Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga leo anasherehekea kufikisha umri wa miaka 55 na ameamua kutangaza mchongo mkubwa wa Taifa leo kwenye siku yake kubwa ambao una thamani ya milioni 550 Tsh.

Namshukuru sana Mungu kwa kunipa nafasi ya kuwaongoza CMG, katika kuangalia na kuona kuna biashara nyingi na Vijana wengi ambao wana biashara lakini bahati mbaya hakuna kitu chenye gharama kama kutangaza biashara”———CEO wa CMG

“Katika kufikiri nikasema hii miaka yangu 55 kwanini nisichague tena Vijana 55 ambao watakuwa na matangazo yenye thamani ya Tsh. Milioni 10 kwa kila kijana yawe ya mwezi mzima na hayo matangazo yatakuwa na thamani ya Tsh. Milioni 550”———KUSAGA

“Big Joe Incubator nia yangu ni kuhakikisha kwamba tunafanya kitu ambacho kitafungua milango kwa Watu wengi, itanyanyua middle class na hawa Vijana 150 watainua Watu wengine na tutawabeba kwa ukubwa”———-KUSAGA

“Big Joe Incubator ni project nashirikiana na wadau wengi tofauti ambao wamekubali mawazo yangu ya mimi kufungua milango kwa zaidi ya Vijana 150, hasa wanaojihusisha na techonology lakini wanakosa support ya mafunzo na funds”———KUSAGA
20210609_154702.jpg
 
Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametangaza Baraza la Mawaziri na kuwaweka Wanawake kwenye nafasi nyeti kama Makamu wa Rais na Waziri Mkuu huku Mkewe Janeth akibaki kuwa Waziri wa Elimu, hii ni tofauti na Mabaraza yake ya awali toka aanze kuiongoza Uganda kama Rais mwaka 1986 kwani amewapa nafasi zaidi Wanawake kuliko Wanaume.
20210609_154859.jpg
 
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameipongeza Serikali ya Nigeria kwa kuamua kuifungia Twitter nchini Nigeria———“Hongera sana Nigeria kwa kuifungia Twitter, Nchi nyingine ziige pia zifungie Twitter na Facebook maana zinaminya uhuru wa kujieleza”

Itakumbukwa Trump alifungiwa kutumia mitandao Twitter na Facebook January 2021 huu akidaiwa kuchochea vurugu kwenye majengo ya Bunge Marekani zilizosabisha vifo vya Watu zaidi ya wanne.

"Wao ni nani hata wawe wanaamua kipi kizuri na kipi kibaya wakati wao wenyewe ni wabaya? najilaumu kwa kutowafungia nilipokuwa Rais lakini Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg aliendelea kunipigia simu na kuja Ikulu ya White House kwa chakula cha jioni akiniambia jinsi nilivyokua mzuri”

Wiki iliyopita Nigeria ilifungia Twitter nchini humo kwa madai kwamba shughuli za mtandao huo zinahujumu na kuingilia uhuru wa Nigeria kama Nchi huru, hatua hiyo ilichukuliwa siku kadhaa baada ya post ya Rais Muhammadu Buhari kuondolewa kwa kukiuka kanuni za mtandao wa huo wa kijamii.
20210609_155209.jpg
 
Baadhi ya Waislamu Nchini Burundi wameendelea kupaza sauti za kutaka kuachiwa huru kwa Sheikh Rashidi Ndikumana aliyekamatwa na Polisi baada ya kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi kuwaomba radhi Waislamu kufuatia tamko lake hivi karibuni.

Hii ni baada ya Waziri huyo aitwae Gervais Ndirakobuca kuongea kwenye mkutano na Viongozi wa dini mbalimbali Burundi na kusema Wananchi wanakerwa na kelele za Makanisa na Adhana za Misikiti na kusema adhana alfajiri ni kero kwa Raia kwani ni jukumu lao Waumini kujua wakati wa kusali bila kukumbushwa na adhana.

Baada ya matamshi hayo kulizuka vuta nikuvute kati ya Polisi na baadhi ya Waumini katika mtaa wa Buterere kusini mwa Bujumbura ambako Sheikh huyo anaishi na kuongoza Masjid Madina ambapo Sheikh huyo alimtaka Waziri huyo kutambua kwamba adhana katika Uislamu ilikuwepo kabla ya kuzaliwa kwake na itaendelea kuwepo na akamuagiza kuwataka radhi Waislam katika kipindi kisichozidi wiki moja lasivyo watamuomba Rais Evariste Ndayishimiye kumfuta kazi.
20210609_215513.jpg
 
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea nchini Tanzani Kim Yong Sung leo June 9 2021 katika Ofisi za CCM Makao Makuu Dodoma.


20210609_215654.jpg
 
Rais Samia Suluhu amemteua Jaffar Haniu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais IKULU akichukua nafasi ya Gerson Msigwa ambaye aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na pia wakati huohuo Msemaji Mkuu wa Serikali, kabla ya uteuzi huu Haniu alikuwa Mtendaji Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Africa Media Group Limited.
20210609_215825.jpg
 
Baada ya Rais wa Ufaransa kupigwa kofi jana, Ofisi ya Rais imesema inafahamu kulikuwepo na jaribio la kumshambulia lakini haijaeleza zaidi, Rais Macron alipigwa kofi jana alipozuru Drome kukutana na Wamiliki wa Migahawa na Wanafunzi kuzungumza maisha baada ya janga la Covid-19.

Tayari Watu wawili wanashikiliwa kutokana na tukio la jana ambapo mmoja wao ni Mwanaume aliyempiga kibao Rais, hata hivyo France 24 jana ilimnukuu Mhariri na Mchambuzi wa siasa za Ufaransa Marc Perelman akisema tukio la Rais kushuka kwenye gari yake na kusalimia Watu hakikuwepo kwenye ratiba ya Rais kwa siku ya jana, aliamua tu ghafla kusimamisha msafara na kusalimia Watu waliokua wakimpungia.
20210609_215942.jpg
 
Rais Samia Suluhu amemteua Jaffar Haniu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais IKULU akichukua nafasi ya Gerson Msigwa ambaye aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na pia wakati huohuo Msemaji Mkuu wa Serikali, kabla ya uteuzi huu Haniu alikuwa Mtendaji Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Africa Media Group Limited. View attachment 1813567
Tulitarajia hili kutokea muda sii mrefu...
 
#bajeti kuu "Wizara ya Fedha na Mipango imeanza mchakato wa kuomba mkopo wa dharura wa dola za kimarekani milioni 571 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) ili kukabiliana na athari za ugonjwa wa COVID-19 kwa matumizi yatakayoainishwa" Dkt.
@mwigulunchemba1
, Waziri wa Fedha na Mipango
 
Kuhusu tathimini ya utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2020-21, katika kipindi cha mwaka 2020-21, Serikali ilipanga kukusanya jumla ya shilingi Trilioni 34.88 kutoka katika vyanzo vya ndani na nje. Hadi Aprili 2021, shilingi Trilioni 24. 53 zimekusanywa sawa na asilimia 86.1 ya lengo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom