Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210616_054534.jpg
20210616_054600.jpg
 
Benki kuu ya Tanzania (BOT) imeipa idhini Kampuni ya Teknolojia ya huduma za kifedha ya NALA MONEY kuweza kutoa huduma zake hapa Tanzania kwa ushirikiano na Equity Bank Tanzania.

Tanzania ilikuwa ni Nchi ya kwanza NALA kuomba idhini lakini ilipata kibali na kuanza kutoa huduma zake kwenye nchi za Kenya, Uganda na Uingereza kabla ya Tanzania, habari njema ni kwamba tayari BOT imeiruhusu NALA kutoa huduma zake kwa watumao fedha kutoka Uingereza kuja Tanzania kwa kupitia ushirikiano na Benki ya Equity.

"Naishukuru Benki Kuu ya Tanzania kwa kutuamini na ninafurahi sana kuona teknolojia ya nyumbani inavuka mipaka na kufikia watu wengine duniani, naamini Mungu ametupa uwezo wa kufanikisha hilo” ——— Benjamin Fernandes Mwanzilishi wa NALA.View attachment 1819476
Huyo Benjamin Fernandes ni hb haswaah, hivi anaishi wapi?
 
Mchekeshaji kutoka kundi la Mizengwe Jumanne Alela (Mzee Matata) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taaarifa hizo zimethibitishwa na Mchekeshaji mwenzie wa Mizengwe Mkwere ambaye awali aliweka video akiwa analia kwenye ukurasa wake wa Instagram ambayo ilifuatiwa na post ya taarifa za kifo cha Mzee Matata.

June 13,2021 Katibu wa Chama Cha Waigizaji (TDFAA)- Wilaya ya Kinondoni alitoa taarifa ya kuugua kwa Mzee Matata ambayo ilielezea kuwa hali yake ni mbaya na amelazwa Muhimbili.

Taarifa ya Katibu ilisema———-“Mzee Matata hali yake mbaya alipelekwa Temeke Hospital kwa ajili ya matibabu kutokana na hali yake kahamishiwa Muhimbili ambapo alikuwa kalazwa mwanzo na kuruhusiwa juzi ila leo hali imebadilika ghafla kwa taarifa nilizopewa kakata kauli na ana kwikwi ya mfululizo DUA & SALA vinahitajika”
20210616_141343.jpg
 
Mchambuzi wa soka ambae juzi alitangaza kugombea Urais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Oscar Oscar amesema jina lake limekatwa kwenye orodha za wanaowania Urais huo TFF, tulipomuuliza ni kwa sababu gani amesema amepewa sababu tatu za kwanini jina lake limekatwa lakini hajataka kuziweka wazi kwa sasa, tunaendelea kufatilia zaidi.
20210616_141621.jpg
 
Ubalozi wa Tanzania nchini China umetangaza kuwa Makampuni 16 ya Tanzania yamepata kibali cha Serikali ya China kuuza Maharage ya soya katika Soko la China.

Hatua hii inafanya idadi ya Makampuni ya Tanzania yenye idhini ya kuuza maharage ya soya nchini China kufikia 65 baada ya Makampuni 49 kupata kibali hapo awali.

“Hii ni habari njema kwamba wigo wa mahusiano ya kibiashara kati ya China na Tanzania unazidi kupanuka, kwa sasa fursa hii imekuja na changamoto tunachozalisha nchini ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji ya soko, hivyo hii ni fursa kwa Watanzania kulima maharage ya soya kwa wingi” ———Mberwa Kairuki, Balozi wa Tanzania nchini China
20210616_141742.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom