Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210525_054257.jpg
20210525_054543.jpg
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo amewateua Watangazaji wa Clouds Media Group Millard Ayo na kuwa Mabalozi wa Uhamasishaji Utunzaji wa Mazingira Nchini.

Waziri Jafo akiwa Dodoma amesema Mabalozi hao wameteuliwa kutokana na ushawishi wao kwa Jamii ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira na upandaji miti.

Mabalozi wengine walioteuliwa ni pamoja na Haji Manara, Antonio Nugaz, Nandy, Harmonize, Idris Sultan, Monalisa, Mbunge Esther Matiko, Mbunge Joseph Musukuma, Diamond Platnumz, Mwandishi wa Radio Uhuru Sakina Abdulmasoud na May Zumo. View attachment 1796837
Mbunge Esther Matiko
Mh na huyu yumo?
 
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amewasili leo mjini Cairo wakati akiendeleza juhudi za kuuongeza nguvu mpango wa kusitisha mapigano uliofikiwa kati ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza. Akiwa Cairo, Blinken atakutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi kabla ya kuelekea Jordan kwa mazungumzo na Mfalme Abdullah II.

Baada ya mazungumzo na rais wa Wapalestina Mahoumd Abbas katika makao yake makuu ya Ukingo wa Magharibi hapo jana, Blinken aliapa kuyajenga upya mahusiano ya Marekani na Wapalestina kwa kufungua upya ubalozi mdogo mjini Jerusalem pamoja na kuwapa msaada wa mamilioni ya dola kwa ajili ya ujenzi wa Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita.

Alikutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kusisitiza uungwaji mkono wa Israel kujilinda yenyewe dhidi ya mashambulizi ya maroketi kutoka kwa wanamgambo wa Hamas.
20210526_140151.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom