Serikali imetangaza kuwa inatarajia kupandisha madaraja Watumishi wa Umma 90,000 Nchi nzima lengo likiwa ni kuonesha namna wanavyowajali lakini pia ikiwa ni kutimiza takwa la kisheria linalotaka Watumishi waliokidhi vigezo kupandishwa madaraja.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Licha ya kutoa ahadi hiyo, pia amewataka Watumishi kufanya kazi kwa weledi wakifuata taratibu, miongozo na maadili ya umma, huku akisisitiza kuwa Serikali haitomvumilia Mtumishi yeyote atakayekiuka miiko na sheria za kazi.
Msichana mmoja anayetambulika kwa jina Happy Nyasumo (18) Mkazi wa Kata ya Majimoto Wilaya ya Serengeti katika Mkoa wa Mara anashikiliwa kwa kosa kumuua Mume wake Bebe Mbogo (26) kwa kumkata kwa panga shingoni kwa madai halikuwa chaguo lake baada ya wiki mbili kupita tangu kufugwa kwa ndoa yao.
Happy aliolewa March 31, Mwaka huu kwa mahari ya ng’ombe sita lakini ndani ya wiki moja Happy alirudi kwao kijiji cha Mosongo na kuwaambia Wazazi wake kuwa huyo Mwanaume sio chaguo lake na warudishe ng’ombe zake, hata hivyo Wazazi walikataa na kumtaka arudi kwa Mumewe kwakuwa ndoa ni kuvumilia.
Akielezea tukio hilo Diwani wa Kata ya Majitoto Johannes Masirori amesema Aprili 14, 2021, saa 4 usiku baada ya Mume wake kulala fofofo Happy alimuua Mume wake kwa kumkata
na panga kali shingoni mara tatu, panga hilo Mumewe alilinoa kwa ajili ya kukatia miti ya kuchomea mkaa.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu amethibisha kushikiliwa kwa mtuhumiwa huyo na kutoa rai kwa Wananchi kutojichukulia sheria mkononi pia ameagiza hatua kali za kisheria zichukuliwe endapo uchunguzi utakapokamilika na kumkuta Msichana huyo na hatia.
Serikali imesema kuwa hakuna upungufu wa chanjo kwa akina Mama Wajawazito na Watoto chini ya miaka mitano na kwamba chanjo hizo zipo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na Hospiatali na kwamba zinatolewa bure bila malipo .
Akizungumza na Wataalamu wa Afya katika Kituo cha Afya Kaloleni, Arusha, Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu upungufu wa chanjo hazina uhalisia na kwamba chanjo zipo za kutosha katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini .
Dr. Subi amesema ni jukumu la Wataalamu wa Afya kuwahudumia Wataalamu na Watoto bila kikwazo ikiwa ni njia mojawapo yakupunguza na kuondoa kabisa vifo vya akina Mama na Watoto nchini.
Serikali imewaagiza Waganga Wakuu wote nchini kuweka Televisheni na vipeperushi katika vituo vya kutolea huduma za Afya hususani majengo yanayowahuduma akina Mama Wajawazito na kuweka vipindi vinavyoelimisha akina Mama juu ya afya za uzazi na jinsi ya kujikinga na magonjwa.
Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard wakati akizungumza na Wataalamu wa Afya katika Kituo cha Afya Kaloleni, Arusha.
“Naagiza Waganga Wakuu wote nchini kununua na kuweka Televisheni katika vituo vya kutolea huduma za afya na Hospitali ili kuwapatia fursa akina Mama kujifunza afya ya uzazi ikiwa ni njia ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito”———Dkt. Subi
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Innocent Bashungwa amekutana na Viongozi wa Vyombo vya Habari vya Taasisi za Dini nchini (TAREMA ) Kujadili juu ya changamoto ya leseni za usajili wa Vyombo vya Habari vya Taasisi zao, mkutano umefanyika katika Ukumbi wa TCRA.
Pamoja na mambo mengine Bashungwa amesikiliza maoni na changamoto mbalimbali ili kupatiwa majibu na ufafanuzi wa kisera utakaosaidia kuendesha Taasisi hizo muhimu zinazojenga Jamii kimaadili kupitia mafundisho ya kiroho na kiimani.
Bashungwa pia amewapongeza Viongozi hao kwa kazi kubwa waliyojitoa kuifanya ambayo imekuwa msaada kwa Taifa na ametumia nafasi hiyo kuwaomba Viongozi wa Dini kote nchini kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu pamoja na kuliombea Taifa letu.
Bashungwa ameielekeza pia TCRA kukukaa na Viongozi hao ili kufanyia kazi maoni yaliyowasilishwa kwake huku akiwaagiza kila mwaka kuwa na mkutano utakaowakutanisha na Wadau wao ili maamuzi yatakayofanyika yatumike katika mabadiliko na sera pamoja na uendeshwaji wa Vyombo vya Habari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isidor Mpango na Gavana wa Benki Kuu nchini Prof.Florens Luoga, Ikulu jijini Dodoma leo April 16, 2021.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, Edward Hoseah, ameshinda Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa kupata kura 293 kati ya 802 zilizopigwa akifuatiwa na Flaviana Charles mwenye kura 223, Shehzada kura 192, Albert Msando kura 69 na F. Stolla kura 17.
Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi leo Aprili 16, 2021 amekabidhi Ofisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambayo pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali kwa Gerson Partinus Msigwa ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dodoma.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.