Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210426_053232.jpg
20210426_053253.jpg
 
Katika kuadhimisha miaka 57 ya Muunganao wa Tanzania, Rais Samia Suluhu ametoa msamaha kwa wafungwa 5,001 waliokuwa wakikabiliwa na adhabu ya vifungo mbalimbali huku akiwataka Wafungwa wote walioachiwa huru kutumia vema mafunzo waliyopata Gerezani na waungane na Wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa huku wakiheshimu na kuzingatia sheria.

Miongoni mwa Wafungwa hao waliopewa msamaha na Rais leo, 1516 wameachiwa huru baada ya kupunguziwa robo ya adhabu na Wafungwa 3,485 wamepunguziwa robo ya adhabu badala ya punguzo la kawaida la theluthi moja na wataendelea kutumikia sehemu ya kifungo iliyobaki.
20210426_181417.jpg
 
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya zote nchini kuacha kugombana na kufanya kazi kwa ushirikiano kwakuwa hilo ndio lengo na madhumuni ya wao kuwepo katika maeneo yao.

Ameyasema haya wakati akizungumza na Sekritarieti ya Mkoa wa Tanga juu ya kutimiza wajibu wao wawapo katika maeneo yao ya kazi huku akitoa pongezi kwa RC, DC na Wakurugenzi wa Tanga kuwa hawana tabia za kugombana.

“Nawataka Ma-RC na Ma-DC kujitafakari, hatuwavumilia Viongozi watakaokuwa wanagombana na kuna mgogoro mmoja tumeupata unakuta RC anamkwamisha DC asifanye kazi vizuri, RC anagombanisha DC na Wananchi, hatutovumilia”———Ummy
20210426_181928.jpg
 
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema kwakuwa Sherehe za Muungano hazijafanyika mwaka huu kwasababu ya kifo cha Hayati Magufuli, fedha zilizotengwa kwa sherehe hizo zitagawanywa kwa Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar.

“Kwa busara za Mama yetu (Rais Samia Suluhu Hassan ) ameagiza fedha zilizokuwa zitumike kwa ajili ya Sherehe za Muuangano mwaka huu, zitagawanywa kwenda pande zote mbili za muungano kwa ajili ya shughuli za maendeleo”——— Dr. Philiph Mpango ameyasema haya kwenye Kongamano la Muungano, leo April 26, 2021 Chimwaga mkoani Dodoma.
20210426_182106.jpg
 
Zaidi ya Wanawake 85 Kenya wamelalamika kupata mabadiliko ya mzunguko wa hedhi baada tu ya kupata chanjo ya Corona iitwayo AstrazaZeneca, hii inakuja huku Nchi mbalimbali zikisema tafiti zaidi zinahitajika ili kujua madhara ya chanjo hiyo hususani kwa Wanawake.
20210426_184859.jpg
 
Mtandao wa Netflix usiku wa kuamkia leo umeanza kuionesha Filamu ya ‘SLAY’ ambayo Mwigizaji wa Tanzania Idris Sultan ameshiriki na kuigiza kama Kijana Tajiri anaetafuta Mwanamke wa kuoa mwenye mapenzi ya kweli.

Ni filamu ambayo imeonesha sehemu ya mtindo wa maisha wanayoishi baadhi ya Wanawake mjini kwa kutegemea kuwinda Wanaume lakini pia Wanaume wanaotamba na mali zisizo zao.

Director ni Adze Ugah na imeigiziwa Nchini Afrika Kusini ikiwahusisha Ramsey Noah, Idris Sultan, Enhle Mbali, Kaly Bossy Asante na wengine, ni filamu ambayo pia Netflix wameeleza inaweza kutazamwa na yeyote mwenye umri wa miaka 16+, link ya kuitazama moja kwa moja naiweka muda sio mrefu kwenye insta story.
20210426_185044.jpg
 
Mwanariadha Mang'suli Hussein (45) Mkazi wa manispaa ya Kigoma ujiji aliyeamua kukimbia kwa miguu kutoka Kigoma April 15 kuja Dar es Salaam kutazama Mechi ya Yanga Vs Simba May mwaka huu kwa Sasa amefika Itigi akiitafuta manyoni ikiwa ametumia siku 12 tangu aanze safari———“natarajia kutumia siku 18 kufika Dar”

Mwanariadha huyu anasema moja ya changamoto anayokutana nayo njiani inayomfanya kuchelewa safari yake ni Watu mbalimbali kutaka kupiga nae picha na mapokezi yanakuwa mengi kwa kila Kijiji.
20210426_185324.jpg
 
Rais wa Zanzibar, Dr.Hussein Mwinyi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Donald Wright ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kudumisha uhusiano baina ya Marekani na Zanzibar.
20210427_172956.jpg
20210427_173034.jpg
20210427_173055.jpg
20210427_173112.jpg
 
Club ya FC Bayern Munich ya Ujerumani imemtangaza Kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann (33) kuwa kocha wao mpya kwa mkataba wa miaka mitano akichukua nafasi ya Hans Flick anayeondoka Bayern, Nagelsmann ataanza kazi July 1 2021.
20210427_173321.jpg
 
Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema kuna Watu wamejitokeza mitaani ambao wanawadanganya Walimu ambao hawajaajiriwa kuwa wanatakiwa kutoa Tsh. Milioni moja ili wapate ajira kwa haraka kwani nafasi hizo hazitatangazwa na Serikali bali zitatolewa kisirisiri.

Waziri Ummy ameyasema hayo mapema hii leo wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika Shule ya Sekondari Zingibari Wilayani Mkinga, Tanga.

Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya uchunguzi ili kujua kama Watu hao wapo ndani ya Wizara au nje na kuwachukulia hatua za kisheria haraka.

Ummy pia amesema ajira hizo zikiwa tayari basi watatangaza kwa utaratibu unaotakiwa na kila mmoja anayehitaji atafuata utaratibu na hakuna atakayependelewa.
20210427_173515.jpg
 
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Pwani, Mhandisi Yudas Msangi, amesema Daraja jipya la Wami lenye urefu wa mita 510 na Barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 3.8 linalounganisha miji ya Chalinze – Pwani na Segera – Tanga litakamilika mwezi Septemba mwaka huu.

Mhandisi Msangi amemueleza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, mkoani Pwani wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi huo uliofikia 50.5% na kumuahidi kuwa kazi itakamilika kama ilivyopangwa.

Naibu Waziri Waitara amesema ujenzi wa Daraja jipya la Wami ni mkakati wa Serikali katika kuongeza ufanisi katika barabara ya Chalinze - Segera na kupunguza adha kwa abiria na wasafirishaji wanaotumia daraja la zamani lenye urefu wa mita 88.75.

“Kutokana na umuhimu wa daraja hili Serikali imeamua kujenga daraja jipya ili kuondoa adha katika daraja la zamani lililojengwa mwaka 1959 kutokana na kutokidhi mahitaji ya magari yanayopita kwa sasa, kuwa jembamba na lenye njia moja na Barabara zake unganishi kupita katika miinuko mikali na kona mbaya na hivyo kusababisha ajali za mara kwa mara”———Waitara
20210427_173814.jpg
 
Aliyekua Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaamu Polycarp Kadinari Pengo amemtembelea Mjane wa Hayati Magufuli, Mama Janeth Magufuli nyumbani kwake muda mfupi baada ya Kutoka Kanisani kwenye Misa Takatifu ya siku 40 tangu kifo cha Hayati Magufuli.
20210427_173951.jpg
20210427_174013.jpg
20210427_174033.jpg
20210427_174049.jpg
20210427_174110.jpg
20210427_174125.jpg
 
Mjane wa Hayati Magufuli, Mama Janeth Magufuli akiwa na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na Waumini wengine asubuhi hii katika Kanisa la ST. Peter’s, Dar es salaam, baada ya Ibada ya siku 40 tangu alipofariki Hayati Magufuli.
20210427_174412.jpg
20210427_174428.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom