Angalia hii picha kwa makini kisha zunguusha simu yako juu chini halafu tuambie unafikiri picha halisi ni hiyo ya kwanza uliyoona au ya pili baada ya kuzunguusha simu yako?
Angalia hii picha kwa makini kisha zunguusha simu yako juu chini halafu tuambie unafikiri picha halisi ni hiyo ya kwanza uliyoona au ya pili baada ya kuzunguusha simu yako?View attachment 1796074View attachment 1796075
Nahodha wa Simba SC amepewa zawadi ya Tsh milioni 2.5 kwa kuwa mchezaji bora wa mechi (Man Of The Match) upande wa Simba SC katika mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs.
Bocco kwenye mchezo huo wa robo fainali alifunga magoli mawili katika ushindi wa 3-0 wa Simba dhidi ya Kaizer Chiefs lakini Simba walitolewa kwa aggregate ya 4-3, zawadi hiyo imetoka kwa mdhamini wao Emirate Aluminium
Mfanyabiashara Fred Ngajiro maarufu kama Fred Vunjabei amepitishwa na Baraza Kuu la UVCCM kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha kupitia kikao cha Baraza Kuu ambacho kimemalizika jana Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Kamati ya utekelezaji chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komredi Kheri James ilikuja na pendekezo la jina la mwenyekiti huyo wa kamati ambapo baadae alithibitishwa na wajumbe kwa kura nyingi za ndio, Katibu wake ni Rose Manumba na pia Baraza lilichagua Wajumbe wengine wanne wa kamati kutoka Bara na Visiwani.
Katibu Mpya wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa ni Victoria Charles Mwanziva ambaye jina lake limeridhiwa na Baraza Kuu Taifa kuelekea Mabadiliko ya Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa.
Hizi ni picha kutoka IKULU Dar es salaam zikionesha Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Mfanyabiashara Alhaji Aliko Dangote pamoja na Viongozi mbalimbali wa Tanzania baada ya kikao kilichofanyika IKULU leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo amewateua Watangazaji wa Clouds Media Group Millard Ayo na kuwa Mabalozi wa Uhamasishaji Utunzaji wa Mazingira Nchini.
Waziri Jafo akiwa Dodoma amesema Mabalozi hao wameteuliwa kutokana na ushawishi wao kwa Jamii ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira na upandaji miti.
Mabalozi wengine walioteuliwa ni pamoja na Haji Manara, Antonio Nugaz, Nandy, Harmonize, Idris Sultan, Monalisa, Mbunge Esther Matiko, Mbunge Joseph Musukuma, Diamond Platnumz, Mwandishi wa Radio Uhuru Sakina Abdulmasoud na May Zumo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amekabidhiwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Iringa Dr. Abel Nyamahanga.
Queen Sendiga ameahidi kufanyakazi kwa ushirikiano bila ya kujali tofauti ya Vyama na kusema ataifuata Ilani hiyo ambayo ni ya Chama kilichopo madarakani.
Queen ni Mwanachama wa Chama cha ADC na mwaka 2020 aligombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu kupitia ADC.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limethibitisha kutokea kwa vifo vya Watu wa sita wa familia moja waliofariki kwa kuzama Mto Ruvuma katika kijiji cha Mkalawa Wilayani Nyasa walipokua wanavuka kuelekea shambani kwa kutumia Mtumbwi uliotengenezwa na magome ya miti May 22, 2021.
RPC wa Ruvuma Simon Maigwa amesema mpaka sasa wamepata mwili mmoja ambao ni wa Mtoto wa mwaka mmoja na wengine bado wanatafutwa na timu ya uokoaji———-“Ule Mto maji yake yana rangi nyekundu na una mamba yawezekana wameliwa au wamehamishiwa eneo jingine”
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.