Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amekagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Nduli-Iringa na kuwataka TANROADS kufanya utafiti wa kwanini Wahandisi wazawa hawakutuma maombi licha ya Kampuni ya SINOHYDRO kutangaza kazi kwenye mradi huo.
Ujenzi wa mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 40 na unahusisha upanuzi wa njia ya kuruka na kutua ndege kuwa KM 2.1 na upana mita 30, ujenzi wa maegesho mapya ya ndege na njia ya mchepuko, kusimika taa kwenye njia ya kuruka na kutua ndege, jengo la zimamoto, jengo la kituo cha zimamoto, jengo la muda la abiria.
Panya wa kiume kutoka Tanzania, Magawa ambaye mwaka jana alitunukiwa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini Cambodia, anastaafu Mwezi huu.
Magawa alizaliwa Tanzania Nov 5,2014 akiwa na uzani wa KG 1.2 na urefu wa Sentimita 70, alipewa mafunzo na Shirika lisilo la Kiserikali la Apopo kutoka Ubelgiji lenye Makao yake Morogoro Tanzania na alipewa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini.
Wasimamizi wake wanasema Magawa mwenye umri wa miaka saba kwa sasa ameanza kupunguza kasi yake ya kutegua mabomu kwakuwa amezeeka na ni wakati wake wa kupumzika.
Shirika la Matibabu ya Wanyama la Uingereza lisilokuwa la kiserikali PDSA lilimtunza medali ya dhahabu kwa kujitolea kwake kuokoa maisha kupitia kazi yake ya kubaini mabomu hatari yaliyotegwa ardhini Cambodia, inadhaniwa huenda kuna hadi mabomu Milioni sita ya kutegwa ardhini katika Nchi hiyo ya kusini mashariki mwa bara Asia.
“Mwanafunzi Josephat John aliyekuwa anasoma kidato cha nne Shule ya Sekondari Kom iliyopo kwenye Manispaa ya Shinyanga alizua taharuki baada ya kujianika juani huku akiwa amevaa mabango yenye ujumbe wa kupinga kuchaguliwa masomo ya biashara (ECA) ambayo anadai hajawahi kusomea kwani yeye amesoma masomo ya Sayansi(PCB)”———TAMISEMI
“Mwanafunzi huyu amepata Div II:21 na masomo ya sayansi anayodai amesomea amepata DCC yenye jumla ya pointi 10, mwisho wa pointi za Wanafunzi waliopangiwa Tahasusi hii ni 8 sawa na BCC, hivyo huyu hajakidhi vigezo vya kuchaguliwa katika Tahasusi hii ya PCB kulingana na idadi ya nafasi zilizopo mwaka huu”———TAMISEMI
“Hata hivyo Mwanafunzi huyu hajapangiwa Tahasusi ya Biashara (ECA) kama anavyodai, bali amepangiwa kusoma Stashahada Maalumu ya Ualimu kwa Masomo ya Physicis na Hesabu katika chuo cha Ualimu Songea ambapo ni miongoni mwa Maeneo aliyochagua katika machaguo ya vyuo alianza na Ufundi, Afya kisha Elimu”———TAMISEMI
“OR TAMISEMI inaendelea kumtafuta mwanafunzi huyu ili iweze kufahamu nia na shida ambayo amekumbana nayo mpaka kufikia kufanya kitendo hiki, kama kuna mzazi au mlezi yoyote anahitaji ufafanuzi wowote awasiliane na kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 0735-160201 na 0262-160201“———-TAMISEMI
“Rais(Samia) ameshatoa msimamo wake wa uongozi kwamba ataendeleza mazuri yote yaliyofanywa na watangulizi wake (Marais Wastaafu) na waliotangulia mbele za haki na ataanzisha miradi mipya, Ndege 8 zipo na Ndege 3 zitafika wakati wowote kuanzia sasa”———Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.