Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais Samia Suluhu amemteua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akichukua nafasi ya Mwigulu Nchemba ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
20210331_163459.jpg
 
Rais Samia Hassan amemteua Balozi Hussein Kattanga ambaye ni Balozi wa Japan kuwa Katibu Mkuu Kiongozi akichukua nafasi ya Balozi Bashiru Ally ambaye ameteuliwa kuwa Mbunge, nafasi ya Katanga itajazwa baadaye.
20210331_164307.jpg
 
Rais Samia Suluhu amefanya uteuzi wa Wabunge wapya watatu leo, ambapo amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Bashiru Ally kuwa Mbunge huku nafasi yake ya Ukatibu Mkuu Kiongozi ikichukuliwa na Balozi wa Japan Hussein Kattanga.

Wabunge wengine walioteuliwa na Rais leo ni Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mbarouck Nassor.
20210331_164907.jpg
 
Rais Samia Suluhu amefanya uteuzi wa Wabunge wapya watatu leo, ambapo amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Bashiru Ally kuwa Mbunge huku nafasi yake ya Ukatibu Mkuu Kiongozi ikichukuliwa na Balozi wa Japan Hussein Kattanga.

Wabunge wengine walioteuliwa na Rais leo ni Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mbarouck Nassor.View attachment 1739591
Safi sana... tena hapo kamuheshimu sana.. Ilipasawa amtae kabisa...
 
Rais samia Suluhu amemteua aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe kuwa Waziri wa Uwekezaji na Naibu Waziri wake ni William Nasha, pia ameitoa Wizara hiyo kutoka Ofisi ya Rais na kuishusha chini ya Waziri Mkuu———“natoa miezi 3 nendeni mkaunde haraka hii Wizara, vinginevyo mnanionesha hamjui mnalotakiwa kufanya ndani ya Wizara”
20210331_171347.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Liberata Mulamula kuwa Waziri wa Mambo ya Nje akichukua nafasi ya Kabudi ambaye amehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ni Balozi Mbarouck Nassor.
20210331_173817.jpg
 
Rais Samia Suluhu amemteua aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara akichukua nafasi ya Geoffrey Mwambe ambaye amehamishiwa Wizara ya Uwekezaji.
20210331_174942.jpg
 
Rais Samia amemteua Pauline Gekul kuwa Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Abdallah Ulega ambaye amerejeshwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa Naibu Waziri———“nimemrudisha Ulega
Mifugo na Uvuvi kwasababu alikuwa kule, aende akamsaidie Waziri”
20210331_180648.jpg
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na imani nae na kumbakiza kwenye Wizara hiyo aendelee kutekeleza majukumu ya Uwaziri———“Asante sana Mh. Rais kwa kunibakiza Wizarani, namuahidi Rais wetu Samia nitafanya kazi kwa kujituma sana ili nisimuangushe yeye pamoja na Watanzania wote”

“Namshukuru Mh. Naibu Waziri Ulega kwa kunisaidia vyema sana kwa kipindi alichokuwepo nami Wizarani, namtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya kwa nafasi ya Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi”———BASHUNGWA

“Ninamkaribisha sana Mh. Naibu Waziri Pauline Gekul katika Wizara ili tuchape kazi na kumsaidia Rais wetu Samia kutekeleza dira na malengo aliyotukabidhi kuyasimamia kwa niaba yake pamoja na Watanzania”———BASHUNGWA
20210331_185011.jpg
20210331_185044.jpg
20210331_185108.jpg
 
“Namshukuru sana Mungu, Mimi sikuota wala sikutarajia kwamba Mimi Mtoto wa Masikini kutoka kwetu Buhigwe kule ningepata nafasi ya kuwa Makamu wa Rais, Asante sana Rais Samia nakuahidi kuwa Mzalendo kwa Nchi yangu”- Makamu wa Rais, Philip Mpango baada ya Kiapo Ikulu Chamwino Jioni leo

“Yuda alimsaliti Yesu kwa vipande vya fedha, sitokuwa kama Yuda, naahidi kukusaidia kazi Rais Samia na kutekeleza Ilani ya CCM uliyozunguka kote ukiinadi, nitume popote, wakati wowote nitakwenda”- Makamu wa Rais, Philip Mpango
20210331_205459.jpg
20210331_205328.jpg
20210331_205348.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom