Makapuku Forum

Makapuku Forum

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Patrobas Katambi amesema taarifa ya mgomo uliodumu kwa siku 11 wa Madereva 500 wa Kiwanda cha Dangote Mtwara (wanaodai maslahi yao), imefika Wizarani tangu juzi na wameanza mchakato wa kuufanyia kazi mgogoro uliopo.

“Nilimuagiza Kamishina wa Kazi kwa ushirikiano na Uongozi wa Mkoa wa Mtwara kulishughulikia na kuleta taarifa kuwa kuna mambo wamekubaliana, kwakuwa limeibuka tena leo, niwaombe sana Madereva na Watanzania wote muwe na subira”———KATAMBI

“Tuipe Wizara nafasi ya kuliingilia na kuchukua hatua stahiki za kisheria haraka ili kulinda haki za Madereva, ajira na uchumi kwa faida ya Wafanyakazi, uchumi wa Nchi yetu na haki za Mwekezaji”———KATAMBI
#MillardAyoUPDATES

“Ondoeni shaka hakuna jiwe litasalia juu ya jiwe, haki ya kila mmoja italindwa na kupatikana, busara ituongoze kuwa watulivu Viongozi wenu tunalifanyia Kazi haraka”———KATAMBI
20210418_212305.jpg
 
Vilabu 12 vikubwa Ulaya vimeamua kutangaza rasmi kuanzisha michuano mipya ya European Super League, UEFA inapinga vikali michuano hiyo ambayo imepangwa kuwa inafanyika kuanzia August na May kwa kucheza nyumbani na ugenini.

Michuano hiyo itakuwa na jumla ya Timu 20 zitazotengeneza makundi mawili A na B yenye Timu 10, wanaomaliza nafasi tatu za juu kila Kundi wanafuzu robo fainali, nafasi ya nne na tano kucheza Play off huku fainali ikichezwa uwanja huru.

Timu tano kati ya 20 zitakuwa zinashuka kila mwaka na tano kupanda, vilabu vilivyoridhia kuunda michuano hiyo ni AC Milan, Inter, Juventus, Atletico, Barcelona, Real Madrid, Arsenal, Liverpool, Man City, Man Utd, Chelsea na Tottenham.
20210419_050718.jpg
 
20210420_031324.jpg
20210420_031341.jpg
20210420_031357.jpg
20210420_031419.jpg
20210420_031457.jpg
 
Rais Samia Suluhu amemteua Dkt. Mboni Ruzegea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ali Mcharazo ambaye amestaafu.

Rais Samia Suluhu amemteua pia Dkt. Revocatus Mushumbusi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ladislaus Nshumbemuki ambaye amestaafu.
20210420_032028.jpg
 
Rais Samia Suluhu amemteua Prof. Makenya Maboko kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), amemteua pia Ernest Mihayo kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Bahari Dar es salaam, baada ya wawili hao kumaliza muda wa vipindi vyao vya kwanza.

Rais Samia amemteua pia Prof. Esther Lugwisha kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kumaliza kipindi cha kwanza.
20210420_032119.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Richard Masika kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) akichukua nafasi ya Marehemu Prof. Peleka, uteuzi huu umeanza April 16,2021.

Rais Samia amemteua pia Prof. Joseph Msambichaka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) akichukua nafasi ya Prof. Manase Salema, uteuzi huu umeanza April 15,2021.
20210420_032214.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom