Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mchezaji wa Inter Milan na Timu ya Taifa ya Denmark, Christian Eriksen Jumamosi iliyopita alianguka uwanjani na kupoteza fahamu kutokana na tatizo la moyo (cardiac arrest) dakika ya 42 ya mechi ya Euro 2020 Denmark vs Finland.

Taarifa mpya kuhusu Eriksen leo ni kwamba bado yupo hospitali akipatiwa matibabu lakini anaendelea vizuri na ametumia ukurasa wake wa instagram kuwashukuru wote waliomuombea wakati alipopata matatizo.

"Asante sana kwa salamu zenu nzuri na ujumbe kutoka ulimwenguni kote, ina maana kubwa sana kwangu na familia yangu niko sawa na bado ninahitajika kupitia vipimo hospitalini lakini ninajihisi sawa na sasa nitawashangilia vijana kwenye Timu ya Denmark katika mechi zijazo” ——— Christian Eriksen.

Ericksen ni miongoni mwa Wachezaji wa soka waliowahi kuitembelea Tanzania kwenye upande wa Mbuga za Wanyama ambapo alikuja Ngorongoro na Mpenzi wake mwaka 2017.
20210615_143827.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo akiongea na Vijana kwenye uwanja wa Nyamagana Mwanza amesema malipo wanayostahili kulipwa Wasanii wa muziki kutokana na kazi zao kuchezwa kwenye Radio na TV mbalimbali za Tanzania pale kazi zao zinapotumika yataanza kutolewa December 2021 kwa Wasanii hao.

“Ili kuikuza sekta ya Sanaa Serikali tumeimarisha haki miliki za Wasanii, nataka kuwataarifu Vijana kuwa kuanzia December mwaka huu Wasanii wataanza kulipwa mirabaha yao kutokana na kazi zinazotumiwa kwenye radio, runinga au mitandaoni” ———Rais Samia.
20210615_143955.jpg
 
"Kuna mkeka wa Ma-DC utakaotoka karibuni na wote ni Vijana ingawa baadhi yenu tunapowapa fursa mnafanya mnayoyafanya, mnatuangusha... mnaopata fursa mkalitumikie Taifa kwa umakini/ufanisi sababu Vijana sasa ndio wanaendesha Taifa”

“Mbali na mkeka wa Wakuu wa Wilaya bado nina mkeka wa Wakurugenzi na Makatibu Tawala wa Wilaya haujatoka kwahiyo ni fursa zenu Vijana”——— Rais Samia, Mwanza leo.
20210615_144115.jpg
 
“Juzi niliona pale Morogoro Vijana na Wajasiriamali wadogo wametengewa maeneo mbali na Watu na kwakuwa walikotengewa hawauzi wamerudi maeneo ambayo wameondoshwa na niliona Mgambo wakienda kuwavamia, kuwapiga na kuharibu vitu vyao”

“Nimesikitika sana na niseme hapa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa eneo hilo hawana kazi, kwasababu kuna njia nzuri zaidi wangeitumia kusema na wale na wakaondoka sio picha ile niliyoiona kwenye TV, nakuagiza Waziri wa TAMISEMI kalisimamie hili”———Rais Samia Suluhu akiongea na Vijana Mwanza leo
20210615_144411.jpg
 
“Namuagiza Waziri wa Michezo kuanza kujenga Academy za Michezo kwenye Mikoa, nimekusikia Waziri Bashungwa ukisema kuhusu kujenga Sports and Arts Arena ile itajengwa eneo moja lakini Academy zitajengwa kwenye Mikoa mingi”———-Rais Samia akiongea na Vijana Mwanza leo
20210615_145759.jpg
 
“Kwenye Mtandao kuna fursa pana za Vijana kujiajiri na wengi wenu nashukuru mna Viji-TV vyenu huko mnaviendesha lakini Vijana mitandao hiyohiyo mnaitumia kwa njia isiyo, Vijana badala ya kujipanga mnatumia muda mwingi kulaumu na kushutumu, naomba sana kama una jambo la kulaumu”

“Laumu alafu toa pendekezo tufanye vipi, kama una shutumu... shutumu kuwa na ushahidi unashutumu nini na utoe ushahidi tulichukulie hatua lakini mkiishia tu kuingia mitandaoni kusemana na kusemana hiyo haitosaidia” ——— Rais Samia akiwa Nyamagana Mwanza leo.
20210615_145911.jpg
 
“Tumeanzisha mfuko wa maendeleo ya michezo ili kuziandaa na kuzisaidia Timu zetu za Taifa na kwenye mwaka ujao wa fedha tumefuta VAT ya nyasi bandia ili kuboresha viwanja vyetu na hapa nizungumze na CCM, viwanja vingi vinamilikiwa na CCM lakini hali zake haziridhishi sasa fursa imetoka niombe viwanja vitengenezwe viwekwe nyasi bandia ili Vijana wetu wavitumie, Naibu Katibu Mkuu andaa mpango wa kuboresha na kama hamna uwezo tafuteni Wawekezaji”———Rais Samia akiongea na Vijana Mwanza Leo
20210615_152215.jpg
 
Benki kuu ya Tanzania (BOT) imeipa idhini Kampuni ya Teknolojia ya huduma za kifedha ya NALA MONEY kuweza kutoa huduma zake hapa Tanzania kwa ushirikiano na Equity Bank Tanzania.

Tanzania ilikuwa ni Nchi ya kwanza NALA kuomba idhini lakini ilipata kibali na kuanza kutoa huduma zake kwenye nchi za Kenya, Uganda na Uingereza kabla ya Tanzania, habari njema ni kwamba tayari BOT imeiruhusu NALA kutoa huduma zake kwa watumao fedha kutoka Uingereza kuja Tanzania kwa kupitia ushirikiano na Benki ya Equity.

"Naishukuru Benki Kuu ya Tanzania kwa kutuamini na ninafurahi sana kuona teknolojia ya nyumbani inavuka mipaka na kufikia watu wengine duniani, naamini Mungu ametupa uwezo wa kufanikisha hilo” ——— Benjamin Fernandes Mwanzilishi wa NALA.
20210615_160036.jpg
 
'Epuka sana kumchukia mtu anayezungumza kitu kibaya juu yako, huwezi kujua, kaamka leo kavurugwa hasira zake kakumalizia wewe, kesho mwenyewe akikaa atajuta na kukuomba msamaha'


Msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz amewajibu wanaotaka aondolewe kwenye tuzo za BET, akisema ni mawazo yao na anayaheshimu.


'Mimi naheshimu mawazo ya kila mtu, mtu akinifurahia, akinitukana akinisema mimi nashukuru',
alisema Diamond kupitia kituo cha TV cha Wasafi.


Wanaompinga msanii huyo kupitia mitandao ya kijamii wanadaiwa kufanya hivyo ili kuonesha hisia zao kutokana na msanii huyo 'kushiriki siasa akikiunga mkono chama tawala cha CCM' nchini humo, kilichoshinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 unaolalamikiwa kuwa ulikuwa na udanganyifu.

Hata hivyo tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania imepinga madai haya na kusema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.


Lakini pia wanadai kwamba msanii huyo yuko karibu na wanasiasa, wanaodaiwa kukiuka haki za binadamu.
20210615_193853.jpg
 
Saudi Arabia imepiga maarufuku raia kutoka mataifa mengine kufanya ibada ya Hija nchini humo mwaka huu 2021 ili kudhibiti virusi vya corona.


Ni mahujaji elfu sitini pekee wanaoishi kwa sasa katika ufalme huo watakaoweza kushiriki Hija, kulingana na tangazo lililotolewa kwenye vyombo vya habari vya taifa hilo.


Watu takriban milioni mbili vinginevyo wangetembelea Maka na Madina msimu wa kiangazi kwa ajili ya Hija hiyo inayofanyika kila mwaka kulingana na imani ya kiislamu.


Huu utakuwa ni mwaka wa pili kwa Waislamu kukosa kutekeleza moja ya nguzo kuu za dini ya hijja.

20210615_194352.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom