Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. John Kondoro kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) baada ya kumaliza muda wa kipindi cha kwanza, uteuzi huu umeanza April 15,2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Suzana Steven Chaula baada ya kutoridhishwa na utendaji wake, kuhusu Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Eng. Ronald Rwakatare, Waziri Mkuu amesema suala hilo atalikabidhi kwa Mamlaka ya uteuzi.
Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo leo Jumatatu, Aprili 19, 2021 wakati alipotembelea Kituo cha Kikuu cha DART-Gerezani ambapo alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Viongozi hao.
“Tangu Mtendaji Mkuu ameingia DART ana miaka mitano hakuna hata basi moja alilonunua, na anasema hana fedha kwani abiria hawasafiri si kila siku wanapigania kule Kimara na wote wanalipa unasemaje hakuna fedha ya kununulia magari!?”———MAJALIWA
Mtayarishaji Mkongwe wa Muziki Tanzania P Funk Majani amechaguliwa na Chama cha Umoja wa Watunzi na Watayarishaji wa Muziki Tanzania (TPCA) kuwa Mwenyekiti wao, akizungumza kupitia XXL ya cloudsfmtz leo Majani amesema kama Kiongozi anaamini atafanikisha kutimiza malengo ya umoja huo kwa faida ya tpca na Taifa kwa ujumla.
“Ukiwa na umoja unaweza kufanya michakato mingi ikiwemo kusaidiana upande wa Sheria, Elimu, Bima za Afya, fursa kuwafungulia milango nje ya Tanzania Producers Wadogo, uwezo wa kununua vyombo kwa bei nafuu, kufanya Festival au Show zetu , kutafuta soko la kuuza Muziki, mirabaha nk” ———MAJANI
“Mimi kwa sasa nina Familia yangu ambayo nina-play kama Baba na wanavyoendelea kufanya vinaathiri mpaka Familia yangu hii nyingine kwasababu inahusishwa nao, uchafu wao (Kajala na Paula) una reflect kwa hawa wengine, wamekosea wanatuvunjia heshima”———Mtayarishaji wa Muziki, majani kwenye XXL ya cloudsfmtz
“Maisha sio Instagram, vitu vya Kifamilia mnatatua Kifamilia naona Instagram wanasema eti ‘toa tamko’, nitoe tamko Instagram!?, masuala ya kuvujisha vujisha mavideo sio sahihi”———MAJANI
“Kama kuna ugomvi wa kimapenzi kwanini muweke mtandaoni, matatizo ya Familia huwezi kuweka kwenye mtandao, jiheshimu wengine watakuheshimu”———MAJANI
“Nilishawaambia tangu mwaka jana kwamba Mimi nilishajitoa, nilishanyoosha mikono kwa Mtoto (Paula), Mtoto anatafuta laana alishaniambia wewe sio Baba yangu, Kajala sio Familia yangu nilifanya uamuzi mbaya kuzaa na Mtu ambaye sio sahihi kuwa Mama, yanayoendelea kwa sasa hayanihusu, Mtu ameshakuambia wewe sio Baba yangu utafanya nini utamlazimisha?”———Mtayarishaji wa Muziki, Majani majani kwenye XXL ya cloudsfmtz
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Mara Warwick, Ikulu ya Chamwino leo April 19, 2021.
Club ya Tottenham Hotspurs imemfuta kazi Kocha wake Jose Mourinho na Ryan Mason sasa ndio atakiongoza kikosi hicho, Mourinho alijiunga na Spurs November 2019 kuchukua mikoba ya Mauricio Pochettino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taifa, Alhamisi April 22, 2021, taarifa hiyo imetolewa na Spika Ndugai leo Bungeni.
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Magesa Boniphace kuanzia leo April 20,2021 kupisha uchunguzi dhidi yake.
Waziri Ummy amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo kutoka kwa Wananchi na Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo Hamisi Tabasamu.
Tuhuma hizo zimeelekezwa kwa Mkurugenzi na baadhi ya Wakuu wa Idara za Halmashauri hiyo na zinaonesha kuwa Mkurugenzi kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara hizo wamekuwa wakifanya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za Umma zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Waziri Ummy amemuagiza pia Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kuunda Timu ya Uchunguzi wa tuhuma hizo haraka.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema tangu Mradi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ulipoanza Mabasi yamekuwa yakipungua kutoka 140 hadi 85——-“Watendaji wapo tu ofisini wanapigwa na AC (viyoyozi) wananchi wanaumia, hatuna sababu ya kumbakiza Mtu kama hafanyi kazi”
Amesema wakala huo ulianzishwa na Serikali kwa ajili ya kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi lakini Viongozi hao wameshindwa kusimamia vizuri na hivyo kusababisha mradi huo kutoendelea vizuri.
Waziri Mkuu amesema mapato mengi ya Serikali yamekuwa yakipotea kutokana na uendeshaji wa wakala huo———“kwanini ukatishaji wa tiketi haufanyiki kwa njia ya kielektroniki kwa asilimia 100? , tiketi zinauzwa kwa vifurushi”
“Haiwezekani Watu wanafanya ujanjaujanja tu wakuja na tiketi zao za mfukoni halafu wakimaliza anauza za POS (Mashine ya Kielektroniki ya Kukusanyia Mapato) na Wasimamizi wapo tu, kwanini mnauza tiketi kwa vifurushi hamtumii mashine kukata tiketi, Mnaua wakala huu kwa sababu wauzaji wa tiketi wanakuja na tiketi zao na nyingine mnazileta nyinyi”———MAJALIWA
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.