Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210331_083013.jpg
20210331_083039.jpg
 
Hapa ni Shule ya Msingi Muyama katika Kijiji cha Muyama Wilayani Buhigwe Kigoma aliposomea Dkt Philip Mpango, Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mitatu kuanzia 1968 hadi 1970 na kuhitimu darasa la saba, Mpango alihamishiwa katika Shule hii baada ya kusoma Shule ya Msingi Kipalapala kisha akahamia Kasumo na kumalizia hapa.

Stella Shayo ni Mwalimu Mkuu wa Shule hii, ameeleza historia kidogo ya Dkt Mpango kuhusu kusoma katika Shule hiyo na kuonesha darasa alilowahi kusomea kipindi akiwa darasa la saba.

"Shule hii imeanza mwaka 1954, hili darasa ndilo aliposomea hadi darasa la saba, baada ya kuwa Kiongozi aliwahi kufika hapa amejenga madarasa mawili na ofisi za Walimu, tunapambana sana kwa ajili ya kumuenzi iwe Shule ya mfano"———Mwalimu Mkuu
20210331_090708.jpg
20210331_090735.jpg
20210331_090759.jpg
20210331_090824.jpg
20210331_090901.jpg
 
Sarah Obama ambae ni Bibi wa Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama, amezikwa jana nyumbani kwake Kogelo, Siays Nchini Kenya, Sarah Obama alifariki juzi akiwa Hospitali ya Jaramogi Oginga.
20210331_091158.jpg
20210331_091221.jpg
20210331_091240.jpg
 
Ikulu ya Marekani imeliomba Shirika la Afya Duniani (WHO) kuanza awamu nyingine ya ufuatiliaji ili kujua kiini cha Corona baada ya WHO kusema wameshindwa kubaini chanzo hasa cha Corona licha ya kufanya uchunguzi wa kutosha wakiwa na Timu ya Wataalamu.

Marekani bado inaamini Corona ni virusi vilivyozalishwa maabara China na kusema China haikutoa Ushirikiano kwa Wataalamu na inaficha taaarifa muhimu lakini China bado inakana tuhuma hizo.
20210331_103617.jpg
 
Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, leo inatarajia kutoa hukumu dhidi ya Mfanyabiashara Abdu Nsembo (45) na Mke wake Shamimu Mwasha (41), ambao wanakabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

Inadaiwa kuwa Mei Mosi, 2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini DSM kinyume na sheria ya uhujumu uchumi walikutwa na dawa hizo.
20210331_111819.jpg
20210331_111848.jpg
20210331_111905.jpg
 
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi), imewahukumu kifungo cha maisha Mafanyabiashara Abdu Nsembo na Mkewe Shamim Mwacha baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kujihusisha na dawa za Kulevya aina ya Heroin .

Pia mahakama hiyo imetoa amri ya kutaifisha mali za Wahukumiwa ikiwemo gari aina ya Discover 4 ili liwe mali za Serikali, huku dawa hizo zikitakiwa kuteketezwa.

Hukumu ya kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2020, imetolewa Jaji Elinaza Luvanda baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kati ya Jamhuri na Utetezi na kujiridhisha kwamba Watuhumiwa wamekutwa na hatiani katika makosa mawili ya usafirishaji dawa za Kulevya.

Wawili hao walishtakiwa baada ya kudaiwa Mei Mosi, 2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini DSM kinyume na sheria ya uhujumu uchumi walikutwa na dawa hizo.



Dah hukumu kali sana masikini wale watoto wao jamani bora hata wangemwachia shamim tu nimesikia uchungu sana

Mungu azidi kuwatia nguvi wao pamoja na familia yao jamani
20210331_130234.jpg
 
Mahakama ya Mafisadi, licha ya kuwahukumu kifungo cha maisha Mfanyabiashara Abdu Nsembo na Mkewe Shamim Mwacha baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya kusafirisha dawa za Kulevya aina ya Heroin, pia imetoa amri ya kutaifisha mali zao ikiwemo gari (Discover 4), pichani ni gari ambalo Mahakama imeagiza litaifishwe na kuwa la Serikali.
20210331_135258.jpg
 
Mume wa Shamim Mwacha, Mfanyabiashara Abdu Nsembo akiwa katika chumba cha Mahabusu ya Mahakama ya Mafisadi akisubiri kupelekwa Gerezani, baada ya yeye na Mkewe kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin
20210331_152928.jpg
20210331_153000.jpg
20210331_153141.jpg
20210331_153205.jpg
 
Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, leo Jumatano Machi 31, 2021 ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla ya kuapishwa kwake imefanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan.
20210331_161822.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Mipango na Fedha akichukua nafasi ya Dr.Philip Mpango ambaye ameapishwa leo kuwa Makamu wa Rais.
20210331_161953.jpg
 
Rais Samia Suluhu amemteua Ummy Mwalimu kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI akichukua nafasi ya Selemani Jafo ambaye ameteuliwa kuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais.
20210331_162126.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom