Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210602_071650.jpg
20210602_071716.jpg
 
UNAAMBIWA

Tafsiri ya ‘Kiruka mito’ kwenye kamusi ya Kiswahili ni Mtu asietulia mahali pamoja, tafsiri nyingine ni Mwanaume asieweza kuishi na Mwanamke mmoja kwa muda mrefu kwamba ana tabia ya kuoa na kuacha, kuoa na kuacha.
20210602_111151.jpg
 
"Tunaendelea na maboresho makubwa ya posta kwa lengo la kuongeza ufanisi na tija.

Tumefanya re-branding, tumetengeneza mifumo ya TEHAMA ili Posta iwe kidijitali, tumeanzisha Huduma centres ambapo huduma za Serikali zitakuwa zinapatikana na tunaimarisha biashara mtandao."
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Faustine Ndugulile
20210602_112142.jpg
 
Mbunge wa Momba (CCM), Condester Sichalwe aliporejea bungeni baada ya kutakiwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenda kubadili nguo akidaiwa alizokuwa amevaa awali hazikuwa sahihi kuvaliwa bungeni. Wabunge wenzake leo jioni Juni Mosi, 2021 wameomba mwongozo kwa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson wakidai Spika Ndugai alipewa taarifa za uongo na mbunge wa Nyang'hwale, Hussein Amar hali iliyosababisha kutoa uamuzi wa kumtoa katika ukumbi wa Bunge.
20210602_112326.jpg
 
“Nimewaambia wasimame hapa tuwaone Ma-RC na Ma-RAS wote ili tupate picha ya shughuli itakavyokuwa huko (Mikoani), mfano pale Mwanza nimesema ni kibiriti na petrol kwasababu Samike (RAS) ni mkimya lakini ana zake, yule mwingine RC Chalamila ni mlipukaji kwahiyo sasa sijui kutakuwaje huko lakini tunawaangalia”———Rais Samia Ikulu Dodoma leo baada ya kuwaapisha Viongozi
20210602_134259.jpg
 
“Kamanda Wambura (DCI) najua umefanya kazi nzuri sana, sana sana sana, Utumishi wako kwenye Jeshi la Polisi ni wa kutukuka, karibuni hivi tulikuwa na changamoto hasa kwenye Mkoa wetu wa Dar es salaam ilikuwa inaendelea pia kwenye Mikoa mingine tumekukabidhi umefanya kazi nzuri sana ndani ya muda mfupi hongera sana, na ndicho kilichonivutia nikuweke hapo sasa kuwa DCI”———Rais Samia Ikulu Dodoma leo baada ya kuwaapisha Viongozi

“Kamanda Wambura ni imani yangu utaendelea kufanya kazi yako vizuri kama ulivyoonesha huko nyuma lakini pia utaendelea kutupa mchango kwenye lile ambalo umeliacha sasa hivi, kwasababu kazi ya DCI haitokuchukulia muda mwingi sana nina imani utapata muda wa kutusaidia na huko”———Rais Samia
20210602_134432.jpg
 
“Kwa Iringa ambao Mkuu wa Mkoa ni Queen Sendinga (aliyekua Mgombea Urais 2021 kwa chama cha ADC) tuna exprience ya kilichotokea Mkoa wa Kilimanjaro tulipomuweka RC Anna Mghwira (aliyekua Mgombea Urais 2015 kwa chama cha ACT Wazalendo) Wakuu wake wa Wilaya akina Agness ambaye sasa nimekupandisha kuwa RC lakini kule mlipa shida sana Anna Mgwira”

Mghwira aliambiwa ———> “Wewe sio mwenzetu, kwanza ulitoka wapi, aliyekuleta hapa amekosea” <——— Rais huwa hakosei, tunawavuta hawa kutoka Vyama Vya Upinzani kwasababu nao ni Watanzania na kila tunayehisi ana mchango wa kutoa tutamuingiza”———Rais Samia Ikulu Dodoma leo baada ya kuwaapisha Viongozi
20210602_135124.jpg
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaonya wakuu wa wilaya wanaojaribu kuwakwamisha wapinzani wanaoteuliwa kuwa wakuu wa mikoa.

Samia amesema wapinzani wanaingizwa serikalini kwa kuwa na wao ni Watanzania na wana uwezo wa kufanya kazi.

Akizungumza leo Jumatano Juni 2, 2021 muda mfupi baada ya kuwaapisha makatibu tawala Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, Rais Samia amesema kila mpinzani atakayemuona ana mchango hatosita kumuingiza serikalini.
20210602_140216.jpg
 
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amekiri kuwa walikuwa na baadhi ya wagombea ambao hawakuwa wakikubalika kwenye maeneo waliyogombea nafasi mbalimbali ikiwemo ubunge na madiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Pia, amesema kwa sasa falsafa zake za kisiasa zinakwenda sawa na zile za aliyekuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Marekani, Thomas "Tip" O'Neil Jr.

Amesema O'Neil kupitia kitabu chake cha 'All Politics is Local' amesema siri za ushindi za chama cha siasa ambazo ndizo anazutimia kuongoza mapambano ya kushika dola nchini.

Amezitaja falsafa hizo kuwa ni chama kupata mgombea sahihi na nayekubalika kwa wapiga kura.

"Nikiri kuna maeneo mengi tulikuwa na wagombea sahihi, lakini kuna maeneo kadhaa tulikuwa na wagombea dhaifu, huo ni ukweli na haupingiki kwa sababu waswahili wanasema wali wa kushiba unaonekana kwenye sahani," amesema Mbowe.

Ametaja jambo la pili kuwa ni chama kuwa na ajenda ya kuwashawishi wanachi kukichagua, ambapo kwa upande wa Chadema, Mbowe amesema hakijawahi kukosa ajenda ya kushindana na Chama tawala-CCM.
20210602_140325.jpg
 
“Wakuu wa Mikoa waliowekewa Ma-RAS Wanawake hawa ni Wafanyakazi, Maofisa, Wasomi ni kila kitu kama mlivyo nyinyi, sasa mkienda huko mkawaambia ‘usinibabaishe Wewe si Mwanamke tu’, aliyekuambia nani Mwanamke ni tu!?, wewe ulizaliwa na nani!?, unatunzwa na nani?, aliyekufanya uitwe Baba ni nani!? mambo ya kwenda kudharauliana yasiwepo kafanyeni kazi”———Rais Samia Ikulu Dodoma baada ya kuwaapisha Viongozi
20210602_153030.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom