Mwaka 2017, Mzee wa miaka 70 Lawrence John Ripple kutoka Jiji la Kansas,Missouri nchini Marekani alivamia Bank akiwa na Silaha na akamlazimisha Muhudumu wa Benk ampe USD 3000 (Tsh. Mil 6.9) baadaye alikaa palepale akisubiri Polisi waje wamkamate akisema ni bora aende jela kuliko kuendelea kubaki na Mkewe mwenye gubu ambaye wanagombana kila siku na anampa stress.
Alikamatwa lakini baadaye Rais wa Benki na Muhudumu wa Benki (aliyempa pesa Mzee huyo) waliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwakuwa alionekana ni mwenye stress.
Badala ya kuhukumiwa kwenda Jela kwa kifungo cha zaidi ya miaka 20 kwa uvamizi wa Bank, Mahakama ilimuhukumu miezi 6 ya kifungo cha nyumbani ambako alikuwa anakukwepa wakiamini hiyo ni adhabu tosha kwake.
Ukitaka kununua gari nchini Japan ni lazima kwanza uthibitishe kwa Mamlaka kuwa unayo sehemu ya parking ambayo uta-park gari lako na kama utashindwa kuthibitisha hautoruhusiwa kununua gari.
Uthibitisho wa kwamba una parking hutolewa kupitia fomu maalum (cheti cha parking) ambayo kwa lugha ya Japan huitwa Chushajo Shomeisho na hutolewa kwenye Vituo vya Polisi.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amekabidhiwa rasmi ofisi leo na Mtangulizi wake Humphrey Polepole.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es salaam ambapo Shaka amemshukuru Polepole kwa kutenga muda wake na kuja kumkabidhi ofisi na kumuahidi kuendelea kushirikiana naye muda wote.
"Naomba niwasihi Viongozi wote waliopewa Mamlaka katika Serikali na Chama kwamba wana jukumu kubwa la kumsaidia Rais na Mwenyekiti wetu, Wadau wetu wakubwa ni Watanzania, bila ya kujali vyama vyao dini wala makabila yao”
Akiongea awali, Polepole amesema; "Katika chama chetu, tuna utamaduni wa kuachiana vijiti, leo namkabidhi Ndugu Shaka kijiti hiki akikimbize”
Watu takribani 3,000 wameukimbia Mji wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Goma kuelekea Rwanda leo Jumapili baada ya kutokea kwa mlipuko wa volcano katika Mlima Nyiragongo.
Balozi wa Rwanda nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Vincent Karega amesema ———“mipaka iko wazi na Majirani zetu wanakaribishwa kwa amani"
Serikali nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeagiza Watu waondolewe kutoka Mji wa mashariki wa Goma, baada ya kutokea mlipuko huo wa volcano katika Mlima Nyiragongo uliopo karibu na Mji huo wa mpakani.
Afisa mmoja katika hifadhi ya kitaifa ya Virunga iliyopo kwenye eneo ambako volcano imelipuka amesema hadi hii leo asubuhi tope la moto linalotiririka kutoka kwenye Mlima Nyiragongo limefika kwenye uwanja wa ndege wa mji huo wa Goma na kwamba hali inazidi kuwa mbaya.
Afisa huyo amesema anahofia kwamba tope hilo la moto (Lava) linaweza kufika hadi kwenye fukwe za ziwa Kivu na kusema mlipuko huo unalingana na ule uliotokea mwaka 2002 na amewataka Raia waondoke mahala hapo haraka.
Mwaka 2005 walitumwa wajumbe kutoka shirikisho la soka la Australia wakiwa na mwandishi mmoja kuja Afrika na kumlipa mganga mwingine ili kuwasaidia kuiondoa laana hiyo Wakafanikiwa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.