwe alikua Mkuu wa Wilaya ya Temeke Dar es salaam. View attachment 1824344
Inapendeza sana... Apunguze utoto sasa...Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Albert Msando kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
View attachment 1824346
Inapendeza, upinzani nao upenye serikalini...Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Joshua Nassari kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda.View attachment 1824348
Inapendeza sana... Kutoka viti maalum...Rais Samia Suluhu amemteua Halima Abdallah Bulembo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Tanga.View attachment 1824349
Wasimuangiushe Mama Samia... Wawe wazalendo...Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Basilla Mwanukuzi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Basilla aliwahi kuwa Miss Tanzania 1998.View attachment 1824355
Inapendeza sana, wazee wa suti nyeusi...Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mtangazaji Mwandamizi wa ITV/Radio One Abdallah Mwaipaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.View attachment 1824359
Ndoto yake imetimia... Asiishie hapa sasa aende mbele zaidi... Hongera zake...Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mtangazaji Mwandamizi wa ITV/Radio One Abdallah Mwaipaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.View attachment 1824360
Kimya kingi kina mshindo mkuu... Hongera zake sana...Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mwigizaji Juma Chikoka maarufu Chopa Mchopanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara.View attachment 1824362