Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210402_204329.jpg
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es salaam, Lindi, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) kwa muda wa siku tatu kuanzia leo Jumamosi hadi Jumatatu April 05,2021, athari zinazoweza kutokea ni makazi kuzungukwa na maji na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji———“tafadhali zingatia na ujiandae”
20210403_201337.jpg
20210403_201319.jpg
 
Club ya Polisi Tanzania imewasimamisha Wachezaji wake sita kwa makosa ya utovu wa nidhamu, Wachezaji waliosimamisha ni Rashid Juma, Abdullaziz Makame, Pius Buswita, Tariq Seif, George Mpole na Abdulamalick Adam.
20210403_202159.jpg
 
Timu ya Madaktari wanane nchini Urusi wamepongezwa kwa ujasiri wao kufuatia kupambania maisha ya Mgonjwa aliyekuwa anafanyiwa upasuaji wa moyo licha ya jengo la Hospitali kuwaka moto.

Unaambiwa wakati Hospitali ikiendelea kuwaka moto kwa nje na hata kwa ndani kwenye baadhi ya vyumba huku Watu wengine wakikimbia ili kujiokoa, Madaktari hao waliendelea na kazi na wakafanikiwa kukamilisha upasuaji salama.

Kikosi cha Zimamoto kilifika na kuendelea na zoezi la kuuzima moto lakini Madaktari waliendelea na upasuaji licha ya kupewa ishara kuwa nje kuna ajali ya moto, walichofanya Watu wa Zimamoto ni kukipa kipaumbele chumba cha upasuaji kwa kuzuia moshi kuingia na kupambana ili moto usikifikie chumba hicho.
20210403_202329.jpg
20210403_202343.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom