Makapuku Forum

Makapuku Forum

“Nazungumza Kiswahili, Kingereza, Kifaransa, Kihaya, Kinyambo na Kisukuma jumla ni lugha sita ninazozungumza”———Matungwa Mutatina, Mkalimani ambaye alizua gumzo kwenye shughuli za kumuaga Hayati Dkt. Magufuli Dodoma
20210329_180458.jpg
 
“Baada ya changamoto ile kutokea kwenye mitandao ya kijamii nimeona vitu vingi vikifananishwa na Mimi na simu zilikuwa nyingi sana, kilichotokea Mimi sikuweza kumsikia vizuri mitambo ya sauti yangu ilikuwa inakata licha ya Watu wengine kusikia vizuri”———Matungwa Mutatina, Mkalimani aliyezua gumzo kwenye shughuli za kumuaga Hayati Dr.Magufuli Dodoma

Nilivyosikia kicheko cha Watu nilijua hili cheko la kwangu kuna sehemu nimekosea hivyo ikabidi nifanye Retrospective interpretation, ikabidi nitafsiri kwenda mbele huku kwa kurudi nyuma” ———Mkalimani

“Nilichotafsiri cha tofauti ni yale maneno ambayo nilikuwa nayasikia moja moja hivyo ikabidi niunganishe yale maneno machache ambayo nilikuwa nayasikia na nikapata kile nilichokisema”———Mkalimani
20210329_180605.jpg
 
“Sifa za Mkalimani ni kujua stadi za lugha (ujuzi), kujua misamiati ya kutosha kwenye lugha ambazo unazitumia kutafsiri, mfano kiswahili tunasema ‘umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu’, kwa kingereza tunawekaje sentensi hii?”-Matungwa Mutatina, Mkalimani aliyezua gumzo kwenye shughuli za kumuaga Hayati Dr. John Pombe Magufuli

Vipi kwa swali hili la Mkalimani, sentensi hii “umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu” kwa Kiingereza inapaswa kutafsiriwa vipi?
20210329_180809.jpg
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetupilia mbali tuhuma za Club ya El Merreikh ya Sudan kuwa Simba SC iliwahujumu wakiwa Dar es Salaam kwa madai kuwa vilitolewa vyeti kuwa Wachezaji wao wana Corona na kushindwa kucheza Game ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

CAF wametoa majibu na kueleza kuwa vipimo vilivyotolewa vyote vilikuwa halali na hakukua na hujuma zozote kama ambayo El Merreikh wanadai.
20210329_180933.jpg
20210329_180953.jpg
 
Mashirika ya misaada ya kiutu na ya haki za Binadamu yamesema maelfu ya Watu Manusura wa shambulizi la kigaidi kwenye Mji wa Palma, Jimboni Cabo Delgado Msumbiji wameokolewa jana.

Jumatano iliyopita Wanamgambo wenye itikadi kali walianza kufanya mashambulizi katika mji huo wenye hazina ya gesi na kulazimisha Watu 200 wakiwemo wa Wafanyakazi wa kigeni wa kampuni ya gesi kukimbilia kwenye Hoteli na kukaa zaidi ya siku tatu kabla ya kuokolewa.

Tangu Oktoba 2017 Wapiganaji wenye itikadi kali wamevizingira Vijiji na Miji katika maeneo mbalimbali ya Kaskazini mwa Msumbiji na kusababisha karibu Watu 700,000 kuyakimbia makazi yao.
20210329_181119.jpg
 
Mkuu wa wilaya ya Hai amesema Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameleta tumaini jipya wakati bado Taifa likiwa kwenye maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

"Katikati ya majonzi umeleta tumaini jipya, wakati wa saa ngumu umeinua tena mioyo ya Watu kwa faraja ya vitendo, lile swali la 'itakuwaje sasa' umelijibia Chamwino kwa kishindo, sauti thabiti imethibitisha kwamba hautoruhusu Nchi ichezewe na Watanzania wadharaulike, mtakapoiona ishara ya kwanza nanyi mtajua wokovu wenu upo karibu, kazi ya kwanza imethibitisha uthabiti na namna Rais Samia alivyofuzu kwa viwango vya juu toka kwa Mtu uliyemuita Mwalimu na Kaka mwenda zake JPM"———Sabaya

"Namtakia kila la kheri Mhe. Rais sasa ni shwari kuu katikati ya dhoruba, italazimu kumtambua Simba mpole lakini asiyetaka mzaha"——-Sabaya
20210329_220248.jpg
 
Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) limetupilia mbali tuhuma za Club ya El Merreikh ya Sudan kuwa Simba SC ya Tanzania iliwahujumu wakiwa Dar es salaam.

Madai yaliyotolewa na Club hiyo yalidai kuwa vilitolewa vyeti kwamba Wachezaji wake wana Corona hivyo kushindwa kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

CAF wametoa majibu na kueleza kuwa vipimo vilivyotolewa vyote vilikuwa halali na hakukua na hujuma zozote kama ambavyo El Merreikh wanadai. View attachment 1738151
20210329_220546.jpg
 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dr. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa 100%, Wabunge waliopiga kura ni 363 na wote wamepiga kura ya NDIO, hakuna kura iliyoharibika.
20210330_124444.jpg
 
“Tumezoea kuwanukuu Wanafalsafa mbalimbali Duniani, lakini leo nataka nimnukuu Mtanzania mmoja anayeitwa Pierre Liquid niseme Mama Samia ni Konki Fire na Mama Samia yupo juu yupo Mawinguni, na ndio maana amefanikiwa kumteua Mpango kuwa Makamu wa Rais”-Mbunge wa Kawe, Askofu Gwajima
20210330_124608.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom