Makapuku Forum

Makapuku Forum

Club ya soka ya Simba imetambulisha Basi lao jipya aina ya TATA ambalo litakua likitumiwa na Wachezaji wake, usajili wa namba za Basi hilo ni T 372 DVK.
20210618_042041.jpg
20210618_042328.jpg
 
"Napata maoni kuhusu Ubalozi ambao nimempa Eric Omondi, unajua kuna Watu hawajaelewa maana ya Ubalozi kwanza baadhi ya Watu hawajui kwamba Afrika Mashariki ni moja wote sisi ni Ndugu"

"Mtu akishangaa Eric kuwa Balozi sijui kwanini, kila Meya ana style yake ya kuwakarimu na kuwapokea Wageni, Mimi Mgeni yeyote akinitembelea namkarimu kwa namna ninayoona inafaa, Mbwana Samatta alinitemblea nikampa ubalozi wa Temeke na alikuwa wa kwanza kabla ya Eric”

"Kuna Ubalozi wa Hiari na Balozi wa Malipo, hawa ni Mabalozi wa hiari, yoyote akinitembelea naweza kumwambia kuwa Balozi na akaitangaza Temeke, wengine wakisikia Balozi wanajua huyu amesaini hela ndefu kumbe hamna ni hiari na kulibeba jambo na kulitangaza na ni jambao ambalo naweza kumwambia Mtu yoyote akinitembelea”———-Abdallah Mtinika Meya wa Temeke
20210618_042512.jpg
 
Msanii wa vichekesho Jumanne Alela maarufu kama Mzee Matata aliyefariki jana amezikwa leo kwenye makaburi ya Buguruni Malapa jijini Dar es salaam.

Matata alikua akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na alipelekwa kwenye Hospitali mbalimbali za Dar es salaam kabla ya kupewa rufaa na kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili alikofia jana. RIPMzeeMatata
20210618_042641.jpg
20210618_042657.jpg
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imewakumbusha Watanzania uwepo wa namba maalum ya kubonyeza kwenye simu zao ambayo itawawezesha kufahamu kama vitambulisho vyao vya Taifa vimetumika kusajili laini ya simu ambayo hawaifahamu.

Hivi karibuni kumukuwepo na baadhi ya Mawakala wasio waaminifu ambao usipokua makini kwenye kusajili laini wanaweza kutumia kitambulisho chako na kusajili laini nyingine kwa kutumia jina lako bila wewe kufahamu na line hizo ndio zinatumika kutapeli na kufanya uhalifu.

Njia ya kwanza ya kujiweka salama ni kuhakiki kujua status ya kitambulisho chako cha Taifa kwa kubonyeza *106# na kisha utakutana na option mbalimbali, ni rahisi na ni zoezi la sekunde chache litakalokusaidia kukaa kwenye mstari unaotakiwa.
20210618_131835.jpg
 
Aliyekua DC wa Hai Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake leo wamefikishwa tena kwenye Mahakama ya Wilaya iliyopo Sekei Arusha,ili kujibu tuhuma zinazowakabili, Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matano.

Itakumbukwa June 04,2021 Sabaya na wenzake walifikishwa Mahakamani hapo ambapo baadaye Tumaini Kweka, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka anayeshughulika na usimamizi wa kesi alisema———-“uchunguzi katika baadhi ya makosa yanayomkabili Lengai na wenzake umefikia kwenye kiwango ambacho tunasema ni tamati ya kuweza kuwafikisha Mahakamani”

“Mkurugenzi wa Mashtaka baada ya kujiridhisha kwamba kweli tuhuma zilizokua zinamkabiki Lengai na wenzake kisheria zinatengeneza kosa akaamua leo wafikishwe Mahakamani, kama mlivyoona alikua akituhumiwa kuongoza magenge ya kihalifu, vitendo vya rushwa, kutakatisha fedha haramu ambayo ni matokeo ya vitendo vya rushwa”

“Vilevile Mkurugenzi alijiridhisha kwamba kuna unyang'anyi wa kutumia silaha, ndio maana amefikishwa Mahakamani leo kwa hayo makosa matano lakini kwa unyang'anyi wa kutumia silaha ni makosa mawili aliyatenda katika wakati mmoja lakini kwa wakati tofautitofauti, na kama tuhuma nyingine zitathibitika basi Mkurugenzi wa Mashtaka ataamua vinginevyo" ——— Tumaini Kweka.
20210618_132301.jpg
20210618_132325.jpg
20210618_132346.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza siku saba za maombolezo ya Kitaifa kufuatia kifo cha Rais wa kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda kilichotokea jana June 17, 2021 Jijini Lusaka, Zambia, katika kipindi hicho cha maombolezo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Rais Samia ametuma pia salamu za rambirambi kwa Rais wa Zambia, Edgar Lungu , Familia ya Marehemu na Wananchi wote wa Zambia kwa kumpoteza Kiongozi wao.

RIPMzeeKaunda
20210618_132640.jpg
 
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya (34) na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza kesi inayowakabili huku wakiwa katika ulinzi mkali.

Sabaya alifika mahakamani hapo leo asubuhi Juni 18, 2021 akiwa katika basi la Magereza huku watu waliofurika mahakamani hapo wakimzomea.

Mkuu huyo wa wilaya wa zamani alishuka kwenye gari akiwa amevaa suti ya bluu mkononi akiwa ameshika vitabu huku uso wake ukipambwa na tabasamu licha ya zomeazomea kutoka kwa watu waliokuwepo mahakamani hapo.
20210618_132824.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia kesi ya uhujumu uchumi na kuwaachia huru wafanyakazi sita wa kampuni ya meli ya Sinota Shipping Company waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na ndege mmoja aina ya tausi.

Washtakiwa hao ambao wote ni raia wa China ni Jin Erhao (35), Chengfa Yang (49), Ren Yuangqing (55), Shu Nan (50), Chen Shinguang (45) na Gu Jugen (57) wote wakazi wa mtaa wa Sokoine, Ilala jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa baada ya kuachiwa walitoka mahakamani huku wakikimbia na kupanda gari kisha kuondoka.
20210618_133134.jpg
 
Kutokea Kanisa la KKKT Kunduchi inafanyika Ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwanachama wa CHADEMA na Mjumbe wa Kamati Kuu Mstaafu wa Chama hicho , Profesa Mwesiga Baregu aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili Juni 13, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Viongozi na Watu wengine mbalimbali wamejitokeza akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka.
RIPMzeeBaregu
20210618_141236.jpg
20210618_141302.jpg
 
Shirika la Afya Duniani (WHO) imesema Bara la Afrika lipo katika wimbi la tatu la maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona na kwamba kuna haja ya kupatikana kwa chanjo zaidi.

Hayo yameelezwa jana Alhamisi Juni 17, 2021 kupitia tovuti pamoja na mitandao ya kijamii ya shirika hilo.

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona Afrika ni zaidi ya milioni tano huku nchi saba zikiishiwa na chanjo.
Kwa mujibu wa WHO jumla ya watu 136,030 wamefariki kutokana na ugonjwa wa Covid -19 katika nchi tofauti za Afrika.

Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti amesema Afrika ina uhitaji wa mamilioni ya chanjo hadi sasa kutokana na ugonjwa huo kushika kasi.

Uganda na Namibia zinakabiliwa na wimbi la tatu la maaambukizi huku watu wakiripotiwa kufa kila siku.

Afrika Kusini, Morocco, Tunisia, Ethiopia na Misri zimeripoti ongezeko kubwa la maambukizi ya corona barani humo.
WHO inasema hakuna muda kamili kubaini ni lini chanjo zaidi zitapatikana lakini limesisitiza kwamba kuna haja kushughulikia upatikanaji wake kwa haraka.

20210618_141557.jpg
 
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wamesomewa mashtaka mawili yanayowakabili kati ya mashtaka sita waliyonayo pamoja na wenzao watatu.

Imeelezwa leo Ijumaa Juni 18, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa mashtaka mengine manne upelelezi wake bado haujakamilika.

Wakili mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka amemweleza hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya, Salome Mshasha kuwa upande wa mashtaka umekamilisha upelelezi na upo tayari kuwasomea maelezo watuhumiwa.
20210618_141720.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom