Makapuku Forum

Makapuku Forum

“Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulipendekeza jina langu kuwa Makamu wa Rais, ni heshima kubwa sana, sikuwahi kuota, nimepigwa na butwaa”———Dr. Philiph Mpango
20210330_131007.jpg
20210330_131025.jpg
 
Rais wa Chama cha soka Congo DR Constant Omar (63) ametangaza kuwa hatogombea tena nafasi ya hiyo katika muhula mwingine baada ya kumaliza muda wake mwisho wa mwaka huu.

Omar ambaye ameongoza Chama cha soka Congo kwa miaka 18, amefikia maamuzi hayo ikiwa pia Timu ya Congo DR imeshindwa kufuzu AFCON 2021, Omar amewahi pia kuwa Makamu wa Rais CAF na Rais wa muda wa Shirikisho la soka Afrika (CAF)
20210330_131541.jpg
 
Club ya Man City imethibitisha kuwa Mshambuliaji wake Raia wa Argentina Sergio Aguero (32) ataondoka Man City mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake kuisha akiwa ameichezea Timu hiyo kwa miaka 10, ungependa kumuona wapi Sergio baada ya City?
20210330_132328.jpg
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania, kuthibitishwa kwa Dr. Mpango kuwa Makamu wa Rais kunamuondolea sifa ya kuendelea kuwa Mbunge wa Buhigwe———“naitaarifu Tume ya Uchaguzi (NEC) kuwa kiti cha Ubunge, Buhigwe kipo wazi”
20210330_142009.jpg
 
Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kesho ataapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla ya kuapishwa kwake itafanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kuanzia saa 9:00 alasiri.
20210330_171222.jpg
 
“Mh. Waziri Mkuu kama Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, katika kipindi hiki tunahitaji sana Waziri wa Fedha, kwahiyo na kwa hali yetu ilivyo basi utaangalia angalia huko tunahitaji sana Waziri wa Fedha ili mambo yaweze kwenda”- Spika Ndugai baada ya Mpango kuthibitishwa kuwa Makamu wa Rais Mteule na kupoteza sifa ya kuwa Mbunge
20210330_171347.jpg
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo March 30,2021 ameshiriki kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi, Rais Mstaafu Dr.Shein, Waziri Mkuu Majaliwa na Wajumbe wengine.
20210330_171519.jpg
20210330_171535.jpg
20210330_171551.jpg
20210330_171608.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Florencs Turuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma akichukua nafasi ya Dkt. Charles Msonde ambaye amemaliza muda wake.

Rais Samia pia amemteua Mhandisi Dkt. Richard Masika kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) akichukua nafasi ya Prof. Patrick Makungu ambaye muda wake umekwisha, mwingine aliyeteuliwa ni Dkt. Blandina Lugendo ambaye anakuwa Mwenyekiti wa Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) .

Rais Samia pia amemteua Paulina Nkwama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, kabla ya uteuzi Nkwama alikuwa Katibu Tawala Msaidizi (Elimu) Mkoa wa Kilimanjaro na anachukua nafasi ya Winfrida Rutaindurwa ambaye amemaliza muda wake.
20210330_185904.jpg
 
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo amethibitisha kumshikilia kwa mahojiano Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania (TPA) Deusdedit Kakoko na kusema baada ya upekuzi nyumbani kwake wamemkuta na USD Elfu 3 na Fedha za Kitanzania Tsh. Milioni 1.5

Mbungo amekanusha kuhusu picha na video zinazosambaa mitandao zikionesha fedha nyingi zinazodaiwa kukutwa nyumbani kwa Injinia Kakoko na kusema hawajakuta rundo la fedha nyingi Kama inavyosambazwa.

"Taarifa za kukutwa na pesa nyingi ambazo picha na video zake zinasambaa sio kweli, sio za kwake sio sahihi ni Watu nadhani ni Maadui zake wanajaribu kutengeza hoja ya kuonesha alikuwa na hizo fedha”- Mbungo

Kukamatwa kwa Kakoko kunakuja kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye alimsimamisha kazi na kuagiza achunguzwe.
20210330_190053.jpg
 
Mbunge wa Jimbo la Hai (CCM), Saasisha Mafuwe ametoa mapendekezo leo Bungeni, Dodoma akiomba Tanzania iwe na siku maalum ya kumkumbuka Hayati Dr. John Pombe Magufuli (Magufuli Day) kwa ajili ya kuyaenzi mazuri aliyoyafanya Hayati Magufuli enzi za uhai wake.

“Napendekeza kuwe na Magufuli Day ili kumuenzi JPM lakini pia hapa Dodoma kujengwe kituo Maalum cha kutunza kumbukumbu za Hayati Magufuli na kwenye mtaala wetu kwenye somo ambalo Hayati alilipendekeza la Historia ya Tanzania, kuwe na Historia ya Magufuli”———-Mbunge wa Hai, Mafuwe
20210330_190253.jpg
 
Makamu wa Rais Mteule, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa kuwaaaga rasmi baada ya kuteuliwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kupitishwa na Bunge kushika wadhifa huo, jijini Dodoma Leo,
20210330_195654.jpg
20210330_195713.jpg
 
Msafara wa Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Philip Mpango, ukiondoka katika viwanja vya Bunge Dodoma, baada ya Rais Mhe. Samia Suluhu kumteua na Bunge kumthibitisha kwa 100% kwa kura zilizopigwa na wabunge 363, leo Jumanne 30/03/2021.View attachment 1738954
20210330_200031.jpg
 
“Safari hii tutafika salama, Mama yetu Samia Suluhu uliandaliwa vizuri kuwa Rais wa Tanzania, kwa utumishi ambao aliufanya kwa kushirikiana na Mtangulizi wake Hayati Magufuli na sasa Mama anaifanya safari kwa kushirikiana na Dr. Mpango watakwenda vizuri”———Dr. Tulia Ackson Naibu Spika

“Tanzania iko salama, iko katika mikono salama, tutavuka salama na tutavuka salama huko tunakotaka kwenda na hatuna haja ya kuwa na shaka katika mambo yote haya tujifunze mambo mawili ambapo kwanza, kama Viongozi na kama Wananchi ni vizuri sana kuheshimiana kwasababu hatuifahamu kesho yetu”———Dr. Tulia Ackson

“Pengine wapo Watu walikuwa wanamtazama Makamu wa Rais kama ataendelea kuwa Makamu hivi na sasa ameshakuwa Rais na hili ni funzo kwetu sote kuheshimu kila Mtu umuonaye kwasababu huifahamu kesho yako”———Dr. Tulia Ackson

“Jambo la pili na la mwisho ni kwamba wanadamu hatutadumu milele, ni vizuri kujitahidi kuufanya utumishi wako wakati huu na usisubiri kesho maana kesho sio yako na sisi sote humu ndani ni Watumishi wa wale waliotuchagua hivyo tujitahidi kuwapa utumishi uliotukuka ili na sisi yumkini tuwe tumejifunza kwa maisha haya mafupi ya Dr. John Magufuli na sasa tukiungana kwa pamoja kumuunga mkono Rais wetu mpya Mama Samia”———Dr. Tulia Ackson
20210330_214656.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom