Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210421_073903.jpg
20210421_073919.jpg
 
Maelfu ya Watu nchini Marekani, wanaendelea kushangilia hukumu ya kwanza, iliyomtia hatiani Polisi wa Kizungu kwa mauaji ya Mtu mweusi (George Floyd), katika historia ya Taifa hilo.

Hata hivyo, Rais wa Marekani Joe Biden amesema kutiwa hatiani kwa Derek Chauvin, kwa mauaji ya George Floyd, kunaweza kuwa hatua kubwa, katika vita dhidi ya ubaguzi wa kimfumo, lakini hakutoshi.

Biden aliyekuwa akizungumza katika Ikulu ya White House akiwa na Makamu wake, Kamala Harris, muda mchache baada ya Mahakama kumtia hatiani Chauvin, kwa mashitaka matatu ya mauaji, amesema Marekani haipaswi kutosheka na hukumu hiyo pekee, bali kusonga mbele hadi mfumo mzima, uwe umebadilishwa.

Viongozi hao wawili wamelitolea wito Baraza la Congress, kuyashughulikia haraka mageuzi ya Polisi, ikiwemo kuidhinisha muswaada wa sheria uliopewa jina la Floyd, aliyeuawa akiwa amegandamizwa goti shingoni, mwezi Mei mwaka jana.
20210421_104630.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taifa, Kesho Alhamisi April 22, 2021, taarifa hiyo imetolewa na Spika Ndugai leo Bungeni ambapo amewataka Mawaziri na Wabunge wote kuhakikisha wanakuwa Bungeni kesho.
20210421_125703.jpg
 
Maelfu ya Watu nchini Marekani, wanaendelea kushangilia hukumu ya kwanza, iliyomtia hatiani Polisi wa Kizungu Derek Chauvin kwa mauaji ya Mtu mweusi George Floyd———“hii ni mara ya kwanza kwa historia ya Marekani Polisi Mzungu kuwajibishwa kwa mauaji ya Mtu mweusi, haki imetendeka”
20210421_154601.jpg
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Grace Naledi Pandor kujadili mambo ya kuendeleza ushirikiano baina ya Nchi hizi mbili.
20210421_154729.jpg
20210421_154745.jpg
20210421_154801.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania na kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu biashara na uwekezaji hapa Nchini.

Viongozi hao wakiongozwa na Janson Huang wamempa pole Rais Samia kufuatia msiba wa Kitaifa wa Hayati Magufuli na kumpongeza kwa kupokea kijiti cha Urais katika Serikali ya Awamu ya Sita.

Wamehuhakikishia kuwa Wafanyabiashara wa China wapo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi na kuinua ustawi wa Wananchi kupitia uwekezaji mkubwa wanaokusudia kuufanya kupitia Kampuni zaidi ya 800 za China zilizo tayari kuwekeza Tanzania.

Viongozi hao wametaja maeneo ambayo Kampuni zao zipo tayari kuwekeza kuwa ni viwanda vya kutengeneneza simu, Dawa za Binadamu, magari n.k, Rais Samia amewashukuru kwa salamu za pole na pongezi na kuwahakikishia kuwa Serikali itashirikiana nao kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji.
20210421_154918.jpg
 
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa leo Aprili 21, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo zilizopo jijini Dodoma.

Pamoja na kuzungumzia ushirikiano baina ya pande hizo mbili,wamewakumbusha Wanahabari kuwa kipindi cha mpito kinachowataka Kuwa na Diploma kinaishia December 31, mwaka huu.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amewatoa hofu Wanahabari kuwa wasichukulie hasi Kanuni ya Sheria hiyo kwakuwa ina malengo chanya kwa Taaluma hiyo nchini.

Msigwa ametolea mfano wa Sheria hiyo na ukulima wenye kupata matokeo ambapo amesema———“Mtu anayelima muhogo, hawezi kulima tu bila kufuata kanuni bora za ukulima wa muhogo, hivyo itampasa kupata Elimu ya namna bora ya kulima ili kupata ama kuongeza tija”
20210421_180612.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania kuwa Serikali itafanya kazi changamoto zinazokwamisha uwekezaji ikiwemo upatikanaji mgumu wa vibali vya kazi, kodi, ucheleweshaji wa malipo, urasimu, kushughulikia changamoto zinazojitokeza kwa bidhaa zinazozalishwa nchini na zinazoingizwa kutoka nje ya Nchi na kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Rais Samia Suluhu ametoa kauli hiyo leo Ikulu ya Chamwino, Dodoma, wakati wa mazungumzo yake na Viongozi hao wanaokusudia kufanya uwekezaji kupitia Kampuni zaidi ya 800 za China zilizo tayari kuwekeza Tanzania kwa kufungua viwanda vya kutengeneneza simu, dawa za Binadamu, magari n.k

Viongozi hao wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania wakiongozwa na Janson Huang ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa palmvillage mikocheni wamempa pole pia Rais Samia kufuatia msiba wa Kitaifa wa Hayati Magufuli na kumpongeza kwa kupokea kijiti cha Urais katika Serikali ya Awamu ya Sita.

Wamehuhakikishia kuwa Wafanyabiashara wa China wapo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi na kuinua ustawi wa Wananchi kupitia uwekezaji mkubwa wanaokusudia kuufanya kupitia Kampuni zaidi ya 800 za China zilizo tayari kuwekeza Tanzania.
20210421_180922.jpg
20210421_180939.jpg
 
Rais Samia Suluhu amemteua Dkt. Jones Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) , Dkt Kilimbe anaendeleza wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
20210421_181118.jpg
 
Rais Samia Suluhu amemteua Hab Mkwizu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni za Magazeti ya Serikali (TSN), Mkwizu anaendelea na wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
20210421_181350.jpg
 
Rais Samia Suluhu amemteua Yahaya Mgawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti na Uvuvi Tanzania (TAFIRI),amemteua pia Prof. Erick Komba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Mifugo Tanzania akichukua nafasi ya Shirima ambaye amestaafu.
20210421_181550.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom