Makapuku Forum

Makapuku Forum

FT: Namungo FC 0-3 Raja Casablanca (Haddad 8’ Ngoma 14’ Habti 36’) CAFCC
20210421_183823.jpg
 
Rais Samia Suluhu amemteua Dkt Natu Mwamba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO), uteuzi wa Dkt.Mwamba umeanza leo April 19,2021.
20210421_183938.jpg
 
Spika wa Bunge Job Ndugai, amewataka Wabunge kutovaa tai nyekundu leo jioni wakati Rais Samia Suluhu atakapolihutubia Bunge na kusema kuwa rangi hiyo ni ishara ya mamlaka na inabaki kwa Kiongozi wa Nchi.... “atakayevaa tai nyekundu hatoruhusiwa kuingia Bungeni”
20210422_161316.jpg
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa kuhusu kimbunga Jobo kaskazini mwa Kisiwa cha Madagascar katika Bahari ya Hindi umbali wa Kilometa 930 na kilometa 1030 kutoka pwani ya Lindi na Mtwara.

“Uwepo wa kimbunga hicho unatarajiwa kusababisha ongezeko la upepo na mawimbi katika Bahari ya Hindi hususan katika Pwani ya mwambao wa Mtwara na Lindi”———TMA

“Mamlaka inaendelea kufuatiliia mwenendo na mwelekeo wa kimbunga Jobo kwa kuzingatia mifumo mingine ya hali ya hewa iliyo jirani zaidi na Kimbunga hicho ambayo inaweza kubadili nguvu na mwelekeo wa Kimbunga Jobo katika wakati ujao”———TMA

“Wananchi waendelee kuzingatia tahadhari ya upepo na mawimbi iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania katika maeneo husika, Mamlaka ya Hali ya Hewa itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi”———TMA
20210422_164829.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taifa, leo Alhamisi April 22, 2021, tayari gwaride la kumkaribisha Rais linaendelea muda huu kwenye Viwanja vya Bunge.
20210422_165141.jpg
 
“Miaka 6 imepita tangu niondoke kwenye Jengo hili la Bunge, leo ninayo furaha kurudi tena na kupata fursa ya kuhutubia Bunge ambalo kimsingi limenijenga, limenilea, limeninoa na kufanya uwezo wangu uonekane na kushika nafasi hii niliyonayo leo”———Rais Samia akihutubia Bungeni
20210422_165244.jpg
 
“Nawashukuru sana Marais Wastaafu wote kwa kunilea, uwezo wangu wa Uongozi uliibuliwa na Rais Karume aliyenipa nafasi ya Uwaziri, malezi haya yaliendelezwa na Dr.Kikwete aliyenipa Uwaziri na baadaye Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, nimshukuru pia Hayati Magufuli kwa kuniamini”——-Rais Samia akihutubia Bungeni.
20210422_165358.jpg
 
“Nimekuja kulihutubia Bunge baada ya Nchi yetu kupita kwenye kipindi kigumu, kama inavyokumbukwa March 17 Taifa letu lilipata msiba mkubwa wa kuondokewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Magufuli,hivyo tusimame kumuombea Mpendwa wetu”———Rais Samia akihutubia Bungeni

“Mapenzi ya Watanzania kwa Hayati Magufuli yalidhihirika katika kipindi cha maombolezo ambapo wengi walijitokeza kumuaga, namshukuru Mungu kwa kutupitisha salama kwenye kipindi cha mabadiliko ya Uongozi, dhamana hii ni kubwa na yenye mitihani mingi”———-Rais Samia

“Kuniamini kwa Hayati Magufuli kuwa Mgombea Mwenza wake kumeniwezesha leo hii kuwa Mwanamke wa Kwanza Tanzania kushika nafasi ya Umakamu wa Rais na hatimaye sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”———Rais Samia

“Niliwahi kusema na leo narudia tena kwamba Mimi na Hayati Magufuli ni kitu kimoja, kwahiyo mengi ambayo nimepanga kuyatekeleza ni yale ambayo yalielezwa na Hayati Magufuli wakati akilizindua Bunge hili”———Rais Samia
20210422_172240.jpg
 
“Mwaka jana Taifa letu lilifanikiwa kuingia Uchumi wa Kati ambapo Pato la Wastani wa kila Mtanzania limeongezeka hadi kufikia Dola 1080 zaidi ya kigezo cha Dola 1036, bila shaka ni mafanikio makubwa, jitihada zaidi zinahitajika ili kuongeza kasi ya ukuaji wa Uchumi”———Rais Samia Bungeni
20210422_172404.jpg
 
“Kila Mtu Duniani atapata umauti na kila mauti ina sababu, nimeona kwenye Mitandao taaarifa za uchonganishi, taaarifa tuliyopewa na Madaktari ya kifo cha Hayati Magufuli ni kutokana na tatizo la udhaifu wa Moyo aliloishi nalo kwa takribani miaka 10, nimekua naona mitandaoni wanasema fulani na fulani wamempa sumu, waaache hili”———Rais Samia Suluhu akihutubia Bungeni

“Wanaosema mitandaoni kuwa Hayati Magufuli alipewa sumu, mara fulani na fulani walitega kitu hiki, kama wana taarifa za maana waje tuwasikilize, lasivyo waache kuleta uchonganishi, kama wanafanya hivyo kwasababu hatutowapata warudi kwa Mungu wajiulize je wanafanya sawa!?”———Rais Samia

“Wanaoleta uchonganishi kwenye Mitandao nadhani wanafanya hivyo kwasababu wanajua hatutoweza kuwapata, wanatumia mifumo hiyo huko mingine ambayo bado hatujawa na uwezo wa kuwatafuta, lakini niwaambie tutawatafuta”———Rais Samia

“Taarifa zinazotolewa mtandaoni (kuwa Hayati Magufuli alipewa sumu), ni za kugonganisha Koo na Koo, Makabila na Makabila, wanaochanganisha kama wanajizatiti wanafanya hivyo kwasababu hatutowapata warudi kwa Mungu wajiulize je wanayofanya ni halali?, wao wangekubali?”———Rais Samia.
20210422_180447.jpg
 
“Nchi hii ni mara yetu ya kwanza kupata Rais Mwanamke, najua wapo Watu wenye wasiwasi kuwa kutokana na jinsia yangu sitoweza kuyatimiza niliyosema niwaondoe hofu kwamba Mungu hakuumba ubongo hafifu kwa Mwanamke na ubongo makini kwa Mwanaume, wote tulizaliwa sawa”———Rais Samia Suluhu akihutubia Bungeni leo

“Nawahakikishieni nimekuzwa kwenye Jamii sahihi na nina uzoefu wa kutosha kwenye shughuli za Serikali na CCM, najiamini kuwa ninao uwezo wa kuliongoza Taifa hili kwa kushirikiana na Watanzania wote katika ngazi tofauti”———Rais Samia
20210422_182024.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom