Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Majadiliano ya Serikali, Timu hiyo ndio inayofanya majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania, Serikali ya Uganda na Kampuni za uwekezaji katika mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima - Tanga.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linaendelea kuchunguza tuhuma za kusambaa picha za utupu zikimuhusisha Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Rajab Abdul Kahal maarufu kama Harmonize.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hadi sasa wamehojiwa Watu watano kuhusiana na sakata hilo na wapo nje kwa dhamana.
“Watuhumiwa hao ni Frida Kajala Masanja (36), Paula Paul Peter (18), Raymond Mwakyusa maarufu RayVanny (27), Claiton Revocuts maarufu Baba Levo (34), Catherine John na Juma haji (32)”———MAMBOSASA
"Watuhumiwa hawa wote walikamatwa, wakahojiwa na kwa vile dhamana ipo wazi wapo nje kwa dhamana na taratibu za upelelezi zinaendelea zikikamilika jalada litaenda kwa Wakili Mkuu wa Serikali na kama akiona kuna jinai watafikishwa Mahakamani”———MAMBOSASA
Club ya Simba SC leo imeingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Tsh Bilioni 2 na Kampuni ya Vunja Bei Group ambao unaipa mamlaka ya kuuza na kusambaza jezi na vitu mbalimbali vyenye nembo ya Simba SC.
Rais wa Chad Idriss Deby amefariki Dunia baada ya kupata majeraha kwenye mapambano dhidi ya Waasi, Deby amefariki ikiwa imepita siku moja tangu atangazwe kushinda Uchaguzi wa Urais wa Nchi hiyo kwa muhula wa sita.
Jeshi la Chad limesema Rais huyo kabla ya kifo chake aliungana na Wanajeshi ambao walikuwa mstari wa mbele kupambana na Waasi ambao walifanya mashambulizi wakijaribu kuuteka Mji Mkuu (N'Djamena) na huko ndiko alipopata majeraha, bado taarifa zaidi hazijatolewa.
Rais Deby alitangazwa na Tume ya Uchaguzi jana jioni kuwa Mshindi wa Urais kwa muhula wake wa sita madarakani, Deby ameliongoza Taifa hilo la Afrika ya Kati kwa zaidi ya miongo mitatu.
Alitangazwa Mshindi kwa 79% ya kura, licha ya Wapinzani wake Wakuu kuamua kususia uchaguzi huo wa Aprili 11, Waziri Mkuu wa Zamani, Albert Pahimi Padacke ameshika nafasi ya pili katika kinyang'anyiro hicho kwa kupata 10.32% na idadi ya waliojitokeza ilikuwa 64.81%.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) umekamilika kwa asilimia 100 ambapo kufikia August mwaka huu itaanza kazi kuanzia Morogoro hadi Pugu Dar es Salaam.
Majaliwa ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya mradi huo kuanzia kwenye Kituo cha awali cha Treni Tanzanite hadi Gerezani Dar es Salaam.
"Hata majirani watakuja kujifunza hapa wao wanaiita ya Treni ya Diesel, sisi tunaiita Treni ya Umeme, watakuja kujifunza hapa”———Waziri Mkuu Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA kilichoko Kibaha mkoani Pwani na ametumia fursa hiyo kuwahakikishia Wawekezaji wote kwamba Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano.
”Nimeridhishwa na kufarijika kuona hali ya kazi inayofanyika kiwandani hapa, niwahakikishie kwamba Serikali itaendelea kuwaunga mkono katika uwekezaji wenu, Rais aliona kazi yenu kupitia mitandao na akanituma nije nione”———MAJALIWA
Waziri Mkuu amesema hayo ndio mawazo ya Viongozi wa Tanzania tangu Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Pombe Magufu na Rais Samia Suluhu Hassan.
”Mmewekeza kwa wakati sahihi na kwenye Nchi sahihi na uwekezaji huu lazima utawaletea faida kwa sababu sera zetu za uwekezaji ni sahihi, niwahakikishie kwamba Serikali yetu imejipanga vizuri katika kuwahudumia Wawekezaji”———MAJALIWA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Yustino Ndugai leo April 20, 2021 Ikulu Jijini Dodoma.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.