Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais Philip Isdor Mpango Ofisini kwake Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo April 14, 2021.
20210414_123213.jpg
20210414_123239.jpg
 
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Nigeria Super Eagles Ahmed Musa (28) amefanya maamuzi ya kushtua kwa kuamua kujiunga na Club ya Kani Pillars ya Ligi Kuu Nigeria (NPFL) kwa kipindi chote cha msimu 2020/21 kilichobakia.

Musa kabla ya kurudi Nigeria alikuwa anaichezea Al Nassr ya Saudi Arabia (2018-2020), aliyojiunga nayo baada ya CSKA Moscow kwa mkopo akitokea Leicester City alikodumu (2016-2018), CSKA Moscow (2012-16)

Hii imewashtua wengi kwa sababu kwa umri alionao Musa ilikuwa sio rahisi kurudi Afrika mapema, walitegemea kuendelea kumuona Bara la Ulaya akicheza soka au Asia au Marekani inakoaminika wachezaji wengi wanafuata pesa na sio Kano Pillars inayoshika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Nigeria 2020/21
20210414_181536.jpg
 
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeelezea kusikitishwa na matukio na mienendo ya Wasanii wa Tanzania katika mitandao ya kijamii kwa kushamiri kwa vitendo vya matumizi ya lugha zisizo na staha, malumbano, kukashifiana na hata usambazaji wa taarifa na video zenye mwelekeo wa kudhalilishana.

Baraza limesema vitendo hivyo ni uvunjifu wa sheria na lime toa onyo na kukemea vikali mienendo na vitendo hivi na kuwataka wote wanaohusika kuacha mara moja tabia hiyo.

“Baraza litachukua hatua kali kwa Msanii yeyote atakaebainika kuendelea na kutenda vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria na kanuni zinazosimamia Sekta ya Sanaa, vitendo hivi vinarudisha nyuma juhudi za Serikali yenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa Wasanii, Wadau wa Sanaa na pato la Taifa kwa ujumla”———BASATA

“Baraza linaamini na kusisita kuwa Sekta ya Sanaa hususani Tasnia za Filamu na Muziki wa Tanzania tulipo sasa zinahitajika juhudi za Wasanii wenyewe kwa kujituma zaidi na kuongeza ubunifu iki kufikia tuzo kubwa za Kimataifa kuliko kudhani uvumi na"KIKI" zenye kuchafua ndio njia ya kupata mafanikio katika sanaa, Baraza linategemea kuona hali ya upendo, amani, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa Wasanii na Wadau wa Sanaa vinaendelezwa kama hapo awali”———BASATA
20210414_181721.jpg
 
"Kama ambavyo maelekezo ya Serikali yametolewa tunafuatilia kwa karibu sana suala la mabando au vifurushi ili virudi kama ilivyokuwa awali”———Dr. Jabir Bakari Kuwe, Mkurugenzi Mkuu TCRA akiwa Makao Makuu ya TCRA Dar es salaam leo

"Tuna-monitor na tunategemea muda si mrefu vitakamilika na vitarudi vyote kama ilivyokuwa awali, tunafuatilia kila saa na muda sio mwingi vitarudi kama zamani, maelekezo ni kwamba tunarudisha mabando yote kama mwanzo"———Dr.Kuwe
20210414_181925.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom