Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210608_101750.jpg
 
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) imetoa taarifa kwa Wananchi na Wakazi wa Bagamoyo hadi Kigamboni kuwa huduma ya majisafi itakosekana kwa saa 24 kuanzia leo June 08, 2021 asubuhi hadi kesho June 09,2021 kufuatia dharura ya kupungua kwa uzalishaji maji mtambo wa Ruvu Chini.

Sababu ni kupisha matengenezo ya bomba kuu la usambazaji maji lenye inch 54 linalotokea katika matenki ya Chuo Kikuu Ardhi eneo la Victoria na Makumbusho baada ya bomba hilo kupasuka.

Maeneo yatakayoathirika ni Mji wa Bagamoyo, vijiji vya zinga, Kerege, Mapinga, Bunju, Boko, Mivumoni, Kawe, Kinondoni, Ilala, Temeke, Uwanja wa Ndege, Tegeta, kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Kijitonyama, Oysterbay na Magomeni.

Maeneo mengine yatakayoathirika ni Upanga, Kariakoo, katikati ya jiji (City center), Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Mhimbili, Kigamboni Navy na Ferry———“DAWASA imeomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza”
20210608_104744.jpg
 
Huenda leo June 8, 2021 ikawa ni miongoni mwa siku zenye matukio ya kipekee kutokea katika Mkutano wa Bunge, Dodoma ambapo kufuatia Mkutano wa Rais Samia Suluhu Dodoma leo, Wabunge Wanawake wote wamehudhuria Mkutano huo na kupelekea Mkutano wa tatu wa Kikao cha tatu wa Bunge la 12 kufanyika ukiwa na Wabunge Wanaume pekee.
20210608_104923.jpg
20210608_104939.jpg
20210608_105000.jpg
 
Mwimbaji wa Bongofleva akitoa Burudani kwenye Mkutano wa Rais Samia Suluhu na Wanawake Dodoma leo, Rais Samia anazungumza na Wanawake wa Dodoma leo kwa uwakilishi wa Wanawake wote Tanzania.
20210608_113835.jpg
 
Kukosa uwaziri kuliniumiza ama la. Sidhani kama ni jambo ambalo ninaweza nikalielezea, ila kuna baadhi ya mambo yaliyoendana na mimi kukosa uwaziri, kwa kweli yaliniumiza,” hiyo ni kauli ya aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla.

Kigwangalla aliyeanzia nafasi ya naibu waziri wa afya na baadaye kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema hayo kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake jijini Dodoma.

Alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa iwapo ameumia kukosa kuteuliwa nafasi ya uwaziri na hasa alivyopotea kwa muda kwenye akaunti yake ya ‘twitter’ ambako baadhi ya wafuasi wake walidai kukosa uwaziri kumemfanya aumie moyoni.

“Sidhani kama ni jambo ambalo ninaweza nikalielezea, ila kuna baadhi ya mambo yaliyoendana na mimi kukosa uwaziri, kwa kweli yaliniumiza.

“Kwa mfano, unajua kwa bahati mbaya sisi viongozi tukiwa kwenye Serikali kule jambo likishasemwa na mkubwa hata kama haliko sahihi huwezi kulifafanua kwa kuwa limetoka kwenye kinywa cha bosi, mtu mkubwa, huwezi kufafanua.

“Kwa hiyo kuna jambo linaweza likasemwa siyo kweli, siyo sahihi, lakini kwa sababu limesemwa na mkubwa, kiutumishi, kiungwana, maadili ya kitaaluma ya utendaji kazi ndani ya Serikali yanakuzuia wewe kufafanua.




20210608_114020.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi iliyotolewa na wanawake wakati wa mkutano wake kwa ajili ya kuzungumza na wanawake unaofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo.
20210608_114210.jpg
 
“Makatibu tawala 26 hapa ndipo nilifanya vizuri zaidi na sijui kama kuna eneo nitafanya vizuri zaidi ya hapa, makatibu tawala kati ya 26, 12 ni wanawake ni sawa na asilimia 46 kwenye eneo hili tunasogea kwenye asilimia 50, labda uteuzi wa pili kutakuwa na 50 kwa 50.” Rais Samia Suluhu Hassan.
20210608_114310.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom