Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jumla ya TZS bilioni 328.2 zinatarajiwa kutumika kugharamia sensa ya mwaka 2022. Kwa mara ya kwanza katika historia ya sensa nchini, zoezi hilo litatumia teknolojia ya vishikwambi (tablets) katika utengaji wa maeneo ya kijiografia na ukusanyaji wa takwimu uwandani. #Bajeti2021
 
Simu na matumizi yake
20210610_171333.jpg
 
“Serikali imepokea malalamiko kuhusu kucheleweshwa kwa michango ya watumishi kupelekwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na baadhi ya ofisi za Serikali kutopeleka kabisa, napendekeza kulipa michango hiyo moja kwa moja kutokea Hazina“——MWIGULU
 
"kupunguza kiwango cha kodi kutoka asilimia 20 hadi asilimia 15 katika michezo ya kubashiri matokeo ya michezo na hilo litasaidia kuzuia watu kucheza michezo hiyo online (mtandaoni) kwenye nchi nyingine" Dkt. @mwigulunchemba1, Waziri wa Fedha na Mipango
#BajetiyaSerikali20212022
 
"Kuanzia sasa, napendekeza kupunguza faini za makosa ya bajaji na pikipiki kutoka elfu 30 za sasa hadi shilingi elfu 10 kwa kosa moja"Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1, Waziri wa Fedha na Mipango
#BajetiyaSerikali20212022
 
“Serikali inatarajia kukopa Tsh. trilioni 2.35 kutoka soko la nje kwa lengo la kuongeza kasi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo”
 
“Serikali inatarajia kukopa Tsh. trilioni 7.34 kutoka soko la ndani na nje, kati ya kiasi hicho, Tsh. trilioni 4.99 ni mikopo ya ndani ambayo inajumuisha Tsh. trilioni 3.15 kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva”
 
Serikali inakusudia kuanzisha tozo ya ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha 10% kwenye pikipiki zilizotumika kwa zaidi ya miaka 3 zinazoingizwa nchini ili kudhibiti uingizaji wa pikipiki chakavu na kulinda mazingira. Hatua hiyo itaongeza mapato ya Serikali kwa TZS milioni 263.7
 
“Kuhusu elimu kuna kazi kubwa bado iko mbele yetu, bado kuna Shule zina Wanafunzi wengi kuliko idadi ya madarasa na zipo zinazogawa mikondo ili wengine wasome asubuhi na wengine wasome mchana, hii inapunguza muda wa Wanafunzi kusoma”———MWIGULU
#BAJETI2021
 
“Kujenga miundombinu ya Shule kwa kusubiri irushwe mitandaoni ndio tuone inatutia aibu au kusubiri Watoto wakose pa kwenda au wakose pa kukaa ndipo tukimbizane na kufukuzana ni ishara ya kutopanga vizuri, hili tusingependa liendelee kuwepo”—
 
MABORESHO SEKTA YA UTALII: Napendekeza kupunguza ada ya leseni ya biashara ya utalii (TTBL) kwa wakala za safari kutoka Dola za Marekani 2000 hadi Dola za Marekani 500 ili kuhamasisha biashara ya utalii.
 
"Kuongeza kodi kwa asilimia 30 kwa vinywaji vikali lengo ni kuweka utofauti wa vinywaji hivyo na vinywaji vingine vyenye vilevi" Dkt. @mwigulunchemba1, Waziri wa Fedha na Mipango
#BajetiyaSerikali20212022
 
“Kufuatia mazungumzo ya Rais Samia na Kristalina (Mkurugenzi Mtendaji wa IMF), Wizara ya Fedha na Mipango imeanza majadiliano na IMF ya mkopo wa dharura wa USD milioni 571 (wa masharti nafuu) kwa ajili ya kukabiliana na athari za Covid-19”———MWIGULU
#BAJETI2021
 
" Kwa jinsi ambavyo @SuluhuSamia ameanza kuongoza nchi yetu,ni dhahili kabisa amepeta somo kubwa kutoka kwa Rais Mstaafu @jmkikwete ambaye aliamini katika taasisi na hapendi kuonea watu" Mwigulu Nchemba, Waziri Wa Fedha
#BajetiYaSerikali
 
“Serikali itatekeleza miradi ya uboreshaji wa miundombinu itakayogharamiwa na mikopo yenye masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia ikiwemo Mradi wa Kuendeleza Jiji la DSM Awamu ya Pili(DMDP II) wa kukabiliana na mafuriko Bonde la Mto Msimbazi“——MWIGULU
 
#BudgetTZ: Fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida zinajumuisha shilingi trilioni 10.66 kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali, shilingi trilioni 8.15 kwa ajili ya mishahara na shilingi trilioni 4.19 kwa ajili ya matumizi mengineyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom