Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210620_072031.jpg
20210620_072046.jpg
 
Wizara ya Afya Tanzania imesema imeanza kuona viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la mlipuko wa Covid 19 Tanzania, hii ni kutokana na taarifa za ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huu na mwingiliano wa Watu wa Tanzania na Watu wa Nchi jirani na Mataifa mengine Duniani katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

"Tunakuwakumbusha Watanzania wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Covid 19, na tahadhari hii ya leo ni kutokana na hali ya mwenendo wa ugonjwa wa Covid 19 Duniani na ongezeko la maambukizi Afrika zikiwemo Nchi jirani ambazo zimekumbwa na wimbi la tatu la mlipuko wa Covid 19 na maambuki yameongezaka maradufu kuliko ilivyokuwa katika wimbi la pili”

"Kwa mujibu wa taarifa kutoka WHO iliyotolewa katika jarida la wiki ya 24 inayoanzia June 07 hadi June 13, 2021 katika Kanda ya Afrika idadi ya wagonjwa imekuwa ikiongezeka kwa wiki tano mfululizo “

"Mfano katia Wiki moja iliyopita Afrika Kysini, Uganda, Zambia, DRC, Namibia, Angola n.k zimeendelea kuonesha kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa isiyoshuka huku ikiripotiwa Nchi hzio kukumbwa na anuai ya virusi vipya vinavyosababisha Covid 19 kuwa kali zaidi na kuathiri hata mkundi ya wenye umri mdogo” ———-Mkurugenzi wa Idara ya Kinga - Wizara ya Afya, Dkt. Leonard Subi
20210620_104111.jpg
 
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwakuwa Watu wameshindwa kutekeleza maagizo ya kutotembea mitaani kuanzia saa tatu usiku hadi saa 11:30 Alfajiri, anakaza zaidi masharti ya Corona na kuanzia sasa ni marufuku Mtu kutembea usiku kuanzia saa moja usiku hadi 11:30 Alfajiri.

“Shule na Taasisi za Elimu ya Juu zitaendelea kufungwa kwa siku 42, Uwanja wa Ndege wa Entebbe utaendelea kufanya kazi lakini tutahakikisha hakuna kirusi kipya kinaingia Uganda”———Museveni

“Viwanda havitofungwa lakini penye uwezekano sio mbaya kwa Wafanyakazi wakaruhusiwa kuishi kiwandani kwa siku 42 kuzuia kutoka na kuingia, lengo ni kupunguza maambukizi ili tuweze kuwatibu wachache usipofanya hivyo tutaanza kuingia kwenye ligi ya kuchuana na USA, Italy na India na wengine kwa maambukizi makubwa ya Corona”———Museveni

“Ili maisha yetu yaweze kuendeea sekta zifuatazo hazitofungwa, kilimo, viwanda vya uzalishaji, Utaliii, usafirishaji wa mizigo, ulinzi, maduka ya rejareja, huduma za afya na idara za matibabu”———Museveni
20210620_104302.jpg
 
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza masharti mapya ya kupambana na Corona ambapo nyumba za Ibada, mikusanyiko ya maziko na matukio ya kimichezo vyote vimepigwa marufuku kwa muda wa siku 42.

“Sio lazima uende Kanisani kusali, unaweza kusali ukiwa nyumbani, siku zote namuona Mke wangu (Mama Janeth) akiwa anatazama TV (vipindi vya Dini) huku akisali, kuna Wanigeria Mama anapenda kuwatazama, sasa kwanini uhatarishe maisha ya Watu wako wa karibu kisa mikusanyiko ya Ibada”———Museveni

“Maziko yafanywe na Ndugu wachache wa karibu kama tuko Jeshini, mfano Mjomba yangu amefariki siku za hivi karibuni na amezikwa Rwakitura ila sikweda kuzika kwakuwa hata ningeenda nisingeongeza kitu wala sio kwamba ningeenda kumfufua”———Museveni
20210620_104422.jpg
 
Polisi nchini Uganda wamelazimika kuwatawanya Wajasiriamali Jijini Kampala ambao wametakiwa kurudi majumbani mwao ili kutii agizo la Rais Museveni la Wajasiriamali kutoruhusiwa kusambaa mitaani na kufanya biashara katikati ya Jiji kwa lengo la kujikinga na Corona.

Rais Museveni ameagiza maduka na masoko yote yaliyo katikati ya Majiji na Miji yafungwe na Wajasiriamali waache kutembeza bidhaa mitaani, maduka ya chakula pekee ndio yameruhusiwa kufunguliwa lakini kwa sharti la Wafanyabaiashara kupiga kambi kwenye maeneo yao ya biashara.

“Wajasiriamali wa chakula wapige kambi kwenye maeneo ya kazi (badala ya kwenda nyumbani na kurudi), Waziri wa Afya anaweza kuwapa chandarua ili wasing’atwe na mbu, sisi wapiganaji wakati wa mapambano tulikuwa tunalala msituni”———-Museveni
20210620_104538.jpg
 
Imethibitika kuwa Watu wanne wamefariki na wengine wanne kujeruhiwa vibaya baada ya ndege ndogo kuanguka katika mkoa wa Kemerovo kusini magharibi mwa Siberia nchini Urusi.

Taarifa za awali (ambazo hazijathibitishwa) zinasema Watu wasiopungua 7 wamefariki wakati ndege hiyo ya injini mbili chapa L-410 ilipoanguka karibu na eneo la opereshani za ndege la Tanay ambalo hutoa huduma za parachuti.

Msemaji wa huduma za matibabu amesema majeruhi wamesafirishwa kwa Ndege kwenda Hospitali.

Picha zilizochapishwa mitandaoni zinaonesha Ndege iliyoharibika vibaya na gari la kubeba wagonjwa karibu na eneo hilo, Msemaji wa tawi la Rosaviatsia la mamlaka ya usafiri wa anga ya Urusi, amesema operesheni ya utafutaji na uokozi inaendelea lakini alikataa kutoa maelezo zaidi.
20210620_105152.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt.Fenella Mukangara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Mukangara ni Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

Wengine ni Brig. (Mstaafu) Aloyce Mwanjile , Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania, Khalfan Ramadhan, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Capt. Mussa Mandia ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
20210620_105250.jpg
 
"Tangu nimempa Ubalozi Eric Omondi Watu wengi wanagoogle Temeke wanauliza kuna nini huko Temeke tunataka Wawekezaji tuna maeneo mazuri tuna Uwanja mkubwa lazima tuitangaze Temeke”

"Nimepata taarifa Vijana wetu hawajaelewa hili akina Nature, Temba , Chege niseme tu nina mpango mzuri kwa Vijana wa Temeke na nilishazungumza hili hata na Fella ambaye ni Diwani wa Kilungule lakini kwangu ni kama Mshauri wa Sanaa na tulishalipanga tuwalete pamoja Vijana wa Temeke na tuwatumie kwenye masuala ya Kijamii”

"Mimi nataka Watu waendelee kuja akina Jay Z akina Drake wote waje na wakija unadhani watakutana na nani? Mimi Meya sijui chochote kuhusu Muziki Wenyeji ndio haohao akina Chege, Nature, Temba, sisi kama Viongozi tunajenga urafiki hawa wa nyumbani bila hata kuwapa Ubalozi tayari ni Mabalozi tosha”———Abdallah Mtinika
20210620_105347.jpg
 
Rais Samia amemteua Godwin Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Dar es salaam, kabla ya hapo Gondwe alikua Mkuu wa Wilaya ya Temeke Dar es salaam.
20210620_105622.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Albert Msando kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.


20210620_105743.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Jokate Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Dar es salaam, kabla ya hapo Jokate alikua Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Pwani.
20210620_105934.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Joshua Nassari kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda.
20210620_110041.jpg
 
Rais Samia Suluhu amemteua Halima Abdallah Bulembo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Tanga.
20210620_110143.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Vicent Mashinji kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara.
20210620_110245.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom