Makapuku Forum

Makapuku Forum

SOUTH AMERICA] Mabishoo wa Kibrazil wanaongoza msimamo wa kufuzu World Cup kwa Amerika Kusini

Mpaka sasa hawajapoteza mchezo wanazidi kukiwasha Mafundi
20210606_142751.jpg
 
RACISM] Mwanasoka Kinda Seid Visin aliewahi kucheza timu za vijana AC Milan amejiua baada ya kubaguliwa huko nchini Italia

Seid kabla ya kuchukua maamuzi ya kujiua aliandika ujumbe kutokana na maamuzi yake, ujumbe ulisomeka ifuatavyo;

"Sikuja nchini Italia kwa kupenda bali nilichukuliwa kutoka nyumbani Ethiopia na wazazi wawili wa Kiitaliano (Adoption) wakanileta huku kama Mtoto wao"

"Mwanzoni maisha nchini Italia yalikuwa mazuri na kila Mtu alinipenda ila mambo yalianza kubadilika punde baada ya kupata ajira ya kufanya kazi hotelini"

"Wateja walisusia huduma yangu, wengi niliowahudumia walinifukuza kama Mbwa, huko viwanjani pia kila siku ilikuwa ni ubaguzi dhidi ya rangi yangu na Uafrika wangu"

"Nilitengwa kila sehemu, haswa Watoto wa Kiitaliano ambao hawana kazi ila Mimi sikuwahi kuchagua kazi, hivyo nimeamua kukatisha maisha yangu kwakuwa sina wa kumlilia wala wa kunisaidia"

Maandishi kwenye kikaratasi yalisomeka hivyo, ametangulia akiwa na umri wa miaka 20 tu

REST IN PEACE SEID
20210606_142851.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameagiza korosho zote zinazozalishwa katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi zisafirishwe kupitia badari ya Mtwara kwani Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika bandari hiyo kwa kuikarabati na kuipanua.

Amesema hayo leo Jumapili Juni 06, 2021 wakati wa kikao na wadau wa zao la korosho kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Sea View, iliyopo mjini Lindi.

Amesema Rais Samia amewaagiza Viongozi wa Bandari wapitie tozo zote zinazowakwaza wasafirishaji ili kuwavutia kuitumia bandari hiyo———“tunataka wasafirishaji watumie Bandari hii kusafirisha korosho kuanzia na msimu huu"

Waziri Mkuu pia amesema wakulima wakubali kupokea pembejeo kulingana na mahitaji yao na watalipia kulingana na idadi ya mifuko waliyochukua na sio shilingi 110 kwa kila kilo kama inavyelezwa———“kila kilo ni gharama mno, lengo letu ni kuendelea kumpungumzia mzigo mkulima, msiogope kuchukua pembejeo”
20210606_183132.jpg
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama amewaelekeza Wataalamu wa Lishe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kushirikiana na TAMISEMI kuhakikisha kila Shule inakuwa na kibao maalum cha kupima urefu wa Mtoto ili kutambua mwenendo wa makuzi yake.

Ametoa maelekezo hayo leo Dodoma alipokutana na timu ya mradi wa boresha lishe kutoka WFP unaofadhiliwa na EU na kutekelezwa kwa miaka mitano 2017 hadi Juni 2021 Mikoa ya Dodoma na Singida.

Lengo la upimaji huo ni kuufuatilia udumavu wa Watoto na kubaini lishe wanayoipata majumbani ili kufanya ufuatiliaji———“Mtoto mwenye lishe duni na aliyedumaa tutambaini tu kupitia urefu wake, mkakati huu ni kwa Watoto wote waliomaliza muda wa Kliniki”

Waziri Mhagama ameiomba pia Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia SIDO na VETA kutengeneza vibao vya kupima makuzi ya Watoto kwa kila Mkoa.
20210606_183503.jpg
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzungumza na wanawake zaidi ya 10,000 mkoani Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, amesema hayo leo Juni 6, 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Mtaka amesema Rais Samia atazungumza na wanawake wa mkoa huo kwa niaba ya wanawake wote nchini katika ukumbi wa Jakaya Convertion, Jumanne ya Juni 8, 2021. Hata hivyo, ajenda ya mazungumzo hayo haikuwekwa wazi.

Amesema wanawake kwa uwakilishi wao wa makundi kutoka wilaya za Dodoma na maeneo ya karibu wamepewa mwaliko wa kushiriki kwenye mkutano huo.
20210606_183646.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom