Makapuku Forum

Makapuku Forum

Akaunti zote za Wafanyabiashara zilizokuwa zimeshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na madeni ya kodi, zimefunguliwa.

Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma TRA Richard Kayombo amesema Mamlaka inaingia mikataba ya makubaliano na Wafanyabiashara wenye madeni ili walipe kwa utaratibu maalum.

Kayombo amesema Sheria inaruhusu TRA kushikilia akaunti ya anayedaiwa kodi lakini huwa ni uamuzi wa mwisho baada ya njia nyingine kushindikana.
20210522_193802.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amewateua Mabalozi 23 ambao uteuzi wao unaanza leo May 22,2021 na tarehe yao ya kuapishwa itatangazwa baadaye.

Miongoni mwa walioteuliwa ni Mwandishi wa Habari wa siku nyingi Nchini Tanzania ambae pia ni Mjasiriamali, Hoyce Temu.
20210522_194046.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amewateua Mabalozi 23 ambao uteuzi wao unaanza leo May 22,2021 na tarehe yao ya kuapishwa itatangazwa baadaye ambapo miongoni mwa hao 23 yumo huyu Togolani Mavura ambaye ni Msaidizi wa Rais Mstaafu Dr. Jakaya Kikwete.
20210522_194151.jpg
 
Mtawala wa Sussex mwanamfalme Harry amesema alikuwa akinywa pombe yenye thamani ya wiki moja kwa siku kujaribu kukabiliana na huzuni ya kifo cha mama yake.

-

Prince Harry pia alikuwa tayari kutumia dawa za kulevya "kupunguza hisia alizokuwa nazo za simanzi' zaidi ya muongo mmoja baada ya kifo cha mamake Princess Diana.

-

Harry alikuwa akiongea na mtagazaji maarufu wa televisheni Marekani Oprah Winfrey katika kipindi kipya cha kupeperushwa mtandaoni kuhusu afya ya akili.

-

Alizungumza pia juu ya wasiwasi na mashambulio ya hofu aliyokuwa nayo kama mmoja wa watendaji wakuu wa kifalme na aliyopitia wakati wa mazishi ya mama yake.

-

Diana, Princess wa Wales, alikufa katika ajali ya gari wakati akifuatwa na wapiga picha huko Paris mnamo Agosti 1997.
20210522_194627.jpg
20210522_194650.jpg
 
NIACHIE NIKUACHIE

Polisi wa Israel akikabiliana na Mpalestina baada ya kutokea tena vurumai karibu na msikiti wa al-Aqsa mjini Jerusalem leo, saa chache tangu kuanza kutekelezwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Palestina.
20210522_195515.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom