Makapuku Forum

Makapuku Forum

Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam wameendelea na oparesheni ya ukamataji Wahalifu vinara wanaojihusisha na wizi wa pikipiki, magari na vifaa vya magari pamoja na Wauzaji na Wanunuzi wa vifaa hivyo.

Katika oparesheni hiyo Watuhumiwa 49 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wakiwa na pikipiki 10 aina mbalimbali na vifaa vyake, gari moja aina Toyota Noah likiwa limetolewa viti ambalo limekuwa likitumiwa na Wahalifu kubebea mali za wizi.

Watuhumiwa hao wamekamatwa pia na vifaa vya aina mbalimbali vya magari kama vile milango ya magari, side mirror, power windows, radio za magari, show za magari ya aina mbalimbali, taa za magari n.k.

“Majina ya Watuhumiwa kwa sasa yanahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi na oparesheni hii ya ukamataji inaendelea, Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa Mahakamani baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria”———Mambosasa

“Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inatoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na Wahalifu ili kuendelea kuimarisha Usalama wa Jiji letu, tunatoa onyo kwa wote wanahojihusisha na wizi wa magari,pikipiki na vifaa vya magari kuacha mara moja kwani tumejipanga na tutawafikia popote watakapokimbilia au kujificha”———Mambosasa
20210425_122218.jpg
20210425_122235.jpg
20210425_122255.jpg
20210425_122311.jpg
20210425_122327.jpg
 
Safari za ndege za Shirika la Ndege la Air Tanzania kutoka Tanzania kuelekea Guanzou Nchini China zinatarajiwa kuanza May 08,2021 mara moja kila baada ya wiki mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameyasema hayo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa China hapa Tanzania Wang Ken na kuongeza kuwa safari hizo zitaongezeka kwa kuzingatia muenendo wa COVID 19.
20210425_122535.jpg
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa mpya leo kuwa mwenendo wa Kimbunga hafifu Jobo unaonesha kuwa katika kipindi cha saa sita zilizopita Kimbunga Jobo kimepoteza nguvu yake wakati kikiingia Nchi kavu kusini mwa Mkoa wa Pwani na Dar Es Salaam usiku wa April 24, 2021.

Hali hii ilisababishwa na kuendelea kuimarika kwa upepo kinzani katika mwelekeo wa Kimbunga hicho, mawingu ya mvua yaliyokuwa yakiambatana na Kimbunga hicho yamesambaa Baharini karibu na maeneo ya kusini mwa Pwani ya Tanzania na Msumbiji.

Kwa sasa, Kimbunga hafifu Jobo hakipo katika Nchi yetu na hakuna madhara ya moja kwa moja yanayotarajiwa, hata hivyo masalia ya mawingu yanayoambatana na kilichokuwa kimbunga Jobo yanaweza kusababisha mvua katika baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Pwani.

Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na maelekezo na miongozo inayotolewa na mamlaka husika.
20210425_123101.jpg
20210425_123118.jpg
 
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Lusibilo Joel Mwakabibi baada ya kupokea malalamiko na tuhuma za mwenendo usiofaa, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kutoka kwa Wananchi, Viongozi na vyanzo vingine.

Kufuatia tuhuma hizo Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI kupeleka Timu za uchunguzi mara moja.
20210425_123245.jpg
 
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Nyangi Msemakweli kutokana na tuhuma za ubadhirifu, usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo na mahusiano yasiyoridhisha na Madiwani, Mkuu wa Wilaya na Viongozi wengine wa Wilaya ya Rukwa.
20210425_123452.jpg
 
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Lusibilo Joel Mwakabibi baada ya kupokea malalamiko na tuhuma za mwenendo usiofaa, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kutoka kwa Wananchi, Viongozi na vyanzo vingine.

Kufuatia tuhuma hizo Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI kupeleka Timu za uchunguzi mara moja.View attachment 1763658
Amefanya la maana
 
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Christopher Ngubiagai, amesema wamekamata Jahazi lenye zaidi ya Tani moja ya dawa za kulevya aina ya heroin katika eneo la Pwani ya Kilwa Kisiwani Wilayani humo.

“Raia wa Kigeni wasiopungua 10 walikua ndani ya Jahazi na mpaka sasa bado hajafahamika ni Nchi gani wanayotoka, wanaendelea kuhojiwa”———Ngubiagai

“Niwaambie tu Kilwa sio sehemu sahihi ya kupitisha vitu vya magendo kwakuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama imejipanga vizuri”———Ngubiagai
20210425_191910.jpg
20210425_191946.jpg
20210425_192002.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Leo April 25, 2021 ameshiriki katika mashindano ya 21 ya kuhifadhi Quran Tukufu Afrika, yaliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika mashindano hayo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi. (Swipe kuona picha nyingine)
20210425_192320.jpg
20210425_192345.jpg
20210425_192414.jpg
20210425_192450.jpg
 
Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati akiendelea na ziara yake Mkoani Mwanza leo amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuwaweka ndani (Mahabusu) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji mjini Mwanza (MWAWASA), Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini Mkoa wa Mwanza (RUWASA), Meneja wa Maji Vijijini Wilaya ya Sengerema, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Sengerema na Mkandarasi.

Aweso ameagiza Watu hao wawekwe ndani hadi kesho atakapokutana nao ofisi ya RC Mwanza kwa maamuzi zaidi.

Amefikia maamuzi hayo baada ya kukutana na changamoto kubwa ya kutokamilika, kutumia pesa kinyume na BOQ utekelezaji usiokidhi vigezo kwa mradi wa maji tegemezi kwa Wilaya ya Sengerema wa Busurwangiri ukiwa umetumia Tsh. Bilion 1.8 na Wananchi hawapati maji hivyo kupelekea kunywa maji ya mashimoni yenye tope.
20210425_192659.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom