Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210418_054414.jpg
20210418_054445.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amefanya ziara ya kukagua miradi minne ya maendeleo Dar es salaam ambapo amemtaka Mkandarasi kutoka kampuni ya JASCO anaejenga Barabara ya Makongo kuhakikisha inakamilika kabla ya Mwezi October.

RC Kunenge amezitaka Taasisi za DAWASA na TANESCO kufanya kazi kwa ushirikiano na Mkandarasi huyo kwa kuondoa miundombinu ya maji na umeme iliyopita kwenye mradi ili Mkandarasi asipate changamoto yoyote kukamilisha mradi.

Kunenge amesema Barabara hiyo yenye urefu wa KM 4.5 ni moja ya Barabara muhimu Katika kutatua changamoto ya foleni kwenye Barabara ya Bagamoyo ambapo mradi huo umegharimu zaidi ya Bilioni 8.2.

Kunenge ametembelea pia ujenzi wa Barabara ya Madale kuelekea Wazo yenye urefu wa KM 6 inayogharimu Tsh. Bilioni 9.7 ambapo amemuelekeza Mkandarasi kutoka kampuni ya MECCO kukabidhi mradi mwezi wa tano mwishoni Kutokana na Barabara hiyo kuwa msaada mkubwa kwa Mabasi yaendayo Mikoa ya kaskazini yakitokea Kituo cha Mabasi cha Magufuli.
20210418_123634.jpg
20210418_123650.jpg
20210418_123715.jpg
 
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewasimisha kazi kupisha uchunguzi, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Mhandisi Tamimu Katakweba na Afisa Maji Bonde la Wami Ruvu Simon Ngonyani huku akiagiza Watumishi wengine waliokuwa vinara wa kueneza chuki na kuleta taharuki badala ya kufanya kazi kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Waziri Aweso amesema Mkurugenzi wa MORUWASA pamoja na tuhuma nyingine za kiutumishi lakini alisaini mkataba wa fedha nyingi na Wakandarasi bila kushirikisha Wizara na hata bila uwepo wa Katibu Mkuu kinyume na taratibu, huku Afisa wa Bonde akisimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya utumishi.
20210418_162915.jpg
 
Mgomo wa Madereva takribani 500 wa kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara, umefikia siku ya 11 leo huku Serikali ya Mkoa huo ikisema inaendelea kupambana ili kupata suluhu ya changamoto zinazowakabili Madereva hao ikiwemo maslahi bora ya kazi.

Licha ya juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Mkoa chini ya RC Gelasius Byakanwa Madereva hao wameendelea kusisitiza kuwa wataendelea na mgomo———“Tutaendelea kugoma mpaka aje Waziri wa Kazi, Rais, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais”
20210418_163225.jpg
20210418_163303.jpg
 
“Kuhusu Corona nilishaunda Kamati na punde nitakaa nayo ili tuone tunakwendaje, niwaombe Viongozi wa Dini muwahimize Waumini wenu kuchukua tahadhari za Corona mlifanya kazi kubwa Mwaka jana tulipotangaza ugonjwa huu, kasi ya Mwaka jana itumike sasa”———Rais Samia Suluhu kwenye Kongamano la Viongozi wa Dini leo Dodoma

“Mfumo wa maradhi haya (Corona) ni wa kupanda na kushuka, mara yapo mara hayapo, tupo kwenye hit 3 hatujui hiyo ya 4 itakuwaje ingawa Tanzania hatuna tishio kubwa la aina hiyo lakini yapo, kila hit inapokuja vidudu vinabadilika vinakuwa vya aina nyingine, Viongozi wa Dini wahimizeni Watu wajikinge”———Rais Samia
20210418_202739.jpg
 
“Naomba nijinukuu mwenyewe nilisema ‘huu ni wakati wa kuzika tofauti zetu’, ukiingia kwenye Mitandaoni ya Kjamii kuna uzandiki mkubwa sana kila Mtu anazua lake, kinachokuja kichwani anaweka kule na kuwaamisha Wananchi mambo kadhaa, Viongozi wa Dini mlipige vita hili”———Rais Samia Suluhu kwenye kongamano la Viongozi wa Dini Dodoma leo

“Viongozi wa Dini mkiongea yanabaki kwenye mioyo ya Watu, Sisi Viongozi wa Siasa tukiongea yanabaki kwenye vichwa vya Watu, vichwa vikichanganywa na mambo mengi yanatoka na huu ndio umuhimu wa Viongozi wa Dini kufanya kazi na Sisi, mtatusaidia kusema tunayotaka kusema”———Rais Samia

“Tukumbuke tupo kwenye Mwezi wa Toba (Ramadhan), naomba muendelee kuliombea Taifa letu, Nchi yetu haina Dini lakini Katiba ya Nchi yetu imetoa uhuru kwa Wananchi kuabudu Dini wanazotaka na hii imefanya kuwe na ushirikiano mkubwa, sio kila Nchi jambo hili linawezekana”———Rais Samia
20210418_202905.jpg
 
“Inasikitisha kuona kwamba Watu wanapiga ngoma mitandaoni lakini inachezwa Bungeni, mnalinganisha Magufuli na Samia hawa Watu ni kitu kimoja, nafuatilia mijadala yenu Bungeni haina afya kwa Taifa, mjikite na upitishaji wa Bajeti”———Rais Samia Dodoma kwenye Kongamano la Viongozi wa Dini Dodoma leo
20210418_203047.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom