Makapuku Forum

Mwaka 1995, Sonny Graham (mgonjwa wa Moyo) akiwa amebakisha miezi 6 tu ya kuishi kutokana na tatizo la moyo lililokuwa likimsumbua, alipata bahati ya kupandikiziwa moyo wa Terry Cottle ambaye alijiua kwa kujipiga risasi kichwani.

Baada ya Sonny kupona, mwaka 1997 alikutana na Cherly Cottle (mke wa Terry Cottle) kwaajili ya kumshukuru kwa kukubali kumsaidia kupandikiziwa Moyo wa mume wake (Terry). Baada ya kukutana walijikuta wakiingia penzini na Sonny aliamua kumuoa Cherly Cottle(Mke wa Terry Cottte) na wakafunga ndoa mwaka 2004.

Miaka minne baadae Sonny na yeye alijiua kwa kujipiga risasi vile vile kama ilivyokuwa kwa Terry miaka 12 iliyopita na kumwacha Cherly akiwa mjane kwa mara nyingine tena.
 
Mwaka 1918 huko Marekani ulizuka ugonjwa hatari wa mafua ambao ulisababisha vifo vya watu wengi. Baada ya kuona mafua haya yanasambaa kwa kasi Serikali iliamuru watu wote kuvaa barakoa popote wanapokuwa.

Licha ya serikali kuwalazimisha watu kuvaa barakoa kisheria pamoja na kuwapeleka jela wasiovaa barakoa lakini kuna watu waligoma kuvaa barakoa.
 
Hakuna Uislamu wa aina hii
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…