Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Elibariki Kingu amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri na kumshukuru kufuatia Serikali anayoiongoza kutoa takribani Tsh. Milioni 770 kwa ajili ya miradi katika Jimbo hilo.

“Ninashukuru sana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ameanza tu majukumu ya Urais na tayari ametukumbuka Wananchi wa Singida kwa kutupatia Tsh. Milioni 500 za kujenga Kituo kipya cha Afya Iyumbu”———KINGU

“Ametupatia pia Tsh. Milion 50 za kumaliza Zahanati ya Mnang’ana Sepuka, Tsh Mil 50 za kumaliza Zahanati ya Nsonga ndogo Masweya na Tsh. Mil 50 za kumaliza Zahanati ya Mpugizi Mwaru ambayo Mwaka Juzi akiwa Makamu wa Rais alichangia Tsh Milioni 5 za kunua bati”———KINGU

“Pia ametoa Tsh. Mil 120 za kumaliza Maboma ya Msingi na Sekondari, Asante sanasana Mhe Rais kwa kuwajali Watu wangu wa Singida Magharibi”———KINGU
20210402_164707.jpg
 
Kamati ya Maadili TFF leo imetangaza kumfungia Mwenyekiti wa Yanga SC Fredrick Mwakalebela kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitano na faini ya Tsh Milioni 5 kwa makosa ya maadili.
20210402_164803.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linamshikilia Kusekwa Madaha( 27) mkazi wa kijiji cha Murongo Wilayani Kyerwa kwa tuhuma za kumpa ujauzito Mwanafunzi wa Shule ya Msingi mwenye umri wa miaka 15 anayesoma darasa la nne.

RPC Kagera Revocatus Malimi amesema Mwalimu Mkuu alibaini kuwa Mwanafunzi huyo ana ujauzito wa miezi minne na walipombana ndipo akamtaja Mtuhumiwa kuwa ndiye amempa mimba hiyo.
20210402_164824.jpg
 
Kutoka Dodoma, baada ya kula kiapo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, Jana Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu alifika katika Ofisi za Makao Makuu ya TAMISEMI na kupokelewa na Watumishi katika ofisi hiyo ambapo ameanza kazi kwa kutoa maelekezo na mwelekeo wake.

“TAMISEMI ni kubwa na wanasema ngumu lakini kwangu sio ngumu , kama ni ngumu maana yake mmeshindwa kunisaidia Mimi na Manaibu Waziri kutekeleza wajibu wetu, nampongeza Jafo amefanya kazi kubwa na nzuri ila tutaendeleza alipofikia”———UMMY

“Bado kuna mianya mingi na upotevu wa mapato ya Halmashauri ni wajibu wetu sasa kusimamia kuhakikisha wanakusanya ipasavyo na kudhibiti matumizi yao”——— UMMY

“Katibu Mkuu pitieni taarifa ya CAG na kuangalia zile Halmashauri 8 zilizopata Hati chafu lakini pia Halmashauri 54 zilizopata Hati za mashaka kujua masuala muhimu yaliyojitokeza katika taaarifa ya CAG ndipo hatua ziweze kuchukuliwa”———UMMY
20210402_164848.jpg
20210402_164913.jpg
20210402_164938.jpg
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amewafungia kwa muda wa miezi mitatu Madereva 10 wa Mabasi ambao wamekuwa wakikiuka Sheria ya Usalama Barabarani kwa kuendesha kwa mwendokasi.

Simbachawene ametoa kauli hiyo Dodoma ambapo ameliagiza pia Jeshi la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kuwachukulia hatua Madereva hao ikiwa ni pamoja na kuwapeleka Mahakamani kwa makosa hayo.

Waliofungiwa ni Madereva wa Mabasi ya Kampuni za Kimotco (Arusha- Musoma), Al Saedy (DSM- Kilombero), MB Coach (DSM - Arusha), Baraka Classic (DSM - Masasi), Maning Nice (DSM - Tunduma), Machinga (DSM-Mtwara), Ester Luxury (DSM- Moshi), NBC Classic (Tabora - Kigoma), Kilimanjaro Express (DSM- Arusha) na Kapricon (DSM - Moshi)

“Kwa Mamlaka niliyonayo nawafungia Madereva hawa kwa muda wa miezi mitatu, nawaagiza Wamiliki wa Mabasi haya ambayo Madereva wamekiuka Sheria ya Usalama Barabarani kuhakikisha wanachukua hatua stahiki kwa Madereva wao”———Waziri Simbachawene.
20210402_165001.jpg
 
Polisi Mkoani Kagera wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio la vifo vya Watu watatu wa Familia moja ambalo limetokea katika Kijiji cha Mayondwe Wilayani Muleba Mkoani humo chanzo kikidaiwa kuwa ni imani za Kidini.

RPC wa Kagera Revocatus Malimi amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Editha Martin (48), Sawia Sudi (25) na wa tatu ambaye ndiye Mtuhumiwa na Mhusika Mkuu wa vifo vyote Sudi Mwamadi (49) ambaye baada ya kufanya mauji ya Mke wake Editha na Mtoto wake Sawia na yeye alijinyonga juu ya mti kwa kutumia shuka.

RPC Malimi amesema uchunguzi wa awali umebaini kwamba chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliosababishwa na uamuzi wa Mke na Binti yake ambao mwanzo walikuwa Waislamu lakini wakaamua kubadili dini na kuwa Wakristo jambo lililopingwa na Mtuhumiwa na kusababisha kuwepo kwa ugomvi wa mara kwa mara mpaka kufikia hatua ya kuwaua kwa panga.
20210402_165017.jpg
 
“Taarifa ya Jeshi la Polisi niliyoitoa jana (pamoja na mambo mengine) ilisema tuna imani kama kila Mwananchi atafuata Sheria na kujiepusha na vishawishi vya kufanya uhalifu, Ibada ya Pasaka itamalizika salama na hatutegemei zile Sherehe na Shamrashamra tulizozizoea kipindi cha miaka ya nyuma kuwepo katika kipindi hiki, kwa bahati mbaya taarifa hiyo ilipokewa na tafsiri tofauti kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku Sherehe za Pasaka”- David Misime-SACP, Msemaji wa Polisi

“Jeshi la Polisi halijapiga marufuku Sherehe za Pasaka na ndio maana hata jana Ibada ya Sikukuu ya Alhamisi Kuu ilifanyika Nchi nzima bila bughudha yeyote na Askari wetu waliovaa sare za Polisi na waliovaa kiraia walikuwa doria kuhakikisha amani, utulivu na usalama unakuwepo”———POLISI

“Jambo ambalo hatutegemei kuliona ni zile shamrashamra kubwa kama vile Matamasha na Makongamano ya Pasaka na kwa bahati nzuri wanaoyaandaa kila mwaka kwa utu wao wa Kitanzania, hekima na busara zao hatujasikia wakitangaza maandalizi ya Matamasha hayo”———POLISI

“Ibada za Sherehe za Pasaka kwenye Makanisa, Sherehe za Kifamilia, Hitma, Familia kuungana na kwenda kutembelea sehemu mbalimbali na kusherehekea Pasaka hakuna aliyekataza ili mradi unachofanya kinaendana na kufuata utu, busara, hekima, Sheria , kanuni na taratibu za Nchi”———POLISI
20210402_170249.jpg
 
“Taarifa ya Jeshi la Polisi niliyoitoa jana (pamoja na mambo mengine) ilisema tuna imani kama kila Mwananchi atafuata Sheria na kujiepusha na vishawishi vya kufanya uhalifu, Ibada ya Pasaka itamalizika salama na hatutegemei zile Sherehe na Shamrashamra tulizozizoea kipindi cha miaka ya nyuma kuwepo katika kipindi hiki, kwa bahati mbaya taarifa hiyo ilipokewa na tafsiri tofauti kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku Sherehe za Pasaka”- David Misime-SACP, Msemaji wa Polisi

“Jeshi la Polisi halijapiga marufuku Sherehe za Pasaka na ndio maana hata jana Ibada ya Sikukuu ya Alhamisi Kuu ilifanyika Nchi nzima bila bughudha yeyote na Askari wetu waliovaa sare za Polisi na waliovaa kiraia walikuwa doria kuhakikisha amani, utulivu na usalama unakuwepo”———POLISI

“Jambo ambalo hatutegemei kuliona ni zile shamrashamra kubwa kama vile Matamasha na Makongamano ya Pasaka na kwa bahati nzuri wanaoyaandaa kila mwaka kwa utu wao wa Kitanzania, hekima na busara zao hatujasikia wakitangaza maandalizi ya Matamasha hayo”———POLISI

“Ibada za Sherehe za Pasaka kwenye Makanisa, Sherehe za Kifamilia, Hitma, Familia kuungana na kwenda kutembelea sehemu mbalimbali na kusherehekea Pasaka hakuna aliyekataza ili mradi unachofanya kinaendana na kufuata utu, busara, hekima, Sheria , kanuni na taratibu za Nchi”———POLISIView attachment 1741309

Danganya toto... jioni mtasikia watu kibao kukamatwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom