Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa shule moja kila Mkoa kuanzia Julai kwa ajili ya kufundishia masomo ya sayansi kwa wasichana.
“Wanawake sio viumbe dhaifu ni Watu imara na wenye nguvu kama binadamu wengine na pengine Wanawake wana nguvu zaidi, tuna nguvu za kisaikolojia tunabeba mengi, na tuna nguvu kwenye mioyo yetu tunastahimili mengi kwenye vifua vyetu”———Rais Samia mbele ya Wanawake, Dodoma leo
“Wanawake tuna nguvu kwenye matumbo yetu tunabeba na kuwaleta viumbe Duniani hiyo ni nguvu ambayo Mungu alitupendelea Wanaume hawakupewa hiyo nguvu”———Rais Samia
“Kwenye nguvu za kubeba magunia na mizigo mingine Mungu hakutupa hiyo nguvu, nguvu za kuhamasisha ugomvi na kupigana sisi hajatupewa, sisi yetu midomo tuna midomo kweli ila ukiambiwa sogea hapa mbioo, ila tuna nguvu kwenye mioyo na matumbo yetu”———Rais Samia
“Hili la Watu kudaiwa wakati Mtu amefariki wekeni mpango vizuri, hata Kidini tunaambiwa Mtu akidaiwa hazikwi mpaka deni lilipwe ila sio kwa deni la Serikali, sisemi deni lisilipwe ila uwekwe mpango mzuri wa deni kulipwa bila kuzuia maiti kuzikwa”———Rais Samia akizungumza na Wanawake Dodoma leo
“Moja ya mpango mizuri ni kutoa gharama za matibabu kabla ya mgonjwa kufariki sio hadi Mgonjwa amefariki ndio unamwambia bila kulipa deni lako Milioni 3 au ngapi mwili hauzikwi hii hapana tukaweke mpango vizuri sio kuzuia maiti”———Rais Samia
Serikali imeeleza kuwa inakusudia kuanzisha vituo vya kulea vipaji katika shule mbalimbali na katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, ili kuhakikisha vipaji vya Watoto havipotei.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ametoa kauli hiyo leo katika uzinduzi wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (UMISSETA) inayofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara huku Mgeni rasmi akiwa ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Bashungwa amesema mashindano hayo ni msingi wa kuvumbua vipaji maana ili kufanya vizuri katika michezo ni lazima uimara uanzie chini, mashindano yanaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya TAMISEMI.
Bashungwa amesema ili kukuza vipaji zaidi katika uzinduzi huu wamealikwa wavumbua vipaji kutoka vilabu mbalimbali nchini, Taasisi ya Mbwana Samatta na mawakala kutoka nchini Sweden.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameahidi kukutana na kuzungumza na vijana atakapokuwa katika ziara yake mkoani Mwanza.
Kiongozi mkuu huyo wa nchi ameeleza hayo leo Jumanne Juni 8, 2021 katika kongamano la wanawake mkoani Dodoma akibainisha kuwa kufanya hivyo ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na makundi mbalimbali nchini kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kusikia mambo yanayowahusu.
"Kama ambavyo mnafahamu tayari nilishakutana na viongozi wa dini mkoani hapa, na nilikutana wazee pale Dar es Salaam kwa niaba ya wazee wote wa Tanzania na pia viongozi wa taasisi binafsi kwa niaba ya sekta binafsi na nitazungumza na vijana pale Mwanza Kwa niaba ya vijana wote wa Tanzania, leo ni zamu ya wanawake,” amesema Samia.
“Nimeongeza Wanawake kwenye teuzi, upande wa Makatibu Tawala hapa nimefanya vizuri zaidi na sijui kama kuna eneo nitafanya vizuri zaidi ya hapo, kati ya Makatibu Tawala 26 Wanawake ni 12 hii ni sawa na 46%, labda uteuzi wa pili utakuwa 50 kwa 50”———Rais Samia akizungumza na Wanawake Dodoma leo
“Mahakamani tuliteua Majaji 28 na kati yao Majaji 12 au 13 ni Wanawake sawa na asilimia 43%, hii inamaanisha 50 kwa 50 haiko mbali, kwa sasa Mahakama Kuu Majaji Wanawake ni 40 kati ya 86”———Rais Samia
“Bungeni tuna Naibu Spika Mwanamke Dr. Tulia, Wabunge Wanawake idadi imeongezeka, nimemteua Katibu wa Bunge Mwanamke kwa mara ya kwanza katika historia ya Nchi yetu, kwenye miaka michache ijayo tunaweza kufika au kukaribia sana usawa wa kijinsia”———Rais Samia
“Kwenye mambo ya kidigitali Wanawake bado, Wanaume leo wengi wamejiajiri kupitia mifumo ya kidigitali ila Wanawake ni kuuza nyanya na michicha kwenye digitali wapo wachache sana, lazima tuzibe pengo hili, Dunia sasa inaendeshwa kidigitali”———Rais Samia akizungumza na Wanawake Dodoma leo
“Kuna pengo la kidigitali kwa Wanawake, hata Mimi nikikwama kitu kidogo kwenye simu yangu nina kajukuu kangu kanaitwa Ibra ana miaka 9 anaichukua anaitazama dakika chache anasema Bibi tayari lakini nina Kajukuu kanaitwa Samia ukimpa angalia anasema sijui mpe Ibra”———Rais Samia
“Hata kwa Familia zetu Watoto wa kiume wapo faster kidigitali kuliko Wanawake ndio maana tukaweka Shule za kufundisha Wasichana Sayansi ili tuzibe pengo hili la kidigitali kwa Wanawake”———Rais Samia
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla leo Juni 08 amefanya mazungumzo na Kamanda Mpya wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam ACP Jumanne Muliro aliefika kuripoti kwa Mkuu wa Mkoa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Simon Sirro.
Katika Mazungumzo hayo RC Makalla amemuelekeza Kamanda Muliro kuendelea na operesheni ya kuwashughulikia kikamilifu Majambazi na Wahalifu ili Dar es salaam ibaki kuwa tulivu na Wananchi wafanye shughuli zao salama ambapo kwenye mazungumzo hayo RC Makalla amesema kwa sasa hali ya usalama Dar es salaam ni shwari na hataki kusikia Majambazi yakifanya uhalifu. View attachment 1812692
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla leo Juni 08 amefanya mazungumzo na Kamanda Mpya wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam ACP Jumanne Muliro aliefika kuripoti kwa Mkuu wa Mkoa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Simon Sirro.
Katika Mazungumzo hayo RC Makalla amemuelekeza Kamanda Muliro kuendelea na operesheni ya kuwashughulikia kikamilifu Majambazi na Wahalifu ili Dar es salaam ibaki kuwa tulivu na Wananchi wafanye shughuli zao salama ambapo kwenye mazungumzo hayo RC Makalla amesema kwa sasa hali ya usalama Dar es salaam ni shwari na hataki kusikia Majambazi yakifanya uhalifu. View attachment 1812696
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.