Makapuku Forum

Makapuku Forum

“Reli ya kisasa/Standard Gauge Railway, Dar es Salaam – Morogoro (km 300) ujenzi umefikia 91%, Morogoro – Makutupora (km 422) ujenzi umefikia 61% na ujenzi wa reli Mwanza – Isaka umeanza ambapo Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 372.34 za ujenzi wa kilometa 341 za reli” ———Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
20210606_050307.jpg
 
“Ujenzi wa Meli MV- Mwanza (Hapa Kazi Tu) umefikia 74% na katika mwaka wa huu kuna mikataba 9 ambapo ujenzi wa Meli mpya 3 zitajengwa katika maziwa makuu, Meli mpya moja katika Bahari ya Hindi na pia kutakuwa na ukarabati wa Meli 5 katika Maziwa ya Victoria na Tanganyika”———Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
20210606_050440.jpg
 
Kutana na Malkia wa nguvu Nandy kwenye stage ya Nandy Festival 2021.. wote tunajua rangi nyekundu inamaanisha nini, hiki ni kipisi tu cha kazi ya Malkia huyu hapa Mwanga Center Kigoma usiku huu akiendelea kututhibitishia kwamba ukikomaa michongo inafanikiwa kama kwake Mtoto wa kike, Malkia mwenye Festival yake.
20210606_051831.jpg
 
Umati uliojitokeza kwenye show ya kwanza ya Nandy Festival 2021 Kigoma umemfanya Nandy ashindwe kujizuia kwa furaha baada ya kuweka video fupi iliyochukuliwa kwenye tamasha lake kutoka angani na kuandika ———> “Kigoma niko hapa natokwa machozi, sio rahisi ila mmenifuta jasho, Asanteni”
20210606_051945.jpg
 
Kanisa la SCOAN limethibitisha kuwa Mhubiri maarufu kutoka nchini Nigeria, Temitope Balogun Joshua maarufu T.B Joshua amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 57.

Taarifa za awali zinasema TB Joshua ambaye ni Mwanzilishi wa Kanisa hilo la Synagogue Church of All Nation (SCOAN) na Kituo cha Televisheni cha Emmanuel amefariki muda mfupi baada ya Ibada.

Taarifa ya Kanisa hilo imesema———“Mungu amechukua maisha ya Muhudumu wake TB Joshua kulingana na uwezo wake, amefariki akimuhudumia Mungu”
20210606_132817.jpg
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Malongo, ameutaka Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), kuhakikisha unaboresha huduma zake na kuongeza ufanisi kwa watumishi wake ili kuvutia wateja wao ambao wamekuwa wakilalamika kuhusu utoaji wa huduma zao.

Akizungumza katika uzinduzi wa karakana sita zinazohamishika (Mobile Workshop), vifaa stahiki vya kuchunguza ubovu wa magari pamoja na viti 33 vya wenye mahitaji maalum kwa ajili ya kusaidia abiria wanaovuka katika vivuko vyote nchini vinavyosimamiwa na Wakala huo.

Malongoamesisitiza kuwa licha ya Wakala huo kuwa na Karakana kila Mkoa lakini bado huduma zinazotolewa ndani ya karakana hizo haziridhishi hali inayopelekea Watu kuamini Wakala umebweteka kutokana na kukosekana kwa ushindani wa kibiashara na kuwa ni Taasisi ya Serikali pekee kwenye matengenezo ya magari———“75% ya niliowahoji walisema TEMESA wamebweteka na pia wafanyakazi wao kutokuendana na mabadiliko ya teknolojia”

Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle, amesema, ununuzi wa wa karakana zinazohamishika umelenga kusogeza huduma kwa wateja waliombali na karakana za mikoa na pia kutoa huduma ya matengenezo ya dharura yanayotokea maeneo yasiyo na karakana hasa magari na mitambo yanapokuwa safarini au kazini nje ya ofisi.
20210606_133214.jpg
 
Serikali ya Nigeria imesema itawachukulia hatua za kisheria watu watakaobainika kukiuka katazo la matumizi ya mtandao wa kijamii wa Twitter.

Juni 4, 2021 Nigeria ilitangaza kusitisha matumizi ya mtandao huo
baada ya Twitter kufuta ujumbe uliowekwa na Rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari kwa kukiuka sheria za mtandao huo.

Msemaji wa Serikali ya Nigeria amesema kuondolewa kwa ujumbe huo kulikatisha tamaa lakini sio sababu pekee ya kusimamishwa kwa muda kwa matumizi ya mtandao huo.
20210606_133323.jpg
 
Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Dunia (WB) imeidhinisha mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya Sh2.3391 trilioni kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi minne ya maendeleo.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Juni 6, 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na waandishi wa habari siku moja kabla ya kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Dk Mwigulu amesema mradi iliyopitiwa fedha hizo ni ya uboreshaji wa barabara za vijijini na fursa za kijamii (RISE), mradi wa kuimarisha mazingira ya ufundishaji na mafunzo katika taasisi za elimu ya juu (Heet).
20210606_142112.jpg
 
Mkazi wa Kongwa Agnes Chiloya akifurahia kupatikana kwa maji kijijjini kwake, kwani awali ilimlazimu kuamka Saa nane usiku kuwahi kuchota maji.

Serikali kupitia Wizara ya Maji imeanza kujenga visima katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.
20210606_142239.jpg
 
KATIBU mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesikitishwa na mauwaji ya raia kaskazini mwa Burkina Faso, maafisa wa Burkina Faso wamesema watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wenye msimamo mkali wa kidini wamewauwa watu wapatao 138 katika mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kufanywa tangu machafuko yalipozuka nchini humo mwaka 2015.

Stephane Dujarric msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, amesema, Guterres ameghadhabishwa na mauaji ya watu hao wakiwemo watoto 7.

Mauaji hayo yamefanywa na watu wasiojulikana katika kijiji cha Solhan kilicho katika mkoa wa Yagha eneo la Sahel nchini Burkina Faso.

20210606_142348.jpg
 
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umetamba kuwa, upo kwenye mipango mizito ya kukisuka upya kikosi chao kitakachofanya vizuri na kuandika rekodi mpya katika michuano ya Afrika, mwakani.

Katika kufanikisha hilo, uongozi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa klabu chini ya Mkurugenzi wa Uwekezaji ambaye pia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili, Injinia Hersi Said wamefunguka kujipanga vizuri kuhakikisha wanatimiza hilo.

“Kama utafanya tathimini basi utagundua kuwa kati ya wachezaji 16 ambao tumewasajili msimu huu, ni wachezaji wasiozidi watatu ndiyo ambao wameshindwa kuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi na pia ni kwa sababu mbalimbali.
20210606_142445.jpg
 
ANASTAAFU] Hii sura sio ngeni sana kwako, ni sura maarufu kwenye mechi za El Classico nchini Hispania

Lakini pia ni sura hii tuliiona kwenye fainali ya UEFA, Chelsea vs Manchester City, alisimama kama Mwamuzi wa kati

Anaitwa Mateu Lahoz, Mwamuzi bora kwa siku za hivi karibuni ametangaza rasmi kustaafu baada ya michuano ya EURO 2020
20210606_142651.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom