Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mshambuliaji wa zamani wa Man City Raia wa Argentina aliyejiunga na FC Barcelona hivi karibuni Sergio Aguero ameondoka Man City kwa kugawa zawadi kwa staff wa timu hiyo ambao amefanya nao kazi kwa miaka 10.

Aguero kabla ya kuondoka aliamua kuchezesha bahati nasibu kwa staff wa Man City nani atamuachia Range Rover yake inayotajwa kuwa na thamani ya Pound 40,000 (Tsh milioni 130).

Bahati nasibu hiyo imefanyika na mshindi akapatikana lakini amewanunulia saa staff wote kama zawadi yake kwa kuishi nao vizuri.

Aguero ametajwa kununua saa 60 za brand ya Hublot au Tag Heuer ikitajwa kila moja kuwa na thamani isiyopungua pound 1000 (Tsh milioni 3.2)
20210603_170756.jpg
20210603_170812.jpg
20210603_170828.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo June 3 2021 Ikulu Dodoma amepokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame uliowasilishwa na Mjumbe Maalum na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda,Dkt. Vincent Biruta.

Katika ujumbe huo, Rais Kagame ametuma salamu za pole kufuatia kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli , amempongeza Rais Samia kwa kupokea kijiti cha Urais na amemhakikishia kuwa Rwanda ipo tayari kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania.

Rais Kagame amesema hali ya Rwanda ni shwari na ipo tayari kukuza zaidi uhusiano wake na Tanzania hususani katika utekelezaji wa miradi ukiwepo mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo na ujenzi wa Reli ya kisasa ya kuunganisha Jiji la Kigali (Rwanda) na Isaka (Tanzania) ambayo itasaidia usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es salaam kwenda Rwanda.

Rais Samia amemshukuru Kagame kwa kumtumia ujumbe huo uliojumuisha salamu za pole na pongezi na amemuhakikishia kuwa Tanzania ipo tayari kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Rwanda.
20210603_170951.jpg
20210603_171008.jpg
20210603_171024.jpg
 
UNAAMBIWA

Miti ni muhimu sana pia kwenye mazingira ya mijini kwani huwa inanyonya gesi ya kaboni iliyo hewani na kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, majani yake huchuja gesi zenye sumu zinazochafua hewa kama vile dioxide ya nitrojeni na dioxide ya sulfur, utafiti wa hivi karibuni uliofanywa Uingereza umeonesha kwamba baadhi ya miti ina uwezo wa kupunguza chembechembe za uchafu hewani kwa hadi asilimia 79.
20210603_172428.jpg
 
UNAAMBIWA

Mbali na kwamba miti inatupa kivuli inaweza pia kupunguza joto linapokuwa kali kwenye Miji na Inafanya hivyo kwa kunyonya mionzi ya jua na kutoa maji hewani kupitia majani yake, kawaida sehemu za mijini huwa na joto kali sana wakati wa kiangazi lakini utafiti wa mwaka 2019 uliofanywa Marekani ulionesha kwamba miti inapofunika asilimia 40 ya Mji inaweza kupunguza joto kwa nyuzi joto 5 wakati wa kiangazi.
20210603_172646.jpg
 
UNAAMBIWA

Kwenye kamusi ya Kiswahili tafsiri ya neno 'Uduanzi' ni "tabia ya kufanya ujanja wa kishamba, mambo ya zamani Watu walishayaacha huo ni uduanzi, mfano kukopa pesa alafu usilipe deni ni uduanzi tu, jambo lolote lisilo na maadili katika jamii ni uduanzi tu, kubadilisha Wanawake mara kesho huyu yule ni uduanzi.... "
20210603_172745.jpg
 
UNAAMBIWA:

Watafiti kutoka The University of California, Berkeley wanasema Mtu kukosa usingizi wa kutosha kunaweza kumfanya awe mpweke na anayejitenga na Watu wengine, vilevile kunaweza kumfanya akatamani kuwa pekee yake muda mwingi.
20210603_172859.jpg
 
"Ligi yetu imepanda hadhi tangu tuingie madarakani, tumekuwa wa nane Afrika, tumewazidi Nigeria na Algeria licha ya kwamba tukicheza nao Timu ya Taifa kupata matokeo imekuwa ngumu." - Rais wa TFF, Wallace Karia.
20210603_173019.jpg
 
"Baada ya Manji kupata matatizo na kuondoka, Yanga ilipita katika wakati mgumu, nimeshirikiana na Sanga kuisaidia Yanga. Mimi ni Coastal si Yanga, walikuwepo Tenga amecheza Yanga, Malinzi alikuwa Katibu Mkuu wa Yanga lakini hawakuifanyia Yanga kama nilivyofanya mimi."

"Ukienda mtaani utasikia watu watakwambia hakuna Rais wa TFF aliyeionea Yanga Sc kama Karia, lakini ukienda ndani ya TFF watakwambia hakuna mtu aliyeisaidia Yanga kama Karia, kama mkiwapata viongozi wasema ukweli, watawaambia

"Siwezi kuifanyia mabaya Yanga, hizi ni timu zinazoililetea heshima Taifa, mimi ninaheshimiwa huko nje kwa sababu ya Simba na Yanga. Sisi wenyewe hatutambui ukubwa na heshima wanaotupa hawa mabwana kwenye ukanda wetu huu, hizi timu naziheshimu sana."

Rais wa TFF, Wallace Karia
20210603_173116.jpg
 
MWANAFUNZI wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Iringa, Petronel Mwanisawa (22) amefariki dunia kwa kunyongwa na mpenzi wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanamshikilia mtuhumiwa, Prudence Patrick (21), ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho.

Kamanda Bwire amesema tukio hilo limetokea Juni 1, mwaka huu maeneo ya Kihesa.

Amesema siku ya tukio marehemu hakurudi nyumbani kwao jambo ambalo si kawaida yake, hivyo wazazi wake waliingiwa na hofu na kuanza kumtafuta.

"Marehemu alikuwa anaishi na wazazi wake, na huyu mtuhumiwa yeye alikuwa amepanga, Kwa hiyo siku ya tukio alitoka kwenda chuo, lakini mpaka usiku akawa hajarudi, ndipo wazazi walianza kupata wasiwasi, wakampigia simu rafiki yake lakini hawakufanikiwa," amesema Kamanda Bwire.
20210603_173326.jpg
 
TANZIA

Mwanamuziki mkongwe Ismail Issa Michuzi amefariki dunia asubuhi hii katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar alikokuwa akitibiwa maradhi ya tumbo.

Ismail, ambaye ni kaka yake mpiga picha maarufu na blogger Muhidin Issa Michuzi, amefariki akiwa na umri wa miaka 61.

Ismail atakumbukwa kuwa mmoja wa viongozi na waanzilishi wa bendi ya Dar International chini ya Marijani Rajabu na pia alihudumu kama katibu wa bendi toka mwanzo wake hadi mwisho.
20210603_173424.jpg
 
Pamoja na wasanii kumuunga mkono msanii mwenzao Diamond Platnumz katika kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kumpigia kura katika tuzo za BET alizochaguliwa kushiriki, baadhi ya wadau wanaona hastahili kuungwa mkono.

Wadau hao wamemkemea waziwazi kupitia mitandao ya kijamii wakidai kuwa hajalitumia vema jina lake la msanii mkubwa kukemea maovu, badala yake amekuwa akifanya mambo yake binafsi.

Baadhi ya wachangiaji suala hilo katika mtandao wa Twitter wamekwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa watawaunga mkono wasanii wa Nigeria anaoshindana nao kuwania tuzo hiyo katika kipengele cha ‘Best International Act’ wakiwamo Wizkid, Burna Boy, Emicida, Headie, Aya Nakamura, Youssoupha na Young T & Bugsey.

Hata hivyo mshindi wa tuzo hizo anachaguliwa na jopo la majaji 500 wa BET na hapatikani kwa kupigiwa kura.

Baadhi ya wasanii wamemuunga mkono wakitaka apigiwe kura, huku wengine wakimkumbusha ajiulize kwa nini watu wanahamasishana kutompigia kura (ingawa hakuna kura zitakazopigwa kutoka kwa wananchi katika tuzo hii).

Mwimbaji Ray C amemtaka Diamond kujiuliza kwa nini wakati huu wa tuzo za BET ndio mambo hayo yanatokea na sio kipindi cha nyuma ambapo ameshinda tuzo nyingi kubwa.

Ray C alidai kipindi cha katikati Diamond alikuwa msanii mwenye majivuno sana na kubeza wenzake, pia kitendo chake cha kucheka hadharani mara baada ya kuahirishwa tamasha la Fiesta Novemba 2018 ambalo linawahusisha wasanii wengine, ndipo alipotengeneza huo mpasuko unaonekana kwa sasa.
20210603_173630.jpg
 
Ni kitu gani huwa unaanza kufikiria kabla ya kuingia kwenye uhusiano au ndoa? Achana na kufikiria mwonekano wa mwenza wako, kipato, tabia ama kupima virusi vya Ukimwi, bali kuna la ziada unapaswa kulizingatia.

Hilo si lingine bali na kupima afya zetu kwa undani zaidi, ili mnapoingia katika ndoa muwe na uhakika wa kuepukana na changamoto za kiafya kwenu na hata vizazi vyenu.

Wataalamu wa afya wanashauri mbali na kupima VVU ni muhimu kufahamu makundi yenu ya damu, kupima homa ya ini aina ya B na C na vinasaba, ili kujihahakikishia mnakuwa na familia bora na yenye afya njema kwenu na kwa watoto mtakaowazaa.

Ili kufahamu kwa undani kuhusu umuhimu wa kupima afya kwa kina kabla ya kuingia katika uhusiano au ndoa na ni magonjwa yapi wenza wanaweza kuepukana nayo, usikose kusoma Jarida la Afya kesho ndani ya gazeti la Mwananchi.

Umewahi kupima afya kabla ya kuingia katika uhusiano au ndoa?
20210603_173748.jpg
 
Kampuni ya mtandao wa simu ya Airtel Africa PLC imekubali kuuza minara ya mawasiliano ya Airtel Tanzania inayomilikiwa kwa ubia na kampuni mbili tofauti – SBA Communications Corp na Paradigm Infrastructure Ltd kwa $175 milioni (sawa na Sh400 bilioni).
Airtel imeeleza hayo jana Jumatano Juni 2, 2021 kupitia taarifa yake.

Wakati SBA ni mmiliki na mwendeshaji wa miundombinu ya teknolojia ya mawasiliano isiyohusisha nyaya (wireless communication), Paradigm, kampuni ya Uingereza unalenga kukuza, kumiliki na kuendesha miundombinu ya mawasiliao isiyo na nyaya katika baadhi ya masoko yanayokua.
20210603_173908.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imesharuhusu usafirishaji wa makinikia baada ya kuweka utaratibu mzuri wa ukusanyaji mapato.

Katika kipindi cha Maswali ya papo kwa hapo Bungeni leo, Waziri Mkuu amesema sheria imewekwa vizuri na kumekuwa na udhibiti wa kutosha ili kutokupoteza mapato.
Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Idd Kassim, mbunge wa Msalala (CCM) ambaye ametaka kujua Serikali ilizuia usafirishaji wa makinikia na nini kimesababisha kuanza tena kuyasafirisha kwenda nje ya nchi.

Waziri Mkuu amesema Serikali ilisitisha usafirishaji wa makinikia tangu 2017/18 kutokana na kubaini kulikuwa na wizi na udanganyifu.
20210603_174022.jpg
 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amewasimamisha kazi na kuagizwa wapangiwe majukumu mengine vigogo wawili wa Mamlaka ya Bandari (TPA) makao makuu na Bandari ya Kiwira Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Amechukua jukumu hilo kwa madai ya uzembe wa kutotoa taarifa za tatizo za ubovu wa meli ya Mv Mbeya II tangu iliporipotiwa mapema mwaka 2020 na kiongozi wa meli hiyo na mabaharia.

Waliosimamishwa ni kapteni wa meli kutoka makao makuu TPA, Abdalla Mwengamno na kaimu meneja wa Bandari Ziwa Nyasa, Hamis Nyembo.

"..., mlikuwa mnatambua changamoto ya meli hii tangu mwaka jana lakini hamkutoa taarifa jambo ambalo limehatarisha usalama wa wasafiri wanaotumia meli hiyo," amesema .
20210603_174143.jpg
 
MONDI: WENGI WAMEJARIBU KUNIUA

Wakati kukiwa na mjadala mkali juu ya kuteuliwa kwake kuwania Tuzo ya BET, staa wa Bongo Fleva, Diamondplatnumz amesema kuna watu wengi walijaribu kumuua, lakini walishindwa.

Diamond ameandika; “Walijaribu wengi kuniua kimuziki wakashindwa, wasanii wakongwe wamejaribu, wakashindwa, media ndiyo usiseme, naona na wanaharakati wa siasa wameanza, hakuna asiyejua ukweli, si lazima niseme, ila ukweli unajulikana, bila mimi Bongo Fleva isingekuwa hivi, mgumu kunishusha..”
20210603_174317.jpg
 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba, Adam Fimbo, amesema ni marufuku abiria kununua dawa mbalimbali hasa za kutibu magonjwa zinazouzwa kwenye magari na vyombo vingine vya usafiri na kwamba endapo mnunuzi na muuzaji watakamatwa watachukuliwa sheria.

Mkurugenzi huyo amesema kabla yakutumia dawa inapaswa Mtu kupata ushauri wa Wataalamu wa Afya wa ikiwa ni pamoja na kupata vipimo.

"Kwanza hilo haliruhusiwi kutangaza dawa kwenye vyombo vya usafiri lazima upate ushauri wa Daktari upime kwanza, natoa wito tena hairuhusiwi kuuza wala kununua”———Adam Fimbo
20210603_204437.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom