Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mchezaji Ibrahima Ndiaye wa Timu ya Taifa ya Senegal ya U23 amejikuta akiachwa na Timu ya Al hilal ya Sudan kwa kuvunjiwa mkataba baada ya kubainika kuwa na tatizo katika ini, tumemtafuta Dr Sizya kutoka voh_updates kutaka kujua tatizo la Ndiaye linatibika au ndio mwisho wa ndoto yake ya Soka.

“Ini ni kiungo muhimu sana ndani ya miili yetu, hufanya kazi zaidi ya 500, moja ya kazi ni kuchuja na kuondoa sumu kutoka kwenye damu”———Dr.Sizya

“Kutokana na sababu mbalimbali kama pombe kupita kiasi, sumu kwenye damu au maambukizi, ini hupata shambulizi na kushindwa kufanya kazi vizuri, hali hii huitwa HOMA YA INI au HEPATITIS, kuna aina 5 ya virusi vya Homa ya ini vi 5 (A,B,C,D,E), aina mbili za virusi (B na C ) ndizo hatari zaidi, Virusi hivi vya homa ya ini B na C husambaa kupitia damu, shahawa au maji maji mengine ya mwili”———Dr.Sizya

“Virusi hivi vina uwezo wa kusambaa na kuambukiza Mtu mara 100 zaidi ya Virusi vya UKIMWI, hii huenda ikawa sababu number moja ya kuachwa na Al hilal kwa kuhofia kuambukiza wengine, zipo dawa ambazo mgonjwa hupewa ili kukabiliana na tatizo hilo, (HCV antiviral drugs) lakini pia lifestyle modifications kama kuacha pombe kunaitajika kama ini limeharibika sana basi upandikizwaji unaweza kuhitajika”———Dr.Sizya
20210420_105801.jpg
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo, jana amekutana na kufanya mazungumzo na Madereva takribani 500 wa Kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara, waliokuwa wamegoma kwa siku 12, baada ya majadiliano Uongozi wa Kiwanda hicho umekubali kuwalipa stahiki zao ikiwemo mishahara na kuahidi kurejea kazini leo.

"Tutasimamia kuhakikisha Kiwanda cha Dangote kinaendelea na uzalishaji na kupata faida, lakini kinatekeleza wajibu wake kwa Watu wetu, hatutaki watanzania wanyanyasike katika Nchi yao”———KITILA

“Nchi hii ni huru, tutalinda haki za Madereva, nanyi pia mtulindie heshima yetu kwa Mwekezaji kwa kuwa Waaminifu”———KITILA
20210420_105953.jpg
20210420_105934.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe amefanya kikao kazi na Wadau wa ndani wa Elimu kwa lengo la kukuza ufaulu Temeke, kikao kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa( Iddi Nyundo).

Kikao hicho kimewakutanisha Wakuu wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari, Maafisa Elimu, Waratibu Elimu Kata, Wadhibiti Ubora wa Shule, Watendaji wa Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi wote.

Gondwe amesema lengo la kikao hicho ni kuwakutanisha pamoja wadau wote wa elimu wa ndani, ili kupeana uzoefu, kujadili kwa pamoja kuhusu Elimu, kusikiliza changamoto za Walimu, pamoja na kujadili kuhusu namna bora ya kuinua kiwango cha ufaulu.

Gondwe amewataka Wadau wote wa Elimu wa ndani kuifanya Elimu kuwa ajenda yao ya kila siku———“Ajenda ya Elimu iwe ni endelevu, mkitoka hapa mkawaambie Viongozi wenzenu kule kwenye kata kwamba kila mkikaa Elimu iwe ni ajenda yenu”.
20210420_110126.jpg
20210420_110156.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom