Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
UNAAMBIWA Utafiti wa Mtandao wa Dove unaojihusisha na urembo Nchini Marekani unaeleza kuwa Wanawake wanaojikubali kuwa wao ni Warembo ni 4% pekee Duniani kote, wengine huwa hawajiamini hata wakisifiwa kuwa wao ni Warembo.
Utafiti huo unaendelea kusema kwamba ni 11% pekee ya Wanawake Duniani huwa wana uthubutu wa kujisifia hata mbele za Watu kuwa wao ni Warembo, wengine hata wakijikubali kuwa Warembo hukosa ujasiri wa kujisifia hadharani kuwa wao ni Wanawake wenye mvuto.
“80% ya Wanawake wanakubali kuwa kila Mwanamke ana kitu cha kipekee kinachomfanya avutie lakini mwenyewe hakioni, 72% ya Wanawake hujisika vizuri kuwa Warembo na 54% ya Wanawake Duniani wanakubali kuwa linapofika suala la urembo Wanawake wao kwa wao hukatishana tamaa na hata yule Mwanamke ambaye Wanaume watamuona Mrembo Wanawake wenzake husema ni wa kawaida tu”———Dove